Imefia wapi Big Results Now (BRN)?

Unko T

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
200
266
Natumaini tu wazima wa afya.

Muungwana husalimu, akidondokwa nguo huchutama!

Big Results Now almaarufu kama BRN au Matokeo Makubwa Sasa.

Wakati wa Bw. Kikwete ilikuwa inaimbwa na kupambwa kwa manukato ya Jasmine. Mpaka mpwa wangu mwenye miaka mitano alikuwa anaimba wimbo wa BRN.

Tufani ya mkuu mpya Kitalani ameziba midomo ya waimba kwaya wote wa BRN. Ghafla bin vuuuuu BRN kimyaaaaa.

Swali binafsi, kama BRN imezima mithili ya mshumaa upeponi, kwa nini walitumia mapesa kuipamba?

Alamsiki!
 
Kilimo kwanza nayo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom