Imani za Kishirikina Katika Mapenzi Sababu ya Mtoto Kuzamishwa Sindano 42 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani za Kishirikina Katika Mapenzi Sababu ya Mtoto Kuzamishwa Sindano 42

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">Imani za Kishirikina Katika Mapenzi Sababu ya Mtoto Kuzamishwa Sindano 42</td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Mtoto mwenye umri wa miaka miwili ambaye mwili wake ulikutwa ukiwa na sindano za kushonea nguo zipatazo 42. </td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Sunday, December 20, 2009 11:48 AM
  Imani za kishirikina ndizo zilizopelekea, baba wa kambo azizamishe sindano 42 za kushonea nguo kwenye mwili wa mtoto wa miaka miwili wa nchini Brazili ili aweze kurudiana na mke wa zamani.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Baba huyo wa kambo alitiwa mbaroni baada ya mtoto wa miaka miwili kuwahishwa hospitali hali yake ikiwa mbaya kufuatia sindano 42 za kushonea nguo zilizozamishwa ndani ya mwili wake.

  Sindano hizo zenye urefu wa sentimeta tano zilizama kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wake.Sindano mbili zilipasua mapafu yake na kumfanya akohoe muda wote huku sindano moja ikiujeruhi moyo wake.

  Akijitetea mbele ya polisi, baba huyo wa kambo aliyetajwa kwa jina la Roberto Carlos Magalhaes mwenye umri wa miaka 30 alisema kuwa mke wake wa zamani ndiye aliyemuamrisha azizamishe sindano za kushonea nguo walizozifanyia mambo ya uchawi na kuziita "Sindano zenye baraka" kwenye mwili wa mtoto huyo.

  Roberto ambaye anajishughulisha na kazi ya kutengeneza matofali, alisema kuwa mke wake huyo wa zamani alimlazimisha azizamishe sindano hizo kwenye mwili wa mwanae wa kambo ili kuurudisha uhusiano wao wa zamani.

  Mke wa zamani wa Roberto, bi Angelina Ribeiro dos Santos, alimlipa mganga mwanamke wa mji wa Candomble, Santana azibariki sindano hizo ili kuyarudisha mapenzi yao.

  Polisi wanaamini kuwa Angelina alifanya kitendo hicho kulipa kisasi kwa mama wa mtoto huyo ingawa hakuelezea sababu ya kufanya hivyo.

  Kwa mujibu wa maelezo yake, Roberto alifanya kitendo hicho kutokana na vishawishi vya mke wake huyo wa zamani ingawa alikiri kuwa yeye ndiye aliyezizamisha sindano hizo kwenye mwili wa mtoto huyo.

  Mojawapo ya sindano hizo ilizama kwenye moyo wa mtoto huyo, ikimaanisha kuwa mtoto huyo atahitaji operesheni ya dharura iwapo damu zitaanza kuvuja kwenye moyo wake.

  Sindano moja ilizama ndani ya mapafu yake wakati sindano zingine zilipita pembeni kidogo ya ogani zake muhimu.

  Roberto na Angelica walikamatwa na kuhifadhiwa kwenye sehemu za siri kufuatia hatua ya watu wenye hasira kulipiga mawe gari la polisi lililokuwa limewabeba.

  Mganga mwanamke aliyezibariki sindano hizo naye alikamatwa lakini huenda akaachiwa huru kwakuwa alikuwa hajui sindano hizo zingetumika kwa kitendo hicho.

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3774062&&Cat=2

  </td></tr></tbody></table>
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  hata... hata... hatari..................
  jamani tuwe tunajiuliza japo mara mbili ndipo tuamue nini cha kufanya.
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,657
  Likes Received: 8,208
  Trophy Points: 280
  kama kawaida...Majuu hamnazo!
   
 4. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kumbe ushirikina sio Africa tu, inasikitisha lakini...
   
Loading...