Imamu apigwa msikitini kwa kuihama CUF

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
IMAMU wa msikiti wa Maziwa Ngo'mbe Kisiwani Pemba, Omar Hussen Said (42) amepigwa na kujeruhiwa jicho baada ya kutokea vurugu ndani ya msikiti wakati wa ibada ya Ijumaa Juni 7 mwaka, imefahamika jana.

Vurugu hizo zimesababishwa na baadhi ya waumini wa msikiti huo ambao wanapinga Imamu Said kuendelea kushika wadhifa huo kutokana na kitendo chake cha kujivua uanachama wa CUF na kujiunga na chama tawala CCM mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishina Msaidizi (ACP) Mohammed Shakani, amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na shambulio dhidi ya kiongozi wa dini Zanzibar.

Aliwataka watuhumiwa hao kuwa ni, Mfaki Ali Juma, Faki Ngome Juma na Abdallah Masoud, wote wakaazi wa Maziwa Ngo'mbe Wilaya ya Micheweni.

ACP Shakani, alisema kwamba Jeshi la Polisi linamsaka Mbwana Haji Mbwana ambaye ametoroka kwa kukimbilia kisiwani Unguja muda mfupi badaa ya tukio hilo.

"Watuhumiwa watafukishwa Mahakamani Jumatatu wakati Jeshi la Polisi tukiendelea kumsaka Mbwana Haji Mbwana ambaye ametorokea Unguja,'alisema ACP Shakani.

Aidha alisema kwamba tangu imamu Said kuamua kujivua uanachama wa chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM kumeibuka kikundi cha waumini ambao wanapiga kuendelea kuwa imamu wao kutokana kutokana na kitendo hicho.

Akifafanua kuhusu vurugu hizo, alisema kwamba wakati Imamu Said, akitoa mawadha ya Ijumaa katika membari ya msikiti alivamiwa na kuanza kupigwa na kujeruhiwa jicho la kushoto na kutibiwa katika hospitali ya Micheweni kisiwani Pemba.

Hata hivyo alisemas kwamba vurugu hizo zilithibitiwa na haraka kwa kutumia mtandao wa askari kazu waliokuwa wameimarisha ulinzi katika misikiti mbali mbali wakati wa ibada ya Ijumaa.

Alisema kwamba watu wanao tuhumiwa kuhusika na vurugu hizo wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka katika kituo cha Polisi Micheweni.

Alisema kwamba Imamu Said anaendelea vizuri baada ya kupata tiba katika hospitali ya Micheweni wakati polisi inaendelea kumsaka mtuhumiwa mmoja.

ACP Shakani amewataka wananchi Kisiwani Pemba kujiepusha na vitendo vya kuchukua sheria mkononi kwa vile vinakwenda kinyume na misingi ya utawala wa sheria.

Imamu Said ni kati ya wanachama 30 wa Chama cha wananchi CUF waliamua kukiama chama cha wananchin CUF na kujiunga na CCM na walipokelewa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM DK Ali Mohamed Shein Mey mwaka huu.

Pamoja na sheria Namba 5 ya vyama vya siasa ya Mwaka 1992 kukataza nyumba za ibada kutumika kwa shughuli za kisiasa bado tatizo hilo limendelea kujitokeza na kuathiri viongozi wa dini ikiwemo kupigwa risasi na kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi, amewataka wananchi Mkoa humo kujiepusha na vitendo vya vurugu ikiwemo kuchukua sheria mkononi.

Source: Nipashe

 
Ina maana CUF hawataki mtu mwenye dini ya kiislamu kuwa mwanachama wa CCM?

Kweli hivi vyama vyetu vya siasa vina udini ndani yake, jaji Tendwa kaa macho.
 
Ina maana CUF hawataki mtu mwenye dini ya kiislamu kuwa mwanachama wa CCM?

Kweli hivi vyama vyetu vya siasa vina udini ndani yake, jaji Tendwa kaa macho.

Pamoja na mimacho mikubwa vile bado atakuambia haoni! Labda ingekuwa CHADEMA.
 
Siasa siasa tuuu....
Hata Mungu wamemsahau kwa sababu ya siasa.!!!
 
Ubaguzi wa Wazanzibari na Udini wa CUF ndio utakaopelekea Jamhuri ya Watu wa Pemba na Jamhuri ya Watu wa Unguja mara tu baada ya Muungano wa Tanzania kufa.

Mimi maombi yangu ni huu muungano ufe, halafu tuwaache wenyewe. Na mtapoanza kuuana, marufuku kukimbilia huku
 
Ina maana CUF hawataki mtu mwenye dini ya kiislamu kuwa mwanachama wa CCM?

Kweli hivi vyama vyetu vya siasa vina udini ndani yake, jaji Tendwa kaa macho.

Wote wadini cuf & ccm
 
hizo ndizo issue za misikitini..kuongoza hivyo viunga wengine huhitaji kuwa mabingwa wa ushirikina.
 

Hivi Vyama Vya KIDINI vitamaliza Wananchi... Kwanini IMAM hana UHURU wa KUAMUA UHURU wake Mwenyewe ???
 
Duh! Tulimtukana Mahita kuwa anapiga propaganda kwa kusema CUF ni chama cha Waislam, kumbe alikuwa akisema kweli!
 
Ongeza na chadema siku watakayo simamisha mgombea wa urais wa tz muslam ndio cku ya kufa chama na wajaribu

Mkuu, unataka kusema kuna mpango ndani ya CHADEMA wa kutosimamisha mgombea wa kiislamu?
 
Ina maana CUF hawataki mtu mwenye dini ya kiislamu kuwa mwanachama wa CCM?

Kweli hivi vyama vyetu vya siasa vina udini ndani yake, jaji Tendwa kaa macho.

naona hao wake zenu hawataki mfuasi wao aje kwenu
 
Mkuu, unataka kusema kuna mpango ndani ya CHADEMA wa kutosimamisha mgombea wa kiislamu?

Chadema ndicho chama pekee kilichojipanga kitaasisi. Ni vigumu sana kwa sasa kuwaaminisha wapenzi wa Chadema kuwa chama chao kinaitikadi za udini. Waislamu walio Chadema kama mgosi Mohamedi Mtoi na wengineo wengi wako comfortable kabisa
 
Last edited by a moderator:
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom