Ibambangulu, nabii mtenda miujiza aliyetabiri kuzaliwa kwa Mwl Nyerere

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,791
8,739
Heshima kwenu Mabibi na Mabwana, Poleni na heka heka za maisha

Km kichwa cha habari kinavyosomeka, Imbangulu ni Nabii mtenda miujiza km ilivyokuwa kwa manabii wengine enzi hizo, inasemekana katk karine ya 19, Nabii huyu aitwaye Imbangulu alipata kutabiri kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpigania uhuru mashuhuri wa Afrika aliyeleta changamoto kubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Kama ilivyokuwa kwa manabii wengine ambao dini hudai habari za kuzaliwa kwao zilitabiriwa na manabii au nabii, basi hata kuzaliwa kwa Mwokozi wa Afrika na Tanganyika yaani Mwalimu kulitabiriwa na nabii wa Mungu aitwaye Ibambangulu, Nabii Ibambangulu inasemekana alikuwa Nabii mtenda miujiza, miujiza mingine aliyoitenda Ibambangulu inasemekana hata Yesu hakuwahi kuitenda, Ibambangulu alikuwa msukuma, alikuwa anaishi Magu ktk mkoa wa Mwanza.

Inasemekana Nabii huyu alikuwa na desturi ya kupanda mlimani na kutazama mashariki wakati anapotabiri kama alivyokuwa akifanya Yesu na manabii wengine wa kidini, hatimaye ilipofika mwaka 1922, Butiama, Mkoani Mara, Mwalimu alipata kuzaliwa.

Km una lolote kuhusu nabii huyu Imbangulu Msukuma wa Magu mkoani Mwanza Karibu
 
Rekebisha title mkuu. Jina limekosa silabi mojawapo. Unazo pia habari za Ng'wanamalundi? Hatukuwa na maandishi na historia za mashujaa na manabii wetu zimepotea. Matokeo yake tunaonekana kama vile hatukuwa na cho chote. Asante sana !
 
Mambo mazito haya, ulikuwapo wakati hayo yanafanyika? Kuna ushahidi gani dhahiri wa kuthibitisha hayo uyasemayo? Umesema alikua anapanda milimani, milima ipi? Anatofauti gani na Mwana malundi? Kwanini hakuwahi kupata unaarufu? Maswali ni mengi..

hivi wewe unapowasoma Mohamed na Yesu ulikuwapo wakati wao?

ushahidi upo nitakuletea

kwanini useme anatofauti gani na mwanamalundi? acha utumwa wa kufikiri

umekaririshwa kuwa manabii wote na mitume wana ngozi nyeupe, huo ni upuuzi

huyu Imbangulu alikuwa ni nabii mkubwa sana sema habari zake hazikupata kuandikwa,
 
Rekebisha title mkuu. Jina limekosa silabi mojawapo. Unazo pia habari za Ng'wanamalundi? Hatukuwa na maandishi na historia za mashujaa na manabii wetu zimepotea. Matokeo yake tunaonekana kama vile hatukuwa na cho chote. Asante sana !
asante mkuu kwa kumjua huyu nabii wetu, utanisaidia maana kuna watu hapo juu washaanza, wakimaanisha haiwezekani nabii kuwa mswahili

ni IBAMBANGULU mods watanisaidia kurekebisha

mkuu sina hakika km hatukuwa na waandishi ila ninachojua ni kwamba, wahuni hawa wa kiarabu na kizungu walipokuja Afrika kuleta dini zao walichoma moto nyaraka za historia ya waafrika kwa madai kuwa zilikuwa nyaraka za mashetani
 
Heshima kwenu Mabibi na Mabwana, Poleni na heka heka za maisha

Km kichwa cha habari kinavyosomeka, Imbangulu ni Nabii mtenda miujiza km ilivyokuwa kwa manabii wengine enzi hizo, inasemekana katk karine ya 19, Nabii huyu aitwaye Imbangulu alipata kutabiri kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpigania uhuru mashuhuri wa Afrika aliyeleta changamoto kubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Kama ilivyokuwa kwa manabii wengine ambao dini hudai habari za kuzaliwa kwao zilitabiriwa na manabii au nabii, basi hata kuzaliwa kwa Mwokozi wa Afrika na Tanganyika yaani Mwalimu kulitabiriwa na nabii wa Mungu aitwaye Ibambangulu, Nabii Ibambangulu inasemekana alikuwa Nabii mtenda miujiza, miujiza mingine aliyoitenda Ibambangulu inasemekana hata Yesu hakuwahi kuitenda, Ibambangulu alikuwa msukuma, alikuwa anaishi Magu ktk mkoa wa Mwanza.

Inasemekana Nabii huyu alikuwa na desturi ya kupanda mlimani na kutazama mashariki wakati anapotabiri kama alivyokuwa akifanya Yesu na manabii wengine wa kidini, hatimaye ilipofika mwaka 1922, Butiama, Mkoani Mara, Mwalimu alipata kuzaliwa.

Km una lolote kuhusu nabii huyu Imbangulu Msukuma wa Magu mkoani Mwanza Karibu
Ushahidi pls
 
nabii huyu wa kiafrika alikuwa na maajabu mengi sana likiwa pamoja na hili
alikuwa akiingia kwenye chumba alikuwa na uwezo wa kujaa chumba kizima na hii ilipelekea mauti yake ambapo siku moja alijaa kwenye chumba na nje kulikuwa na kuku mmoja aliyekuwa anatembea kutafuta chakula aliona kitu kama nyama na akadonoa kumbe ulikuwa mwili wa nabii huyu na hapo hapo mauti yalimfika nabiii wa kiafrika akafa akiwa ameacha maajabu mengi
 
Rekebisha title mkuu. Jina limekosa silabi mojawapo. Unazo pia habari za Ng'wanamalundi? Hatukuwa na maandishi na historia za mashujaa na manabii wetu zimepotea. Matokeo yake tunaonekana kama vile hatukuwa na cho chote. Asante sana !
mkuu nilibahatika kupata pia habari za Ng'wanamalundi,

Nabii huyu alikuja baada ya Ibambangulu,

Ng'wanamalundi alikuwa akitembea juu ya maji km Yesu, hadi wakoloni walikoma, alikuwa na uwezo wa kunyoosha kidole na mti unakauka papo hapo,
 
Back
Top Bottom