Imbori, binti mrembo wa Kimbulu aliebeba historia iliyokinzana kati ya laana na mapinduzi dhidi ya mtoto wa kike!!

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Mwaka 2006 nilibahatika kwenda mkoa wa Manyara na sehemu ya mkoa wa Arusha nikiwa na kazi moja ya kufanya tafiti za vinasaba miongoni mwa makabila ya wafugaji, nilifika mji wa Mbulu sehemu ya Mama Isara (Kainamu) na Haidom. kwa mkoa wa Arusha nilifika wilaya ya Ngororngoro kata za Endulen Esere na Kakesio.

wakati wa matekelezo yangu nilikutana na hadithi ya binti Imbori, jina lake hili ndio limetohoa jina MBULU, wao hulitamka IMBORU, ambapo ndio yalikuwa makazi ya kwanza ya binti huyu wa KIIRAQ (hakuna tofauti kati ya mmbulu na mwiraq, japo wao hudai kuwa mmbulu ni yule akaae mbulu ila yule wa nje ya mbulu ni mwiraq,ila kilugha wapo sawa)

katika mazungumzo ya hapa na pale kwenye baadhi ya kaya ndipo nikapata hadithi ya binti huyo imbori! ambao wao hudai laana za mabinti wao kuzalia nyumbani sana na kutoroka nyumbani bila ya ndoa ikiwa ni sehemu ya laana kutoka kwa binti huyu!



miaka mingi iliyopita kulikuwa na binti mmoja aitwae Imbori alikulia na kuzaliwa sehemu za mamaisara nje kidogo ya mji wa mbulu ambapo kihistoria ndipo chimbuko la wambulu. kutokana na tamaduni za pale mida ya jioni baada ya mavuno huwa wana ngoma za kucheza ambapo vijana wa kike na wakiume hukutana kucheza ngoma. kikabila huiita (nima fighito).

kwenye ngoma hizo alikwepo kijana mmoja aitwae Imbori na kijana mmoja wa kiume aitwae boayi! boayi alikuwa akimpenda imbori kwa muda mrefu, ila kutokana na tamaduni za watu wa pale ilikuwa yapaswa kwenda nyumbani kujitambulisha na kuhalalishwa kindoa.

ilikuwa ni mwiko kwa mtoto wa kike kuzalia nyumbani hivyo kama si kuacha mapenzi nje ya ndoa basi ilikuwa lazima wapate somo la kutazama siku zao kwa kutumia mbalamwezi. vinginevyo mtoto wa kike akithubutu kupata ujauzito alikuwa akibebwa na kaka zake pamoja na kiasi kidogo cha chakula na kwenda kutupwa na kutelekezwa kwenye mlima fulani upo nje kidogo ya mama isara!

kwenye mlima huo binti huyo huenda kuishi peke yake huku akila chakula kile kidogo mpka kitakapoisha, Basi haya yote ndiyo yaliyomkumba imbori baada ya kukosea siku zake boayi akampa ujauzito, ilikuwa ni kesi kubwa kwani kwa uzuri wa binti yule pengine mahari yake ingekua kubwa.

alibebwa na kaka zake huku mama yake akisulubishwa ipasavyo kwa kiboko kuwa ameshindwa kumwelimisha vyema binti yake. akaenda kutupwa kwenye mlima ule ambao ulikuwa na fisi wengi, kikawaida mtu anapoenda kutupwa huko moja kwa moja alikuwa akiacha maombolezo kuwa anaenda kufia kule.

hii ilikuwa tofuti kidogo kwa imbori kwani kijana yule aliempa mimba alikuwa akimpenda kweli, hivyo alihakikisha anafnya kila mbinu kujua anaenda kutupwa wapi. kijana siku ilipowadia alijiandaa mapema na kuufuata msafara ambao ulikuwa ukitoka asubuhi sana. na kupaona alipoachiwa akiwa kwa mbali sana!

baada ya kupaona na kuhakikisha msafara unarudi nyumbani ndipo boayi akaenda kumchukua binti yule na kumpeleka sehemu iliyo nje kidogo ya makazi yao, lile eneo likawa likijulikana kwa IMBORI kwani alikuwa mjuzi wa kupika pombe na watu walikuwa wakitoka mbali kuja kupata pombe kwake. kabla ya imbori mabinti wengi walikuwa wakifia kwenye mlima ule!

hivyo baada ya mafanikio ya binti imbori na kwenda kujenga kijiji chake baadae utamaduni ule wa kwenda kumtupa mtoto wa kike ukaanza kufifia na hatimae kupotea. chanzo kikiwa matokeo ya Imbori kwani ILIPASWA AFIE KWENYE MLIMA ULE ILI KUSAFISHA LAANA YA BINTI KUZALIA NYUMBANI!

(Historia hii niliipata kama hadithi tu kwa kijana Sikai, hivyo pengine kuna mambo yameongezeka au yamepungua, lakini bado funzo litakuwa lile lile)
 
Umefuatilia vyema huko kwa wakoloni ukakuta hakuna historia kama hizi?
Hajakaa akashirikisha ubongo na kufanya tafiti. Hizo story za akina Hercules, Archiles na zinginezo kama akina Robin Hood zinatofauti gani na hii story? Wenzetu wanazitukuza, mdau hapo anazibeza. Afanye utafiti kidooogo atakuta katika kila jamii kuna story kama hizo

Sent from my SM-J700F using Tapatalk
 
kwa simulizi nilizozisikia kijana aliitwa mayo, na walitupwa pembezoni mwa mlima Guwang', Mayo alimuhamisha na kumpeleka sehemu inayoitwa sanu barray(leo hii) jirani na hospital ya wilaya ya Mbulu.
 
Nlikua na dem mbulu delphina baada ya kumaliza form six tukifungiana geto saa 5 asubuh kutoka saa 11 jioni hadi washkaji walikua wanamuita vampire..maana alinikondesha kale kalikizo...ila alikua mtamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom