Imefika wakati sasa Rais anahitaji kufanya interview na chombo cha habari kinachoaminika ili kuweka wazi masuala mbalimbali ya kitaifa

Korro

Member
May 2, 2012
17
65
Tangia Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli aingie madarakani sijasikia akifanya mahojiano ya moja kwa moja na chombo chochote cha habari chenye credibility kufafanua masuala mbali mbali ya kitaifa.

Ninakumbuka tu kulikuwa na press conference ilyofanyika ikulu ambao waandishi wa habari mbalimbali wa ndani na nje ya nchi walialikwa kumwuliza maswali mbalimbali. Press conference nyingine ninayoikumbuka ambayo ilikuwa yenye maswali rahisi rahisi ni ile nyingine ambayo ilifanyika Uganda alivyofanya ziara huko kumtembelea Rais Museveni.

Tokea Rais aingie madarakani imeshakuwa takriban miaka mitatu sasa na mwakani mwezi wa Oktoba tunatarajia kufanya uchaguzi wa kumchagua Rais na Wabunge. Nadhani imeshakuwa muda mwafaka sasa kwa Rais wetu mpendwa kufanya interview na chombo chochote cha habari na hata ikiwezekana chombo cha habari ya kimataifa kama BBC au CNN.

Nimeshangaa sana juzi kumwona Rais Maduro wa Venezuela ambayo nchi yake watu milioni tatu wamekuwa wakimbizi kutokana na hali mbaya ya uchumi lakini amekuwa na ujasiri wa kukabiliana na chombo cha habari kama BBC kwenye kipindi cha hard talk ambao waandishi wake hawaogopi kuuliza maswali magumu ambayo yanaweza yakawaudhi watawala.

Rais wetu mpendwa ataweza kukanusha au kujibu maswali mbalimbali nyeti ambayo watanzania wengi tunajiuliza kuhusu tuhuma nyingi zinazoelekezwa dhidi ya serikali yake. Sasa hivi wasemaji na watetezi wa serikali wamekuwa wakina Cyprian Musiba na Mbunge Joseph Msukuma ambao ni watu ambao hawana sifa wala credibility ya kuzungumzia masuala nyeti ya kitaifa. Wao kazi yao ni kufanya propaganda na kutukana matusi na kusema ukweli ndiyo wanayoichafua CCM na kuifanya chama hiki kikongwe kionekane chama cha kihuni. They are doing more harm than good.

Kwa hiyo kwa sisi wazalendo na tunaoipenda nchi yetu tungependa na kuomba kwa unyenyekevu mkubwa kumshauri Rais wetu mpendwa akubali kufanya interview ya ana kwa ana na chombo chochote cha kimataifa ili aweze kujibu tuhuma hizi zinazosambazwa dhidi ya serikali yake na kuweka mambo sawa pamoja na kuuelezea taifa letu na ulimwengu kwa ujumla ukweli kuhusu hali halisi ya nchi yetu Tanzania ilivyo.

Nawasilisha.
 
Tena hatutaki mahojiano na TBC tunataka BBC swahili ambayo ataelewa Lugha na kueleweka, au Sauti ya Amerika, au DW ndo vyombo vinavyoheshimika siyo hizo global TV, mara Tanzanite ya musiba,
 
Nashauri afanye mahojiano na Tim Sebastian kwenye kipindi cha Conflict Zone - Confronting the Powerful DW au afanye na Stephen Sackur wa HardTalk. Hata kama sipendagi kumsikiliza wala kumwona siku akikubali kuongea na any foreign media halafu watumie kiingilish, siku hiyo ntanunua kiepe na Pepsi na kumsikiliza kwa makini sana.
 
Tangia Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli aingie madarakani sijasikia akifanya mahojiano ya moja kwa moja na chombo chochote cha habari chenye credibility kufafanua masuala mbali mbali ya kitaifa.

Ninakumbuka tu kulikuwa na press conference ilyofanyika ikulu ambao waandishi wa habari mbalimbali wa ndani na nje ya nchi walialikwa kumwuliza maswali mbalimbali. Press conference nyingine ninayoikumbuka ambayo ilikuwa yenye maswali rahisi rahisi ni ile nyingine ambayo ilifanyika Uganda alivyofanya ziara huko kumtembelea Rais Museveni.

Tokea Rais aingie madarakani imeshakuwa takriban miaka mitatu sasa na mwakani mwezi wa Oktoba tunatarajia kufanya uchaguzi wa kumchagua Rais na Wabunge. Nadhani imeshakuwa muda mwafaka sasa kwa Rais wetu mpendwa kufanya interview na chombo chochote cha habari na hata ikiwezekana chombo cha habari ya kimataifa kama BBC au CNN.

Nimeshangaa sana juzi kumwona Rais Maduro wa Venezuela ambayo nchi yake watu milioni tatu wamekuwa wakimbizi kutokana na hali mbaya ya uchumi lakini amekuwa na ujasiri wa kukabiliana na chombo cha habari kama BBC kwenye kipindi cha hard talk ambao waandishi wake hawaogopi kuuliza maswali magumu ambayo yanaweza yakawaudhi watawala.

