Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Imani na Furaha za Watanzania Zadidimia
Kila kukicha tumekuwa tukipata habari za kusikitisha jinsi wachache wanavyoihujumu nchi wakati watanzania walio wengi, hata wasomi, wakiwa hali taabani. Watanzania wanaonekana kukata tamaa kuwa serikali yao haipo kwa ajili yao na pengine labda ipo kwa ajili ya wachache, walio madarakani na wale wanaowazunguka.
Hutakiwi kwenda mbali kushuhudia haya, bali sikila maoni redioni, soma mitandao au hata habari zilizopo magazetini na utaona kuwa nyingi zinakuwa na mguso zaidi kukata tamaa na malalamiko kwa serikali yao.
Leo hii nimesoma habari za investment ya wachina na wakanada (soma link ya hapo chini) na nyingine ya uvumbuzi zaidi wa gesi kule Songo Songo, vitu ambavyo vingetakiwa viwe vichwa vya habari kila mahali, lakini hakuna anayetaka hata kushughulika navyo. Watanzania wamekata tamaa kuwa hizo mali asilia hazina tena faida tena kwao, ni za walioko madarakani.
Langu ni moja tu, hivi hii hali Mh. J. M. Kikwete anaisikia na kuielewa au hivi ni vilio vya mlango visivyomzuia mwenyenyumba kulala?? Wanandugu hebu tuambizane.
http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/Business/biz140420088.htm
http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/Business/biz140420087.htm