Imani ya wananchi kati ya rais JK na mawaziri ni % ngapi?

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF,

Napenda kuleta hoja yangu hapa, Mara baada ya Rais JK kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania 2005 na ukapita mwaka mmoja ywa uongozi wake JK aliibuka kidedea kuwa ana asilimia kubwa ya wananchi kuwa na imani nae kuliko Baraza lake la mawaziri ambalo lilionekaka fika kuwa hali wajibiki kabisa kwa wananchi,

Ila mara baada ya uchaguzi wa 2010 Rais Jk alipo ingia madarakani uaminifu wa wananchi kwa Rais JK umeporomoka kwa asilimia kubwa sana kuliko ubande wa Baraza lake la mawaziri.

Kwanini nasema hili maana kipindi cha kwanza aliwika sana JK na sasa hawiki kabisa ni waziri wake wachache ndio wanao wika eg John Pombe Maghufuli, Anna Tibaijuka,Pinda Mizengo ingawa nae anaanza kushuka uamini kutoka kwa wananchi toka na misimamo yake katika bunge la 10.

Vyombo vya habari na Redets na synovate vilisema sana kuwaminiwa kwa rais katka muhura wa kwanza kuliko baraza lake la mawaziri sasa imekuwa kinyume chake uamini ni zero kwa wamamnchi na hivi vyombo havija sema hilo hata kama JK ndio anamalizia ungwe yake ya mwisho still alipaswa kuwa na % kubwa ya uaminifu kutoka kwa wananchi.

Nawakirisha Hoja karibuni kuchangia kwa mawazo yenu na mtazamo wenu pia
 
Kwa kweli kwangu mimi binafsi na nafikiri na watz wenzangu sina imani na kikwete kabisa, kwanza:
1.Hashughuliki na matatizo ya wananchi ipasavyo ili kuwawezesha kimaendeleo kwa kujenga miundo mbinu imara.
2.Anakuwa kimya sana hasa linapojitokeza janga la kitaifa kama umeme,kama mkuu wa nchi anatakiwa atoe tamko siyo kuwaachia mawaziri pekee.
3.Anawakumbatia sana mafisadi badala ya kuwatimua.
4.Anajilimbikizia mali kupitia kwa mwanae Ritz.
Kwa hayo machache kwa kweli hawezi kuaminika tena, labda kwa sababu anamalizia muda wake ndo maana anaamua kukomba.
 
Kwa kweli kwangu mimi binafsi na nafikiri na watz wenzangu sina imani na kikwete kabisa, kwanza:
1.Hashughuliki na matatizo ya wananchi ipasavyo ili kuwawezesha kimaendeleo kwa kujenga miundo mbinu imara.
2.Anakuwa kimya sana hasa linapojitokeza janga la kitaifa kama umeme,kama mkuu wa nchi anatakiwa atoe tamko siyo kuwaachia mawaziri pekee.
3.Anawakumbatia sana mafisadi badala ya kuwatimua.
4.Anajilimbikizia mali kupitia kwa mwanae Ritz.
Kwa hayo machache kwa kweli hawezi kuaminika tena, labda kwa sababu anamalizia muda wake ndo maana anaamua kukomba.

Nakuunga mkono kwa hayo uliyo yasema, ila kwa hilo la mwisho sidhani kuwa ndio kigezo kwani me nadhani ilimpasa kipindi hiki ndio asimame kidete kabisa kufa au kupona akitoka madarakani awe ameweka kumbu kumbu ila mpaka sasa hajaonesha dariri zozote za kunyanyuka ni anadidimia kila kukicha na ni mwaka wa kwanza wa ungwe yake ya mwisha hata hujaisha matatizo rukuki na anapo nishangaza na serikali yake ni pale anapo sema Uchumi umekuwa sasa hapo huwa simwelewi kabisa ni uchumi umekuwa wapi kwenye makaratasi ya serikali au hazina au statistic za BOT au kwa wananchi au vipi, Me nadhani kukua kwa uchumi ni pamoja na wananchi wako kuwa na maisha yao yanekwenda vizuri bila makerere ya kusema hiki kimepanda sana na mbaya zaidi Dolla ina panda kila siku sasa hapo ndio kukua kwa uchumi jamani au wasomi watusaidi kwa hilo la kukua kwa uchumi inalenga especially nyanja zipi za kijamii kiuchumi nakadharika?

My Take:
Ni wakati sasa wa watanzania kuelezwa kweli nini maana ya kukua kwa uchumi na una reflect vipi katika maisha yao ya kila siku Kijamii,Kiuchumi,Kisiasa na wajue wana kwenda wapi na wajua ni njia zipi zaweza kusababisha kukua kwa uchumi ili wawe washiri wakuu katika kukuza uchumi wao, na tusiwe twapigiwa mboyoyo za kisiasa ati uchumi umekuwa huku uki check exchange rate Tsh ni selling 1620 na Buying 1600 against 1 $ (USD)

Katika hayo yote Imani ya wananchi kwa JK asitegemee itakuja juuu ni itazidi didimia na wengi wanahofu JK kutoboza ungwe yote hii hadi 2015 ni njozi kama wananchi walisha fika hapo basi ujuwe kuna matatizo makubwa tayari wananchi wameisha yachoka na kufikia ukingoni
 
Soma Signature yangu utalijua jibu langu, sina zaidi ya kuchangia, nikimzungumzia huyo Fisadi na genge lake ninaweza kupigwa BAN na Robot
 
Ameona muda wake umeisha,kwa hiyo ameamua kukusanya kila kitu chenye
umuhumi kwake na watu walio karibu naye pomoja na kujaza makabati ya nguo.
 
Back
Top Bottom