Imani za watu wa muambao wa pwani DSM,TANGA,ZANZIBAR,MOMBASA NA MTWARA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani za watu wa muambao wa pwani DSM,TANGA,ZANZIBAR,MOMBASA NA MTWARA

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by MziziMkavu, Nov 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD][​IMG]


  Kula gizani ni kula na shetani.
  To eat in the dark is to eat with the devil.
  This belief discourages eating In the dark, for
  obvious reasons.

  Kushona nguo mwilini kunaleta ufukara; tabia
  hii aidha inajongeza kifo, maana inakuwa kama
  mtu anajishonea sanda yake mwenyewe.
  To mend a garment which is on one’s body
  brings poverty: it also suggests preparing
  one’s own shroud, which betokens death.

  Kufagia usiku kunakimbiza baraka
  .
  To sweep at night is to chase away blessings.
  (This belief contains some truth, in that one
  may sweep up and throw away something of
  value unwittingly.)

  Kutembea hali ya kuwa mtu amevaa kiatu
  kimoja tu kunavimbisha ziwa la mama yake
  mtu.

  Walking about with only one shoe on causes
  one’s mother’s breast to swell. (I suppose this
  is simply to discourage the stupidity of going
  about with only one shoe on.)

  Mtu akinywa maji usiku pasi na kuufumka mtu-
  ngi, usiku roho yake itaingia ndani ya mtungi na
  akitokea mtu akaufunika huo mtungi wakati
  huo huo, basi atakufa papo hapo.

  If a man drinks water at night and leaves the
  vessel uncovered, his soul will plunge into it

  during the night, and if someone accidentally
  puts the lid on, he will die at once.

  Mtu akiona. chungu ya wadudu sisimizi ukutani
  basi atafikiwa na wageni wa ghafla.

  If a man sees a swarm of ants on the wall it
  means that unexpected guests will arrive.

  Kwenda kulala pasi na kuosha miguu, basi hiyo
  miguu italazwa katika moto wa Jahannam.

  If one goes to bed without washing one’s feet,
  they will lie In the fires of Hell.

  Mtu akilala pasipo kuosha miguu, nyayo zake
  zitarambwa na shetani.

  If a man goes to bed without washing his feet,
  the soles of his feet will be licked by the devil.

  Mtu akila bila ya kupiga Bismillahi . . basi
  baraka itaondoka na mtu hataweza kushiba.

  If a man eats without saying grace, there will
  be no blessing, so the food will not suffice.
  (This belief has a religious background. Islam
  teaches its followers to allow religion to per-
  meate all their daily acts: and the great
  majority of the population of Zanzibar and
  Pemba are Muslims.)

  Mtoto mchanga akiachwa peke yake, atageuzwa
  na shetani.

  If a baby is left alone in a room it will be
  changed by the devil for his own. at is firmly
  believed that Albinos are ‘changelings’.)

  Mwenye kufanya mazowea ya kukaa kizingitini
  atakawia kuoa.


  He who develops a habit of sitting on a door-
  step will be late in getting married.

  Kula wima kizingitini, mtu atapigwa dafrau na
  shetani.

  He who eats while standing on the door-step
  will be knocked down by a devil. in tended to
  discourage the habit of eating in such abnormal places.)

  Kula kitu kitamu kinjianjia mtu atasibiwa na shetani.
  He who eats sweet food while walking will be
  possessed of a devil. (It is regarded as bad
  manners to eat while walking.)

  Mwenye kumcheka mkwewe hupata maradhi
  ya chokea.

  He who laughs at his father or mother-in-law
  will develop a stye.

  Kumchungulia mtu mzima aliyekaa uchi kunaleta upofu.

  Looking at a grown-up person naked will
  bring blindness.

  Kuzaliwa na vidole sita ni mabruki.
  To be born with six fingers Is to have good
  fortune.

  Ukiuonyesha mwezi mchanga kidole. basi utakatika kidole.
  If you point at the new moon with a finger It

  will get cut.
  Mwenye kula miguu ya kuku atakuwa daima
  katika mwendo tu

  He who eats a fowl’s legs will become a wan-
  derer.

  Inakatazwa kunywa maji ndani ya kata pasi na
  kuikung’uta.

  It Is forbidden to drink water from a ladle
  without vigorously shaking It first. (To ensure
  that it is clean and free from Insects.)

  Kupeana mkasi mikono kwa mkono kunasabibisha kuchukiana bure.
  Handing over a pair of scissors to someone
  directly causes hatred.

  Kukaa juu ya mto kunaleta majipu matakoni.
  Sitting on cushions causes boils on the but-
  tocks.

  Kukutana na paka mweusi usiku ni nuksi.
  Meeting a black cat at night means bad luck.

  Kunywa maji ya chooni kunapeleka mtu kuwa
  mwongo.

  Drinking water from the lavatory makes a
  man a liar. (Intended to discourage so unwholesome a habit.)

  Kutema mate ndani ya lindi kunaleta kuumwa
  na koo.

  Spitting into the cess-pit causes sore throat.

  Kumbusu mtoto usingizini kunasabibisha mtoto
  huyo kuwa na majivuno ukubwani mwake

  Kissing a sleeping child will make It grow up
  conceited.

  Mwenye kuchukua Quran kichwani ataingiliwa
  na wazimu

  Carrying the Holy Quran on the head will
  cause madness.

  Kukaa kitini na kupunga miguu mbele na nyuma m kufukuza riziki.
  To sit on a chair swinging one’s legs backwards and forwards will drive away one’s
  daily bread.
  (This is regarded as bad manners by Arabs as
  it is a sign of contempt.)

  Kupiga uluzi ni kuita shetani.
  To whistle is to call the devil.

  Ukikanyaga chakula makusudi utasibika na
  maradhi ya matende.

  if you tread on food deliberately you will get
  elephantiasis. (This belief has a religious
  background, and is based on an abhorrence
  of waste.)

  Mwenye kuzowea kula ndani ya chungu atapata
  mvua kubwa siku ya harusi yake.

  One who eats straight from a cooking-pot will
  have heavy rain on his wedding day.


  Mtoto mwenye kuchezea kivuli chake cha taa
  atakojoa kitandani.

  A child who plays with his shadow cast by a
  lamp will wet his bed.

  Kuuza chumvi usiku ni nuksi kwa mwenye duka.
  Selling salt at night brings ill luck to the
  shopkeeper. (This belief is so deep-rooted)
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  kukaa kizingitini utapigwa kikumbo na shetani. Kupiga mluzi usiku ni kumwita nyoka/mchawi,usipotemea mate mahala ulipokojolea basi litakatika ziwa la mama yako. Nalog off
   
 3. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hiyo ya kufagia usiku, nakumbuka tulikuwa tukikatazwa wakati tunakua huko unguja! kumbe ni mila zao
   
Loading...