Imebaki miaka 6 Tanzania kufikia uchumi wa kati. Tuko wapi na tunafikaje kwa haraka zaidi?

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
991
1,000
Najaribu kuwaza tu baada ya kusoma vitabu na machapisho mbalimbali ili kijitathmini kama taifa la Tanzania.

Tuko wapi ili kufikia uchumi wa kipato cha kati na uchumi wenye ushindani ambao ni jumuishi kwa Watanzania wengi.

Kumbukumbu mbalimbali zaonesha baada ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin mwaka 1989 kulitokea imbalance of world powers.

USSR ya Mikhail Goberchev ilianguka na Rais Bush Sr akama mfalme wa dunia. Mpaka hivi juzi China ime-gain power na sasa wanamtunishia Marekani misuli hasa kwenye vita ya kiuchumi.

Nguvu ya China imekuwa kwenye exports ya machineries za aina zote. Kubwa, size ya kati na size ya chini. China anauza Technology, China anauza nguo, China anauza finished product ya vitu mbalimbali.

Nilikuwa nikisoma chapisho mmoja ambapo mkakati wa baadhi ya mataifa ni kuweka himizo kwenye usalama wa taifa kwa ku-connect na uimara au uthabity wa kiuchumi.

Mkakati wa mataifa mengi na China ikiwemo suala la nguvu za kijeshi linaendana sambamba na nguvu za kuichumi kwa kufanya biashara za kila aina. Biashata safi na chafu kwa lengo kuvuna fedha za kigeni.

Unaweza kupitia ukurasa huu hapa chini kuona global trend ya China katokea wapi miaka ya 70 na sasa yuko wapiKwa upande wa pili nampongeza JPM kwa kuona state of urgency kutangaza Tanzania ku-adopt viwanda kama tool ya kutufanya kukuza uchumi wetu.

Rai yangu, tuna haja ya kubadili mkakati wa kukuza uchumi wetu na namna ya kufanya biashara.

Umasikini ni adui anaetumiwa na mabeberu kwa kushirikiana na few nationals walio kwenye sekta ya umma kutuchelewesha. Esau ali-negotiate at point of weakness. Hatuna budi kuu-combat umasikini kwa kujenga mifumo jumuishi ya kukuza uchumi.

Ujinga nao ni doinda ndugu. Nadhani Wizara ya elimu ina wajibu wa kufanya. Haiwezekani tunakuwa na output ya vijana kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo ambao hawawezi kuwa na mchango unaopimika kutufanya kuufikia uchumi wa kati.


Magonjwa mengine yanadhibitiwa watu wanapokuwa na ufahamu na fedha. Sidhani kama unaweza kupata wagonjwa wa kipindupindu masaki, Mbezi au Capri point. Ila mabatini, manzese, tmk na jangwani ambako msimu huu wa mvua watu hawana tumaini kesho itakuwaje.

Tanzania ya viwanda ndio mpango mzima, tunaomba mkakati wa kuifikia uwe jumuishi. Kuna watu wako public sekta wanaona as if private sekta ya Watanzania wakiwa-facilitated watafaidi sana. Kufuatia ujinga huo, ndipo tuna import mpaka toothpick.

Tanzania ya neema inawezekana kama tutakuwa team players (public + private partnership) na kujenga organized systems ambazo zitaongeza fursa za ajira kwa vijana wetu kuzalsisha.

Siku chache zilizopita, BOT "wemeboa" tena. Wanashangaza pale ambapo kila mwaka wanatoa riport za kwanini exports zinashuka badala ya kuja na mkakati wa muda mfupi na muda mrefu namna ya kupunguza imports na namna gani ya kuongeza exports. Na hapa sio exports ya mazao ghafi but rather finished products zenye viwango vya kuuzika duniani made in Tanzania.

Mawaziri na makatibu wakuu, tunajua mna pressure ya uchaguzi mwakani na deliverables ili kutekeleza ilani. Ila sasa, muwe mnapatikana. Kuna wengine hampokei simu, huenda mko vikaoni na ziarani, basi muwe na mfumo wa ku-respond kwa sms kwa mauala ambayo yatajenga Tanzania yetu.

