Imechukua Miaka mitatu Kuredesign Hii logo ya Xiaomi na Imegharimu $305,000

Wabongo bado hatujajua thamani ya vitu kama hivi, na graphic designer wanazaliwa kila siku na hawajui ethics za hii kazi.
Kutengeneza identity ya firm ama company siyo mchezo.
Try to imagine 15,000 ni pesa ndogo sana, hata jeans moja hainunui.
Ndy maana nimeachana na kazi za graphics designing..Kwa bongo hailipi..mtu anataka umfanyie poster design anakwambia ana elfu 5,na wewe Kwa kuwa Una njaa unaamua kukubali tu

Sasa hivi Nimenunua kamera nimeamua kuwa photographer..angalau kuna unafuu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo wabongo tuna tabia za kuchukulia poa profession za watu.
Yani mtu anatoa kazi kwa dharau, anakupangia malipo, anakupa deadline, anataka 10% na bado siku ya malipo anataka akulipie bar na anataka ofa ya vinywaji na chakula.

Hiyo logo mnaichukulia poa ila utakuta mhusika alichora michoro zaidi hata ya 1000, jaribu kumtafuta aliyeshinda hiyo logo na kama atakuwa kafanya interview ndio utaelewa alifanya kazi nzito.

Kama unataka kuona kituko zaidi tafuta redesign ya bendera ya japan, linganisha bei yake na kilichofanyika ndio utaona maajabu
Mkuu kibongobongo kuwa graphics designer ni ngumu sn kutoboa

Mtu anakuletea kazi bei anayokutajia Hadi unacheka,anakuambia hapo si unachora chora Tu na kupaka rangi dakika tano

Nimeachana Nayo sasa hivi naprint t shirts na kupiga picha Tu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kutengeneza logo mpaka uchemshe akili na wakati mwingine jina la kampuni lisomeke kwa kuiangalia hiyo logo, yaani ili ulione hilo jina mpaka wewe naye ujitume kuichanganua hiyo logo.

Sent from my cupboard using mug
Tena hiyo kazi ya logo kuna muda unaimaliza kuifanya alafu unajipa break km siku moja ,ukirudi kuiangalia tena unakutana na makosa kibao
Unaanza kuifumua upya au unakuja na idea nyingine kisha unamwonyesha mteja but anakataa kazi zote mbili

Pesa aliyokulipa sasa ndy utachoka

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Sio rahisi kama unavyoona!

Kuna Psychology na Marketing strategies nyuma take
Unashangaa hio,Pepsi walitumia 1M dollars Ku rebrand logo yao tu,na final product ikawa haina tofauti na former logo zaidi ya kubinuliwa kidogo tu

We unaona kazi rahisi,ila kuna akili nyingi imetumika

Angalia logo ya Amazon ujue Nina maana gani
Unaweza kuamini imebeba msingi wa amazon wa "customer's happiness"?

IMG_0259.jpg

leo ndio nimejua kuwa hii logo inatabasamu
 
Hapana hiyo ndio itakuwa lifetime logo..logo za biashara kubwa huchukua muda sana kukubaliana ndani ya kampuni
So idadi kubwa ya watu kwenye kampuni iliunga mkono hiyo logo?

Napata picha kama kulikua na logo zingine ambazo zilipata kura ndogo ni jinsi gani zilikuwa mbaya zaidi
 
Nahisi walikuwa wanatafuta attention ya watu kwa ajili ya kuuza bidhaa waliyoizindua
Ndio ukweli Huo ata hawatafuti attention, unajua thamani ya design ya logo ya BBC? Japokuwa ilikuwa ni miaka mingi imepita Ila ilikuwa $1,800,000. Shangaa mtu kapewa Huo Mpunga kudizaini Tu BBC inafurahisha Sana, au logo ya Pepsi ukiona simpo Tu ila expensive

Wenzetu wanachukulia serious sana na wanaheshimu Sana kazi ya mtu, huku kwetu mtu akikwambia umtengenezee logo ukisema laki 5 Tu unaskia poa nitakuchek, ndo harudi huyo na ajabu atapata atakaetengeneza ata Kwa elf 90,

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Pesa ile kwa ajili ya Logo kwa Company kama Xiaomi ni ya kawaida
Natambua ni ndogo kwani company revenue ni USD 37billion hivyo unaposema usd 300,000 ni ndogo ina make sense.

Sasa mimi siongelei kwamba hiyo pesa ni kubwa au ndogo bali naongelea gharama za kutengeneza hiyo logo haiwezi fika kiasi hicho cha pesa.
 
Logo inabeba kampuni watu wanatoa mpunga kwa ajili yake.
Kuna makampuni yamewahi kubadili logo zake mauzo yakashuka watu wakaikataa ikabdi warudie logo za awali. Saikolojia ya mwanadamu haieleweki unaweza jikuta unapendaa bidhaa flani kisa logo yake tu na wewe hujui kama ndiyo sababu
 
Ndio ukweli Huo ata hawatafuti attention, unajua thamani ya design ya logo ya BBC? Japokuwa ilikuwa ni miaka mingi imepita Ila ilikuwa $1,800,000. Shangaa mtu kapewa Huo Mpunga kudizaini Tu BBC inafurahisha Sana, au logo ya Pepsi ukiona simpo Tu ila expensive

Wenzetu wanachukulia serious sana na wanaheshimu Sana kazi ya mtu, huku kwetu mtu akikwambia umtengenezee logo ukisema laki 5 Tu unaskia poa nitakuchek, ndo harudi huyo na ajabu atapata atakaetengeneza ata Kwa elf 90,

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Ulaya pia kuna Logo za dola 1 kibao,

Na pia huku bongo kuna watu wanataka hela nyingi na huo uwezo hawana.

Ndio maana Taasisi nyingi wanatangaza mpunga, milioni kadhaa zinawekwa mezani, mna peleka logo zenu na maaana zake, kunakuwa na panel ina chagua.
 
Hata Tanzania zipo logo zenye cost angalau, I think TPB Bank logo.

Personally bila TZS 2M kwa small scale, 8+M kwa medium scale na 20+M kwa large scale kwa Tanzania sifanyi logo.

Nimecharge TZS 2M+ kwa logos tofauti kimataifa na zimeonesha kuwa chachu kwa ukuaji wa kampuni/shirika na brand zake kiujumla.

Tanzania tasnia ya creativity, design na illustration (Sanaa kwa ujumla) inadharaulika maana watu wao wamezoea kutumia maguvu kuliko akili.
 
Kutengeneza logo sio kitu chepesi aisee. Nilikua najaribu kutengeneza yani inachukua mda na akili nyingi kutumika,
 
Back
Top Bottom