Imebainika: Kuliko kuchangia CHADEMA Shilingi milioni 1 kila mwezi ni heri uhamie CCM na ubunge wako!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,901
141,837
Imegundulika kuwa wale wabunge wa CHADEMA waliomwandikia barua za maombi ya kujiunga na CCM, Mwenezi wa chama hicho ndugu Polepole wanakimbia makato ya kila mwezi.

Imeelezwa kuwa CHADEMA wana utaratibu wa kuwakata Wabunge wa viti maalumu Shilingi laki 5 na wale wa kuchaguliwa Shilingi milioni 1 kila mwezi.

Endapo CCM itakubali maombi ya wabunge na madiwani hao kuhamia kwao, CHADEMA itabakia na Wabunge wasiozidi 20 Bungeni.
 
...wabunge na madiwani hao...
Hao madiwani wanakatwa tsh ngapi na hulipwa tsh ngapi?
 
...wabunge na madiwani hao...
Hao madiwani wanakatwa tsh ngapi na hulipwa tsh ngapi?
Halmashauri mirija ya unyonyaji imezibwa madiwani hawapigi dili so hawana cha kuchangia ndio maana kila iitwapo leo wanakimbilia CCM!
 
Hii Serikali Imegubikwa na Ufisadi Mwingi Kuliko Serikali Zote Zilizotangulia, Na Hii Inatokana na Wao Wenyewe Kuamua Kujitoa Kwenye Mpango wa Uwazi Serikalini na Pia Kupitisha Sheria Isiyompa Mamlaka CAG Kukagua Madini. (Sasa Sijui Kazi ya CAG Itakuwa Nini?)
 
kuna dalili za wabunge kuachishwa ubunge km yule alie hamia ACT. CDM ukiongea ukweli adhabu yako ni kukatwa uanachama.
 
Tatizo ni kuihalalisha haramu kuwa safi mchana peupe. Kama wanataka kuhama wahame tu kwa mikataba kuwa tunahamia na ubunge wetu kuliko kuangamiza pato letu kwa uchaguzi mwingine. huku wanetu hawali chakula cha mchana mashuleni. Tuangalie vipaumbele ni nini kwetu.
 
..ipo mantiki ya wabunge wa cdm kuchangia chama chao.

..wanashindana na ccm ambayo ina access na resources mbalimbali za serekali, inapokea mabilioni ya fedha kama ruzuku, na inachangiwa na wafanyabiashara karibu wote wakubwa.

..katika mazingira hayo cdm inatakiwa ifanye nini ili kuweza kushindana na ccm?

NB.

..tatizo ni kama michango ya wabunge inatumiwa vibaya na viongozi wa chama.
 
Wenzao cuf wanakatwa mil3 na hawana hata choo kule Zanzibar
Unadhani mbowe company and sons hiyo
tapatalk_1522571646647.jpeg
 
Hata wale wabwatukaji wanaojifanya wanauchungu na kodi za wananchi kwenye scandal ya chama chake huwaoni!!
Akina Malissa huwasikii!!!
 
Hata wale wabwatukaji wanaojifanya wanauchungu na kodi za wananchi kwenye scandal ya chama chake huwaoni!!
Akina Malissa huwasikii!!!
huwa wanapata mgao hao ukiona wanapinga ufisadi chadema humu ni wanaofaidi mgao wa huo ufisadi
 
Back
Top Bottom