Uchumi ukikiua ni neema kwa wengi.

Chonde chonde, tushirikiane. Hatuna utaifa na nchi nyingine ya kujivunia mbali na Tanzania.

Ifike wakati ikiwa ni aina flani ya final product, ulimwengu u-rely kwa made in Tanzania; tukianza ku-export shilingi yetu itaimarika.

SGR itakuwa na maana sana baada ya kukamilika ikipitisha mizigo mingi inayokuwa exported kwenda nje ya nchi kuliko inayoingia.

Geo-economically, basi hao Rwanda, Uganda, Congo vitu kama nguo wanavyo-agiza, kwanini visitokee hapa, maana tuna pamba.

Kama ni toothpick, kwanini zisitokee hapa, na kuna mianzi mingi tu Iringa. Sitaki kuamini JKN tulie-adhamisha miaka yake 20 ya kuondoka alijenga inclusive economy kama alivyotuambia Mzee Mzindakaya, halafu leo hii player mkubwa ni watu wa rangi toka asia ambao wakichuma wanahamia Uingereza.

Wakati mmoja JPM alijinasibisha yuko tayari kuzalisha mabilionea 100, BOT, Hazina, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara, Kilimo, Elimu wana mkakati gani wa kulifanya hilo litokee.

Mabilionea 100 hao ni waajiri, hao ni walipa kodi, hao wanachangia mifuko ya pensheni kupitia wafanyakazi wao. It high time to join forces to make even that mission of 100 billionaires wa Kitanzania itokee kama indicator ya 2015.

Kenya wana billionaires wengi kuliko sisi licha ya size ndogo ya Ardhi na idadi ya watu. Tunajipangaje japo kuwa sawia na wao bila kufisadi. Maana jirani +254 nae kwa ufisadi hawajambo

Mungu Ibariki Tanzania na weekend njema wazalendo
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,695
2,000
Tutamuongezea muda ili akamilishe ndoto zake
Magufuli si wa kumruhusu astaafu baada ya miaka kumi

Watu kama hawa ni mara chache kuwapata tumpe muda zaidi
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
991
1,000
Tutamuongezea muda ili akamilishe ndoto zake
Magufuli si wa kumruhusu astaafu baada ya miaka kumi

Watu kama hawa ni mara chache kuwapata tumpe muda zaidi
Ingekuwa hoja ni kuongeza muda, Rais Mkapa muasisi wa dira ya Taifa angeomba kuongezewa muda ili atimize objectives zote za Ilani.

2005, Rais Mkapa alimpisha JK.

2025 tunatumai hata JPM anampisha mti ambae Watanzania watamuamini kwa kumpigia kura.
JPM aliahidi hataingeza hata dakika moja.

So tujikite kwenye hoja wakubwa
 

Wood Stone

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
652
1,000
Tutamuongezea muda ili akamilishe ndoto zake
Magufuli si wa kumruhusu astaafu baada ya miaka kumi

Watu kama hawa ni mara chache kuwapata tumpe muda zaidi
Umuongezee muda, wewe kama nani? Msitake kutuharibia nchi. Mkitaka kumuongezea muda, aendelee kuwa mwenyekiti wa ccm ila kwenye uraisi hapana. Ukomo wa uraisi ni miaka 10. Ikifika, wewe ondoka zako uwachie wengine.
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
991
1,000
Hoja ya nyongeza. Kupitia AGOA (Africa Growth Opportunity Act.) Tanzania tuna fursa ya kuingiza products za maziwa ikiwemo cheese.

Bahati mbaya hatujawa na mkakati mahsusi walau ku-export cheese US.

Tungekuwa tushapiga japo hatua, hii habari ya beberu namba moja kuongeza kodi kwa cheese toka Ulaya, ingeweza kuwa neema kwa viwanda vya cheese Tz kama tungekuwa navyo.

Waziri Luhaga Mpina, Waziri Mpango, Waziri Bashungwa natamani walau mngekuwa mnapatikana kwa urahisi ili deals kama hizi ziwe fursa ya kutengeneza ajira ndani na kuingiza forex

 

z12f

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
550
500
Dira ya taifa ya 2025, inalenga Tanzania iwe na GDP per capita ya 3,000 USD.

In 2018, GDP per capita ya TZ ilikuwa 1,134 USD. Hii ina maana GDP per capita iongezeke zaidi ya mara 1.6 in around 7 years.

The growth rate of GDP per capita iwe more than 20% per annum. Since population growth ni at least 2% per annum, then uchumi ukue kwa at least 22% per annum.

Haya ni mahesabu very rough, atakae weza kufanya more accurate calculations ana weza akaziweka hapa.

Hii nadhani haiwezekani. Hatutaweza kufikia lengo hilo la GDP per capita ya 3,000 USD.


Mfano mwingine, in 2012, the population of Kilimanjaro region was 1.64 million.

Since the regional GDP per capita of Kilimanjaro region is above the national average, this means that by 2025, the GDP of Kilimanjaro region should be at least 1.64*3,000 = 4.92 billion USD.


For Dar es Salaam region (2012 population was 4.365 million), the figure should be at least 4.365*3,000 = 13.095 billion USD (by 2025).

Hilo lengo la 3,000 USD, sidhani kama linawezekana.

Vision 2025 pia inaongelea mambo ya Peace, Unity and Stability. Good governance, Pluralistic politics na private sector.

Ili tufikie hiyo 3,000 USD huko mbeleni baada ya 2025, itabidi cylinder zote za uchumi zifanye kazi vizuri. Tusitenge makabila na mikoa fulani ambayo tuna tofautiana nayo kisiasa.

Especially wakati makabila hayo yana high levels of human capital na good entrepreneurship skills (by Tanzanian standards). Na mikoa hiyo ina sekta kama utalii ambayo ni a very big forex earner and government revenue earner.

Una weza uka practice egalitarianism (usawa) bila ku create economic distortions, na economic disincentives. Na bila ya kujenga utengano.

Una weza uka ipiga jeki mikoa ilioko nyuma bila kuifungia spidi governor mikoa ilioko mbele.

Una weza ukawapunguza kwenye civil service ya serikali kuu, kwa sababu hawa kukupa kura. Lakini ukawabakisha kidogo kwasababu serikali kuu inatoa huduma nyingi na hawa watu ni raia na pia ni walipa kodi ambao wanatumia huduma za serikali kuu. Ukiwatoa wote, wanaweza kubaguliwa kwenye kupata huduma za serikali. Kwa hiyo wanahitaji uwakilishi kwa kiasi fulani ndani ya civil service.

Na vile vile usiwapunguze kwenye serikali za mikoa yao, na mitaa yao, na halmashauri zao, kwa sababu hizo ni ‘nchi ndogo’ zao (maeneo yao ya uzawa).

Vile vile wapewe uhuru waku perform vizuri kwenye private sector. Otherwise wataishije, wata kidhi vipi mahitaji yao na hii ni nchi yao, na wana haki nayo kama wengine.

Halafu wasukuma ni wengi, kama wangekuwa wamesoma, wangeweza kujaza nafasi zote za civil service, na majeshi yote na bado wakabaki. Hapo bado hujaweka wengine wa kanda ya ziwa.

So mkakati wa kuwainua wasukuma ulenge pia kuwafanya wawe wafanyabiashara wazuri, na pia waweze kujiajiri vizuri.

Hii si rahisi kwa sababu itabidi watumie hela nyingi sana na bidii nyingi sana, na maarifa mengi sana na muda mwingi sana, ili waweze kuwa na average level za human capital kama za wachagga. Na sehemu kubwa ya hela watakazo zitumia inabidi ziwe zao, na sio za serikali.

Haya yanawezekana ila yafanyike kwa upendo, unyenyekevu na kwa subira na maarifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom