Najijua
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 1,039
- 181
Tangu jana jioni tumeanza kuhabarika kuhusu kusafishwa kwa Mh. Chenge juu ya shutuma ya radar uliyokuwa inamkabili, naamini kusafishwa huku kumekuja wakati huu bwana mkubwa ana wania ukuu wa muhimili wa pili wa dola ( Uspika).
Wakati maelezo haya yanatolewa wakati ambapo ccm inajiandaa na kikao cha kuwajadili wagombea hawa wanaweza tumia maelezo hayo kumpitisha Chenge kama mgombea wao kwa kuwa ameshasafishwa na kwa wao wanaweza tueleza hawana pingamizi dhidi yake kwa kuwa tayari ameshasafishwa.
Napenda kuitaarifu CCM kuwa imani yetu kwao ipo juu ya uteuzi wa jina la spika, hapa ndio tutafahamu dhamira yao ya kweli kabisa kwa Watanzania na nchi ambayo wanadai wanaipenda sana. Matokeo ya uchaguzi uliokwisha hivi karibuni ni ishara tosha kuwa watu wameanza kupoteza imani na CCM na uteuzi wa jina la spika linaweza rudisha matumaini na imani yetu kwao kuwa wana dhamira safi na ya kweli kabisa kwa watanzania.
CCM inahitaji kufanya uteuzi wa jina la mgombea uspika ambaye jamii haina shaka nae hata kidogo kwa kuwa haendi kuwa kiongozi wa bunge pekee bali ni kiongozi wa kitaifa pia na mgombea huyo lazima aaminike na wananchi na wabunge kwa ujumla at BEYOND REASON DOUBT,
Hakika uteuzi wa spika ni salamu tosha za mwaka 2015 na hali ya kisiasa kwao kwa miaka hii mitano ya uongozi wao,
Naomba kuwasilisha