Rais wetu mpendwa ataweza kukanusha au kujibu maswali mbalimbali nyeti ambayo watanzania wengi tunajiuliza kuhusu tuhuma nyingi zinazoelekezwa dhidi ya serikali yake. Sasa hivi wasemaji na watetezi wa serikali wamekuwa wakina Cyprian Musiba na Mbunge Joseph Msukuma ambao ni watu ambao hawana sifa wala credibility ya kuzungumzia masuala nyeti ya kitaifa. Wao kazi yao ni kufanya propaganda na kutukana matusi na kusema ukweli ndiyo wanayoichafua CCM na kuifanya chama hiki kikongwe kionekane chama cha kihuni. They are doing more harm than good.

Kwa hiyo kwa sisi wazalendo na tunaoipenda nchi yetu tungependa na kuomba kwa unyenyekevu mkubwa kumshauri Rais wetu mpendwa akubali kufanya interview ya ana kwa ana na chombo chochote cha kimataifa ili aweze kujibu tuhuma hizi zinazosambazwa dhidi ya serikali yake na kuweka mambo sawa pamoja na kuuelezea taifa letu na ulimwengu kwa ujumla ukweli kuhusu hali halisi ya nchi yetu Tanzania ilivyo.

Nawasilisha.

Hivi akifanya mahojiano kuna kipi kitabadilika Tz? Hela zitamwagwa barabaran? Au utapewa ajira? Umaarufu wake ktk dunia sidhan kama umekuja kwa kuhojiwa na CNN au BBC. Ni sawa na wacheza mpira, ukicheza vizuri tutakufahamu kwa kukusikia au kukuona.
Na pia kila mtu na style yale ya kiuongozi. Wapo wanaopenda kila siku kuwa mbele ya waandishi na wengine hawapendi. Na isitoshe akitaka ataongea na wapiga kura wake ambai ni watz waliopo nchini.
Msimpangie cha kufanya.
 
Hawezi kukubali kuhojiwa, yeye mara nyingi amezoea kutoa amri na maelekezo na kulaumu wasaidizi wake.
 
Tangia Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli aingie madarakani sijasikia akifanya mahojiano ya moja kwa moja na chombo chochote cha habari chenye credibility kufafanua masuala mbali mbali ya kitaifa.

Ninakumbuka tu kulikuwa na press conference ilyofanyika ikulu ambao waandishi wa habari mbalimbali wa ndani na nje ya nchi walialikwa kumwuliza maswali mbalimbali. Press conference nyingine ninayoikumbuka ambayo ilikuwa yenye maswali rahisi rahisi ni ile nyingine ambayo ilifanyika Uganda alivyofanya ziara huko kumtembelea Rais Museveni.

Tokea Rais aingie madarakani imeshakuwa takriban miaka mitatu sasa na mwakani mwezi wa Oktoba tunatarajia kufanya uchaguzi wa kumchagua Rais na Wabunge. Nadhani imeshakuwa muda mwafaka sasa kwa Rais wetu mpendwa kufanya interview na chombo chochote cha habari na hata ikiwezekana chombo cha habari ya kimataifa kama BBC au CNN.

Nimeshangaa sana juzi kumwona Rais Maduro wa Venezuela ambayo nchi yake watu milioni tatu wamekuwa wakimbizi kutokana na hali mbaya ya uchumi lakini amekuwa na ujasiri wa kukabiliana na chombo cha habari kama BBC kwenye kipindi cha hard talk ambao waandishi wake hawaogopi kuuliza maswali magumu ambayo yanaweza yakawaudhi watawala.

Rais wetu mpendwa ataweza kukanusha au kujibu maswali mbalimbali nyeti ambayo watanzania wengi tunajiuliza kuhusu tuhuma nyingi zinazoelekezwa dhidi ya serikali yake. Sasa hivi wasemaji na watetezi wa serikali wamekuwa wakina Cyprian Musiba na Mbunge Joseph Msukuma ambao ni watu ambao hawana sifa wala credibility ya kuzungumzia masuala nyeti ya kitaifa. Wao kazi yao ni kufanya propaganda na kutukana matusi na kusema ukweli ndiyo wanayoichafua CCM na kuifanya chama hiki kikongwe kionekane chama cha kihuni. They are doing more harm than good.

Kwa hiyo kwa sisi wazalendo na tunaoipenda nchi yetu tungependa na kuomba kwa unyenyekevu mkubwa kumshauri Rais wetu mpendwa akubali kufanya interview ya ana kwa ana na chombo chochote cha kimataifa ili aweze kujibu tuhuma hizi zinazosambazwa dhidi ya serikali yake na kuweka mambo sawa pamoja na kuuelezea taifa letu na ulimwengu kwa ujumla ukweli kuhusu hali halisi ya nchi yetu Tanzania ilivyo.

Nawasilisha.
han mada yoyote zaidi ya fly over n dreamliner, mkinikia naa viwanda vilifeli.
 
Back
Top Bottom