Imani kitu kingine

twijuke

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
547
252
Wana Jf poleni na majukumu

Nipo kwenye internet, nimekaa na bwana mmjo mara naona ananyoosha mikono juu, anaongea maneno hayasikiki vizuri, natupia jicho taratibu nabaini yupo kwenye ukurasa wa facebook, lakini napata shida nahisi kama mwenzangu huenda amechanganyikiwa nimsaidie. sasa nagundua kuwa mwenzangu ni mtumishi wa Mungu, nibaada ya kusikia akisema hivi."Ushindwe katika jina la Yesu,nashusha moto kutoka juu mbinguni nakukuteketeza katika jina la Yesu,naachilia uwepo wa mwana wa Mungu,nasema Roho mtakavitu ashindwe na Roho mtakatifu ashinde".



Sasa namsalimia kwa salam ambayo hutumiwa na baadhi ya wachungaji wengi, Shalom naye ananijibu Shalom, nikamwambia mwanzo nilidhni kuna jambo linakusibu, akajbu Hooo...hapana kuna watu wana matatizo huwa wananitumia ujumbe kwenye facebook yangu niwaombee. Ebu check kwenye computer? Hapa ndo nikasema kweli Imani kitu kingine.

Mungu awabariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom