Imani za kishirikina: Prof. Maghembe aunda kikosi cha waganga wa kienyeji ili kuwafukuza Tembo waliovamia makazi ya watu Wilayani Mwanga

Hijja Madava

JF-Expert Member
May 14, 2014
3,250
2,000
Tembo wamevamia makazi ya watu wilayani Mwanga. Wakati sisi wataalam wa wanyamapori tukishirikiana na askari wa wanyamapori kuwaondosha kitaalamu, Mbunge Maghembe ameunda kikosi cha waganga wa kienyeji ili kuwafukuza Tembo hao kwa njia ya kitamaduni.

My Take:
Kama hao ndio wasomi wetu tuna kazi kubwa!
 
riro23

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
731
1,000
Kwahiyo wewe unalalamika nini? unashirikiana na askar wa wanyama pori tangu lini wakati tembo wameshaharibu mazao maeneo yote ya eneo la tambarare(nyika) mpaka wakulima wamekimbia maeneo yao na tangu wiki iliypopta tembo wapo maeneo ya usangi

Ukweli askar wamezembea hii kitu Kama hao waganga wataweza kuwaondoa wawaondoe tu
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,474
2,000
Hii habari sitaiamini mpaka pale tu itakapowekwa picha kama ile ya Mbeya!
Ni mapema mno kutokeka tukio la 'mazishi' nchini mwa Sugu lililohushisha PhD iliyotukuka na sasa mnaleta habari za profesa. Ndio maana innovators na wajasiriamali waliofanikiwa wengi hawajapitia hii formal education yetu hivyo kukwepa hili janga la 'kuchafuliwa' bongo zao kwa kulishwa matango pori!
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,881
2,000
Kuna rafiki yangu mmoja Mpare kutoka Usangi aliniambia Prof Magembe yupo vizuri sana kwenye utamaduni wa mtu mweusi, na bi Mkubwa wake ndio Mistress of The Game.Hata hivyo likua ni katika porojo tu za baraza za kahawa.

Lakini mkuu wote mwajenga nyumba moja mbona kama mnagombea cement? Nyie mkitumia mabunduki na yeye akitumia "utamaduni" nini mbaya? Lengo si tembo waache kuharibu mashamba au kuna lililojificha?
 
Scoundrel

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
532
500
Tembo wamevamia makazi ya watu wilayani Mwanga. Wakati sisi wataalam wa wanyamapori tukishirikiana na askari wa wanyamapori kuwaondosha kitaalamu, Mbunge Maghembe ameunda kikosi cha waganga wa kienyeji ili kuwafukuza Tembo hao kwa njia ya kitamaduni.

My Take:
Kama hao ndio wasomi wetu tuna kazi kubwa!
nakumbuka nilielezwa ya kwamba huyu mheshimiwa amesomea masuala ya wanyama pori kama sikosei!
 
Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,252
2,000
Kule CHATO alipoonekana CHATU mkubwa alipelekewa zawadi za mbuzi , unga etc kama ishara ya kumuabudu kwa kuwaletea neema!!! Usishangae hayo ya prof. Maghembe; kwani mmesahau jinsi cabinet yetu ilivyoongozana kwenda Loliondo kunywa kikombe cha babu?
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,699
2,000
Kwanini waganga wa kiafrika tunawadharau sana kwahiyo sisi afrika hatuna sayansi , yaani hata kidogo.

Mtoa uzi tuombe msamaha

Kibaya ni uchawi na ushirikina lkn uganga una shida gani?
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,900
2,000
Umenikumbusha mkuu, Wagweno ni Wapare halisi? Maana wanamajina yanayoingiliana sana na makabila mengine mfano Minja, Muhando nk na hata lugha yao inatofautiana na kipare cha kawaida
Hao ni kama wachaga hivi. Hata kipare chao ni tofauti na cha kwetu. Wapare halisi huwa"wanawadharau" sana wagweno sijui ni kwanini maana hiyo ni tangia mababu na mababu
 
Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,664
2,000
Tembo wamevamia makazi ya watu wilayani Mwanga. Wakati sisi wataalam wa wanyamapori tukishirikiana na askari wa wanyamapori kuwaondosha kitaalamu, Mbunge Maghembe ameunda kikosi cha waganga wa kienyeji ili kuwafukuza Tembo hao kwa njia ya kitamaduni.

My Take:
Kama hao ndio wasomi wetu tuna kazi kubwa!
Source ya hii habari tafadhali?

Ahsante
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom