Imani yetu kwa serikali ya Kikwete

Bado una imani na serikali ya Kikwete?

  • NDIYO (YES)

    Votes: 215 19.4%
  • HAPANA (NO)

    Votes: 834 75.1%
  • Sijui (Undecided!)

    Votes: 64 5.8%

  • Total voters
    1,111

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete, rais uliyetokea kupendwa na Watanzania wengi hadi ukaweza kupata kura nyingi kukupa ushindi wa kishindo, sisi Watanzania tunakuomba ukirudi kutoka Marekani usafishe hali hii. Mkoloni mweusi kaingia nchini. Anatutukana sisi Watanzania. Anakejeli hali yetu ya Umasikini.

Kwa kawaida sisi wananchi wako tunaishi maisha magumu sana kwa siku tunatumia chini ya dola moja. Hali hii si kwamba bei ya bidhaa ipo chini la hasha bali ni hali ngumu ya maisha. Tunajitahidi kuwa watulivu wakati wewe mwenzetu unasafiri huku na huko kutafuta uwezekano wa kujikwamua na maisha haya tuliyo nayo, hilo tunakusifu kwa juhudi hizo.

Wakati unaingia madarakani ulituahidi mengi sana hata hatuwezi kuyakumbuka yote sidhani kama hata wewe unakumbuka labda hadi upekue makabrasha yako ukaweza kukumbuka ulichotuahidi.

Katika hali isiyo ya kawaida juzi juzi ulisafiri kwenda China wewe na ujumbe wako akiwemo Andrew John Chenge, ambaye aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali katika awamu ya tatu. Kipindi hicho ndicho tulichoshuhudia usaliti wa serikali dhidi ya wananchi wake kwa mambo mengi mathalani ubinafsishaji wa mashirika ya umma na kuwapa wawekezaji au niwaite wapangaji wa uchumi wetu. Inaelekea kwamba wote waliofanikisha ubinafsishaji huu walikuwa na maslahi binafsi kwani ndicho kipindi tulichoanza kushuhudia mgawanyiko wa matabaka katika jamii. Hii ilitokana na viongozi kuanza kujilimbikizia mali za umma. Zoezi hili limevuka mpaka ambapo sasa tunashuhudia mtu kama waziri anakuwa jasiri wa kukejeli wananchi.

Hali hii ni picha dhahiri kwamba ndani ya suti yako kuna chawa, sisi wananchi tunakupigia kelele kwamba katika kola za koti lako kuna chawa mkubwa sana anajaribu kutoboa ili akunyonye shingoni. Kelele hizi sijui kama hujasikia kwani hata watoto unaowapenda na kuwasikiliza wameshakwambia usizibe masikio vua hilo koti chawa aondolewe atakunyonya.

Ni aibu sana kwako kusafiri pamoja na mtu mwenye kejeli kiasi hicho kwa wapiga kura wako. Sisi wananchi wako TUMEKATA TAMAA hatuna imani na baadhi ya mawaziri wako. Tunajua kwamba huwezi kuwa na mawaziri wazuri kwa asilimia mia moja lakini inapojitokeza waziri wako akaonyesha tabia mbaya kiasi hicho macho yetu tunakuelekezea wewe kuangalia UNASEMAJE.

Kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi, tukadanganywa kwamba uchumi utajirekebisha wenyewe, tukakaa kimya. Kumekuwa na mfumuko wa bei ya bidhaa mbali mbali tena muhimu ikiongozwa na bei ya mafuta ya kuendesha mitambo n.k. nalo pia tukakaa kimya. Bila shaka ingekuwa nchi kama Zambia jirani zetu kuhusu hilo wangeandamana.

KWA HILI

1zphbew.jpg

PAMOJA NA MENGINE YANAYOFANANA NA HAYO, SISI WANANCHI HATUTAKUELEWA KAMA HUTAYASHUGHULIKIA IPASAVYO.

Mwisho tunakupongeza kwa juhudi zako za kutafuta wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA

NOTE: Ukimaliza kusoma hii, pitia na hizi ili upige kura bila upendeleo:

Nimekuwa najiuliza kuhusu kura ya kutokuwa na imani (a vote of no confidence) Hii kura iko applicable kwenye sheria zetu za Tanzania au haipo. Lini bunge au baraza la mawaziri laweza kuitumia against waziri mwenzao au bunge juu ya waziri mkuu au raisi wa nchi.

Katika matukio mbali mbali kama vile Israel waliishawahi kumpigia waziri mkuu Nentenyahu kura ya kutokuwa na imani http://findarticles.com/p/articles/mi_qn4158/is_19970625/ai_n14101252. Kenya leo wabunge wamempigia waziri wa fedha Amos Kimunya kura ya kutokuwa na imani baada ya kuuza hoteli ya kitalii kwa siri http://africa.reuters.com/country/KE/news/usnL02638600.html.

Katika nchi yetu hasa wabunge wetu je inawezekana kwa wao kupiga kura ya kutokuwa na imani bungeni kwa Rais, Waziri Mkuu au Waziri yeyote kama wanafikiria hawako –effective kutekeleza majukumu yao?

JF kama kuna mtu anaweza kutupa sheria na mazingira ya kura ya kutokuwa na imani rusha msaada basi!
 
Ipo kwenye Katiba ya nchi na pia Bunge linaweza kumwondoa rais na waziri mkuu ila kuna utaratibu maalum umewekwa.
 
Mpaka Kieleweke,

Shukrani mkuu ngoja niitafute hiyo katiba nafikiri niliisha iona hapa sikufulani!
 
Kwa wabunge wetu hawa huwezi kufanya chochote cha maana.CCM wana viti vingi zaidi na rais ana nguvu sana.
 
Nafikiri bado tuna njia ndefu hadi kufikia kura ya kutokuwa na imani, nafikiri tukiwa na balance ya wabunge wa CCM na Upinzani then tunaweza. Raila kama Waziri Mkuu ndiye kawasukuma wabunge na mawaziri wengine kumpigia waziri wa fedha kura ya kutokuwa na imani naye leo hii Kenya.
 
Uwezekano wa hili kufanyika Tanzania ni mdogo sana kwa sababu ya ubinafsi na ufisadi wa wabunge wa ccm ambao wanajali vyama kuliko taifa lao
 
Mgaya,

Mbali na ubinafsi wa wabunge wa CCM hata wa upinzani wanakuwa na maslahi yao mbele mara nyingi ndio maana migogoro na kuhama vyama ni kila siku. Mfano wa waziri mkuu wa kenya kuongoza baraza la mawaziri kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri wa fedha ni wa kuigwa. Kwetu sasa hivi ilitakiwa Waziri wa fedha, Waziri mkuu na hata JK wapigiwe kura hiyo.

Pamoja na kuwa Kenya wana mapungufu mengi kama vile ukabila, kisiasa wanaonekana kuiva vaidi ya sisi tunaojivunia kuwa tu ndugu moja kwa sababu ya chembe chembe ndogo ya ukabila
 
Kenya na Tanzania, two countries so close and yet too different in political views and perspective. Waziri Mkuu mmoja anajiuzuru kwa ishu ya ufisadi na Mwingine anasimama kidete kupinga ufisadi. The contrast is indispensable. Naamini kabisa tuna wabunge na mawaziri safi wanaoweza kusimama kidete na ku-initiate a vote of no confidence ila tatizo linaweza kuwa support ya kutosha kuipitisha inaweza kuwa ngumu kidogo.
 
Hapa tulipofikia sasa ni pabaya na panaashiria mparaganyiko katika taifa letu. Kwamba wakristo wametoa tamko zito dhidi ya serikali kuhusu OIC na kwamba waislamu nao wanajiandaa ijumaa ijayo kutoa tamko zito kukabili lile la wakristo,na hapo hakuna kiongozi wa nchi aliyeshtuka, ni hitimisho la nchi yetu kukosa uongozi.

Ni muhimu basi vyombo makini kama bunge vichukue hatua. Nami natoa wito kwa wabunge wetu wanapoanza bunge mwezi ujao waandae hoja na kisha wampigie kura Rais Kikwete ya kutokuwa na imani naye, ili tuanza moja. Kumuacha huyu ndugu hadi 2010 ifike ni kukaribisha matatizo makubwa mno kwa nchi yetu huko mbele. Kwa uchungu kabisa, nawasilisha.
 
Samahani hakuna kitu kama kutokuwa na imani na Rais... only kwa Waziri Mkuu. Kwa upande wa Rais ni kumshtaki kibunge (impeachment) tu inawezekana na mchakato wake ni mgumu kuliko kwenda jehanamu
 
Muungwana kalala siku atakayoamka ndege ya rafiki wake EL imeshapaa na kumuacha hoi. Kila kitu kinakwenda hovyo ndani ya nchi hivi yeye anaona? Kama anaona anachukua hatua gani? kukaa kimya na yenyewe ni part ya solution perhaps ndio ameamua kuchukua we never know.
 
Hiyohiyo mheshimiwa Mwanakijiji, issue ni kumuondoa-hiyo lugha sahihi mimi sielewi sana. Naongelea hicho kitu ambacho wabunge wana uwezo nacho. Inawezekana mchakato ni mgumu, lakini utasaidia kumuamsha huyu tembo anayeonekana kulala fofofo!
 
Binti Maria, kama watu wako tayari kwa nini kuhangaika na huo mchakato mrefu na mgumu zaidi???

Suluhu mbona ni rahisi sana? Unahitaji watu kuamua kuchukua nchi yao na kumpa mtu mwingine awaongeze. Hilo tu, wala hakuna haja ya kupitia bungeni au mahakamni. Nchi ni ya wananchi kwa hiyo wanaamua asubuhi tu na inakuwa hivyo. Mifano iko mingi tu duniani. Tatizo letu tunangoja watu wengine waje kutusaidia!
 
Binti Maria mawazo haya tulishawahi kuyaibuwa wakati ule wa mjadala mkali wa bajeti ya mafisadi...Na nikawashauri wabunge waigomee bajeti ili srikali ivunjike...Wakagoma...Sasa sijui kama watafanya sasa hivi...Labda kama wakiona kuna hatari ya kupoteza ubunge wao .
Na kama ni kweli tunataka ku rely on the voters..Basi still kuna kazi ya kufanya kwani rushwa na takrimas huwa zinafanya kazi sehemu mbali mbali na kabla ya uchaguzi wa 2010 tutaona mengi sana tu.
Mshtuko wameupata ccm esp kutokana na mweleka wa huko Tarime...Lakini Mh Rais hatuna uhakika kama yuko intouch na wananchi wake...No wonder naenda kulala mapema.
 
Binti Maria mawazo haya tulishawahi kuyaibuwa wakati ule wa mjadala mkali wa bajeti ya mafisadi...Na nikawashauri wabunge waigomee bajeti ili srikali ivunjike...Wakagoma...Sasa sijui kama watafanya sasa hivi...Labda kama wakiona kuna hatari ya kupoteza ubunge wao .
Na kama ni kweli tunataka ku rely on the voters..Basi still kuna kazi ya kufanya kwani rushwa na takrimas huwa zinafanya kazi sehemu mbali mbali na kabla ya uchaguzi wa 2010 tutaona mengi sana tu.
Mshtuko wameupata ccm...Lakini Mh Rais hatuna uhakika kama yuko intouch na wananchi wake...No wonder naenda kulala mapema.

Ndio maana siku zote nasema bila kuwa na bunge lenye mlingayo wa wabunge hatutapata mabadiliko kutokea bungeni hata siku moja.

wale wachache akina Anna Kilango walipopiga kelele makamba akapendekeza wawajibishwe, unafikiri wanaweza kutokea wabunge wengine wakapiga kelele wakati wanajua kuwa 2010 inakaribia na hawatapitishwa na CCM.

Mabadiliko ya kweli kutokea bungeni yatakuja tukiwa na wapinzani wengi zaidi, bila hivyo CCM watendelea kuiba na njia pekee iliyobaki ni kuwaelimisha wananchi wawe kama tarime.
 
Ni muhimu basi vyombo makini kama bunge vichukue hatua. Nami natoa wito kwa wabunge wetu wanapoanza bunge mwezi ujao waandae hoja na kisha wampigie kura Rais Kikwete ya kutokuwa na imani naye, ili tuanza moja. Kumuacha huyu ndugu hadi 2010 ifike ni kukaribisha matatizo makubwa mno kwa nchi yetu huko mbele. Kwa uchungu kabisa, nawasilisha.

Naunga mkono hoja hiyo kama njia mbadala ya kuiepusha nchi katika vita.
Raisi kashindwa kwa baadhi ya mambo yafuatayo yanayomfanya apoteze sifa za kuwa Raisi mwenye hadhi.

1.Ameshindwa kulinda umoja wa watanzania kwa kupitia hoja ya kadhi na OIC na kuwagawa watanzania kwenye makundi makubwa mno yenye mkinzano mkali wa ugomvi na hivyo kuvunja ahadi yake aliyoapa ya kulinda umoja wa watanzania.Kwa sababu ameshindwa hilo hastahili kabisa kuendelea kuongoza.Hata kama amefanya mazuri yepi kuvuja umoja ni kosa lisilosameheka inabidi afunge virago.

2.Ameshindwa kulinda katiba aliyoapa kuilinda kwa kugeuza ofisi za serikali zitumike kuendesha mihadhara ya kidini kwa kuteua maofisa wa serikali wazunguke nchi nzima kuendesha mihadhara ya kidini ya kuuliza kama watu wanataka kadhi wa kiislamu au hawataki.Kazi ya Raisi si kusimamia mihadhara ya kidini kwa gharama za walipa kodi.

Raisi amekuwa mtumiaji mbaya wa pesa na mali za serikalikama pesa za serikali,magari ya serikali na ofisi za serikali na za walipa kodi kwa kuzitumia kulipia ya mambo yanayohusu hoja ya kadhi wa kiislamu wakati wakizunguka kushughulikia mihadhara ya kuhusu kadhi wa kiislamu.

3.Raisi amekuwa mtumiaji mbaya wa madaraka kwa kutokemea wizara ya sheria na katiba isijihusishe na mambo ya kidini yanayohusu kadhi bali amekuwa akitumia ubabe wa kijinga kuburuza na kushinikiza maafisa wa serikali waendelee na hoja ya kadhi kinyume na matakwa ya taaluma yao ya katiba kwa maagizo mbalimbali mara kwa mara.

4.Raisi kama mhimili muhimu wa utawala katika nchi na mlinzi wa katiba ilibidi azuie hoja ya kadhi isiende bungeni kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa katiba.Lakini bila aibu wala haya aliachia iende bungeni na kuligeuza bunge liwe mahali pa mhadhara wa kiislamu wa kujadili kuwepo au kutokuwepo kwa kadhi wa dini ya kiislamu.Tunaamini Raisi ndiye kaligeuza bunge kiwe kijiwe cha wahuni wa mihadhara ya kiislamu ambao wanafanya bunge ni kijiwe cha mhadhara wa kujadili mambo ya kadhi wa kiislamu jambo ambalo ni la kidini kabisa.Raisi kaligeuza bunge kuwa eneo la mihadhara ya kidini ya mambo ya kadhi wa kiislamu kwa kulipelekea hoja ya kidini.

Bunge letu kwa kuwa nalo limejaa mabwege likaanza mhadhara wa kidini wa kadhi bungeni badala ya kupiga marufuku mhadhara huo usikanyage bungeni.Bunge letu limejaa watu mabwege wasiojali katiba bali posho tu ndio maana wao hawajali kuangalia katiba inasemaje kabla ya kuijadili ndiyo maana hoja ya kadhi ilipenya sababu serikali inajua bunge limejaa mabwege wasiojua katiba au hawaitilii maanani.

Ufumbuzi wa kwanza wa kuepusha vita ni kuwa bunge lipige kura ya kutokuwa na imani ili kuepusha hasira ya wananchi wasizushe vita. Wamwite Raisi bungeni wamwambie aondoe hoja zote za kidini na wampe karipio na onyo kali yeye na serikali yake asirudie tena na wamwandikie barua kuwa hawaridhishwi na utendaji wake kama wawakilishi wa wananchi na wampe karipio kali la kimaandishi kuwa arekebishe utendaji wake kama Raisi kama atakubaliana nao.

Kama Raisi atakataa kutii maagizo ya bunge kwa jeuri basi mahakama ambaye ni muhimili wa tatu itoe amri ya kumtaka Raisi aondoke madarakani kwa sababu ya kuvunja katiba kwa kuingiza hoja za kidini katika serikali na bunge hivyo ni mhalifu mkuu wa kikatiba asiyetakakiwa kuendelea kuongoza nchi.
Kama akikataa kutii hata amri ya mahakama basi Jeshi itabidi liingilie kati kumtimua kwa kuwa bunge na mahakama havina imani na utendaji wake.Endapo Jeshi litashindwa kufanya wajibu wake huo hapo sasa wananchi ruksa kuingia mitaani kufanya chochote wanachoona kinafaa wakifanye.

Kama wabunge watakataa kumchukulia hatua Raisi wakajifanya vichwa ngumu wakakataa kuondoa hoja za kadhi na OIC bungeni na kuendelea kuzijadili hivyo kuendeleza ujeuri wao wa kuivunja katiba iliyopo basi wananchi itabidi waingie hatua ya kulizingira jengo la bunge kwa siku kadhaa wabunge wakiwemo ndani kwenye kikao na kuwashinikiza wabunge wote waliomo ndani ya jingo la bunge wajiuzulu na watangazie taifa hivyo wao wenyewe kutoka humo ndani kujiuzulu kwao na kutamka kuwa uchaguzi mpya uitishwe. Kuzingira mabunge mapumbavu ni njia mbadala kuliko kuanzisha vita inayoweza maliza raia wasio na hatia.

Bunge likishindwa kulinda katiba ambayo lenyewe limeitunga halina budi nalo litimuliwe. Na kama halitaki kuondoka wananchi wana haki ya kuwashinikiza wajiuzulu kwa kulizingira jengo la bunge.Wakiendelea kugoma hata baada ya kuzingirwa basi kinachofuata hapo mimi sitakuwepo nitakuwa nawahi Moscow kwenye mtaa wa machinga wa silaha kuuliza kama bunduki za AK 47 za mitumba wanazo na zinauzwa bei gani na zaweza wasili kwenye jengo la bunge lini na kwa usafiri upi wa haraka.

Yatakayofuata sijui naachia walenga shabaha walenge chochote wanachoweza kulenga kile ambacho roho zao zinapenda kulenga.Shenzi type.
 
Wale wabunge wote wanaotaka kuchaguliwa tena ni lazima wasikilize vilio vya wananchi...Na kama wananchi wakiwatuma wafanye hivyo na wao wakakataa...Then ni wazi wanaweza kuambiwa wakalale mapema la sivyo wanaweza kupigwa mawe na wao pia.

Mambo si mazuri kabisa na kama waheshimiwa wabunge(minus wale mafisadi) Wakilifumbia tatizo hilo macho basi na wao watakwenda na maji ifikapo 2010.

Uchaguzi ujao kweli utakuwa mshike mshike.
 
Nentanyahu hapa nilipo sina mbavu...Lakini ni serious na inawezekana wewe uko bongo...Unajuwa wana forums ambao mko bongo mnaona hali halisi na kweli maneno yako hapo juu yanaonyesha kukasirishwa na kuchoshwa kwa walio wengi hapo bongo...Kwa mfano nilikuwa siju kama Rais ameteuwa watu wa kueneza propaganda za mahakama ya kadhi kwa kutumia pesa ya walipa kodi.

Kweli wabongo lazima watakuwa wamebadilika sana.
Kazi kwa mafisadi sasa.
 
Back
Top Bottom