Imani, Miujiza na Upendo, hivi majini ya kiswahili yataelewa kiingereza?

ngongoti2000

JF-Expert Member
Nov 20, 2017
2,235
2,123
Wadau nipo najiuliza kwa sauti hili kongamano la kidini ambalo linatrend sana hivi sasa la Imani, Miujiza na Upendo (sina uhakika kama linaitwa hivyo lakini mmenielewa) limenifanya nijifikirishe kwamba mchungaji/ Mtumishi ni mzungu/wazungu.

Je, kwenye hiyo miujiza ataweza kuyakimbiza mashetani au majini ya kibongo? manake nafikiri kuna majini machahce sana yanayoelewa kimombo.

Yaani sidhani kama hayo majini/mashetani ya kibongo yanaelewa kiingereza maana hata kama kuna mkalimani wa lugha lakini kauli yenye nguvu ya kiroho inatakiwa itoke moja kwa moja toka kwenye kinywa cha nabii/mtumishi mchungaji.

Naombeni mnipe ufafanuzi kwa hilo plz kwa wanaojua
 
Nilikuwa siamini Sana kuhusu MAJINI yanayopanda vichwani....nilikuja kushangaa kwa "house girl" aliyeishia darasa la 7 ,mdogo na aliyetoka kijijini kuongea lugha ya KIFARANSA pale apandishapo majini.....duuuh dunia hii.....kweli MTU anaweza kubisha kwa ASICHOKIJUA NA KUKIONA.....

Dunia ina maajabu mengi hii.....🤣🤣
 
Ukaongea nae? Yakipanda nadhani kama yaliyopanda yana ujuzi wa kuendesha ndege mkuu unakuta unaweza kuzungusha Charter
Acha tu mkuu nilidhani ni UKICHAA NA DELUSION....

Jirani yangu ni mkongomani....nikamuita ajionee na atueleze ayasikiayo....hatari mkuu wangu....
 
Wadau nipo najiuliza kwa sauti...hili kongamano la kidini ambalo linatrend sana hivi sasa la Imani,Miujiza na Upendo (sina uhakika kama linaitwa hivyo lakini mmenielewa)...
Kutakuwa na mkalimani usiwe kilaza
 
Nilikuwa siamini Sana kuhusu MAJINI yanayopanda vichwani....nilikuja kushangaa kwa "house girl" aliyeishia darasa la 7 ,mdogo na aliyetoka kijijini kuongea lugha ya KIFARANSA pale apandishapo majini.....duuuh dunia hii.....kweli MTU anaweza kubisha kwa ASICHOKIJUA NA KUKIONA.....

Dunia ina maajabu mengi hii.....
Yako yataongea kichina
 
wanapambana na roho na roho hazina lugha rasmi inayotambulika kwao...... Kuna miujiza mingi kwao kwa wenye shida ninauhakika katika hili.....

Ninachokumbuka walipokuwa huku mkoani alisema the man said "hawajaja kuchukua (sadaka etc) wamekuja kutoa (kutoa neno la uzima na injili ya kweli)

Kulikuwa na miujiza na walifundisha sana kuhusu wokovu kuliko injili ya pesa.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom