Imefahamika: Wabunge wa Upinzani kuhamia CCM ni defense mechanism ya Stress za uchaguzi 2020

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
Habari ndugu;

Kumekuwa na wimbi kubwa sana la wabunge wengi wa upinzani toka Ukawa na pengine ambao wanahamia chama cha Mapinduzi CCM. Wengi wamekuwa na mawazo mengi juu ya hali hii na kuhusisha na vitendo vya rushwa kuwa wabunge hao wamenunuliwa au ni kuwepo kwa Lowassa na Sumaye ila hali haiko ivo. Mambo si hayo. Nitofauti kabisa. wabunge hawa wanahofu sana nafasi zao z ubunge kwenye uchaguzi ujao.

Wameona mvua za lasha lasha kwa uchaguzi mdogo wa udiwani wa juzi jinsi gani madiwani wa Ukawa walivoteketea na kuona kuwa mwaka 2020 ktk uchaguzi mkuu itakuwa balaa tena balaa mbaya.

Wameshaona kuwa hawatatoboa hata. Na wanaona wakiendelea kubaki ukawa kuwa hawataambulia kitu. Nafasi zao zitapotea hivi hivi. Wamejawa na hofu sana. Awajiamini tena kuwa watashinda. Ushindi kwao wanaoa ni 0%. Sasa wanaona yanini waendelee kubaki Chadema au Cuf nawakati wakihamia CCM na wakipewa nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM ushindi unakuwa 100%.

Wengi wameona madiwani wale walohamia CCM jinsi walivopokelewa kwa ufahali na kupewa na fasi na mpaka sasa wametoboa wamerudia nafasi zao za udiwani sasa kwa tiketi ya Chama Cha Mapunduzi CCM. Sasa wabunge wa ukawa aka Chadema wakilala wanaangalia ceiling board za room zao huku wakipiga mahesabu ya hatima yao uchaguzi 2020. Wanaona giza tena giza totoro hasa wanavyoona mambo yalivyo badilika ndani ya hii myaka 2.

Hali iko hivi:

Wabunge na madiwani wa upinzani wamejawa na hofu kali. Matumbo yao ni ya moto mabaya na joto kali. Wakipiga mahesabu ya ushindi wanaona ni bila bila. Wakiwa ndani ya Chadema au Cuf ushindi kwao ni ndoto.

Swali la kila mtu kujiuliza:
"Mtu anapoona plan A inagoma si lazima afikilie au abuni plan B?

My take:

CCM ni chama kikongwe na chenye wenyewe. Chaguzi zake ziko tyte tena tyte mno pale tunapoona wanaogombea kura za maoni kuwa ni watu wazito kiuchumi wenye mabillions of money. Kwenye chaguzi za CCM utajiri ni kila kitu: Pesa ni kila kitu!Tumeyaona kwenye uchaguzi wa hii wiki Dodoma jinsi mambo yalivokuwa balaa na changanyikeni!

Ushauli wangu kwa wewe mbunge wa upinzani unaehamia CCM pima na Kuchanganya karata zako uone kuwa utatoboa nafasi ya ubunge kupitia CCM? Je hata kama uchaguzi wa marudio ukifanyika hapo jimboni kwako jeutatoboa kura za maoni ndani ya CCM?

VODACOM : KAZI NI KWAKI
 
Umesema:-
'Wabunge na madiwani wa upinzani wamejawa na hofu kali. Matumbo yao ni ya moto mabaya na joto kali. Wakipiga mahesabu ya ushindi wanaona ni bila bila. Wakiwa ndani ya Chadema au Cuf ushindi kwao ni ndoto.'

Huo utafiti uliufanyia wapi na ni wabunge gani wa upinzania wamekwambia kwamba kwenye uchaguzi ujao wanadhani kushinda ni ndoto? Kwani huo ubunge walio nao si waliupata baada ya kupambana na ccm? Iweje leo waone kwamba kupambana na ccm ni jambo gumu sana? Hata kama ni kushabikia ccm weka basi maelezo yanayoweza kueleweka sio uandike vitu vinavyokudhalilisha. Ungesema hata kwamba waliohama wanatarajia wakishinda kupitia ccm wanaweza kupata uwaziri tungekuelewa.

Unaposema wanaohama si kwa sababu ya rushwa una uhakika upi? Kama mgombea wa jimbo moja yuko ndani kwa sababu ya rushwa, na mwenyekiti wa vijana naye alihusishwa na rushwa (kwenye ccm hiyo hiyo), na Nassari alituonyesha video inayothibitisha rushwa ilitolewa na mtu (wa ccm hiyo hiyo), kwa nini sasa sisi tusiamini kwamba wanaohama UKAWA wamepewa rushwa?
 
Back
Top Bottom