Imagine karne ya 21 kiongozi anatumia neno Mabeberu kama silaha. Anajua kweli ubeberu upo hata kwenye biashara ya mchicha hapa nchini?

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Maana nyepesi ubeberu au beberu kama inavyotumika kwa muktadha wa siasa ni ADUI au UADUI.
Je, tujiulize hapa kwetu tz hatuna mifumo ya kibeberu makazini, kwa wakulima au kwenye biashara?

Kimsingi ukifuatilia hata kwenye biashara ya mchicha ambao huwatunawaona wakinamama wakipitisha mchicha majumbani mwetu ukifuatilia utagundua kuna ubeberu ndani yake.

Silaha kubwa ya dunia ya sasa ni mahusiano , zama hizi neno beberu halina nafasi hata kama tabia/ mfumo bado upo.
 
Bavicha kwa uongo,hata shetani anawashanga

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Ni ujinga kudhani Mabeberu yatakupenda wewe anayekupangia mipango ya kukuua kwa ukimwi na ebola

Ujinga ni mzigo kwa Chadema
 
Maana nyepesi ubeberu au beberu kama inavyotumika kwa muktadha wa siasa ni ADUI au UADUI.
Je, tujiulize hapa kwetu tz hatuna mifumo ya kibeberu makazini, kwa wakulima au kwenye biashara?

Kimsingi ukifuatilia hata kwenye biashara ya mchicha ambao huwatunawaona wakinamama wakipitisha mchicha majumbani mwetu ukifuatilia utagundua kuna ubeberu ndani yake.

Silaha kubwa ya dunia ya sasa ni mahusiano , zama hizi neno beberu halina nafasi hata kama tabia/ mfumo bado upo.
Mkuu 'lukoma' umeanzisha mada ambayo ni nzito kwa wengi wetu hapa, sijui kama hii itapata mjadala wa kutosha.

Nakupongeza kwa wazo lako hili.
 
Ni kupitwa na wakati kwa karne hii ya 21, kuamini ya kwamba umaskini na 'unyonge' wetu eti ni kwa sababu ya hayo Mabeberu! Dunia ya sasa ni ya utandawazi. Tunatakiwa tushirikiane na kila mtu/ kila Taifa duniani ambalo lina msaada kwa nchi yetu.

Tunatakiwa tudumishe uzalendo wa Taifa letu ili wale viongozi wachache wenye dhamana ya kutuwakilisha kuingia mikataba mbalimbali na hao 'Mabeberu' watangulize maslahi ya Taifa na si ya kwao binafsi kama ilivyozoeleka kwa sasa.

Kuendelea kila uchao kuwalaumu na kuwalaani hao Mabeberu, na wakati makosa ni ya sisi wenyewe, haileti mantiki kabisa.
 
Kama unafikiri beberu anakupenda sana kamuulize Lisu,!
Kajibebisha kwao weee mwisho wa siku wakamtelekeza saa hii anabaki kulike coment za kigofo kule twiter tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno beberu lina maana mbili,ya kwanza
1.mbuzi dume,
2.ni mtu mwenyewe tabia za uonevu ( maana inayotokana na kufananisha tabia za mbuzi dume)

Lilipata umaarufu kipindi Cha ukoloni na muda mfupi baada ya Uhuru hasa kutokana na siasa za ujamaa (Socialism) tulizokopi na kumodify siasa za mashariki (Russia).Lilitumiwa na wafuasi wake siasa za uchumi wa kijamaa kujenga hoja kuwa siasa/nadharia za uchumi wa kibeparu (Capitalism) ni wa unyonyaji na kionevu.

Kiukweli matumizi yake kwa Sasa yana ukakasi,kwani Dunia mzima imerithi mfumo wa kibepari ( unaohimiza umiliki mali binafsi,soko huria, ushindani wa kibiashara na kanuni/misingi yote ya demokrasia)

Dr Bashiru Mwalimu wangu wa sayansi ya siasa na utawala anafahamu fika siasa za ubepari na ujamaa. Nashangaa anavyotumia neno hilo (ingawa nae ni mfuasi wa itikadi za Nyerere) wakati Dunia ya ujamaa imeprove failure na hasa ikinathibishwa na udikteta,uonevu,uvunjaji haki za binadamu,uimla na uporomoshaji uchumi
 
Hii nchi bwana CCM itatawala milele.
Watawala mambo yakiwashinda wanasingizia kukwamishwa na Wazungu a.k.a Mabeberu, mambo yakienda vizuri ATUKUZWE M/KITI POMBE.
Wananchi na sisi adui UJINGA ndio ametushikiria hatuwezi kureason tukiambiwa beberu tu chaliiiii.

Kuna siku nimefanya analysis ya mahitaji yangu na nikagundua 80% made in Abroad(Mabeberu), nikajiuliza hivi kama Mabeberu wanataka kuidhuru Tanzania kama tunavoaminishwa na watawala mbona ni rahisi sana haya haiitaji nguvu nyingi?
Ukienda hospital Madawa mengi na chanjo ambazo tunapata kila siku na hatuhoji wala kuzihofia made from abroad.
Awamu hii inawaattack sana hawa mabeberu wakati still tunawategemea sana kwenye mambo mengi, je hatuoni kama tunajiingiza kweny risk kubwa. Kama ni kweli wana nia mbaya na Tanzania kwa nini tusiachane nao tukajitegemea ili tuwe salama zaidi?
 
Budget yetu tunajitegemea kwa asilimia ngapi saiv ... tuanzie hapo
Hata kama tunawategemea baadhi ya asilimia ila sio kuwaangukia hivyo... Halafu nadhani wanaotushika sana mkono kwenye budget huwa wa Scandinavia ambao hawana hata shida sana.
 
Ukiona kiongozi anawalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwake uleta Sana shaka.Huna kila kitu cha kuendelea Kisha unashindwa kukitumia unawatupia lawama wengine
 
Maana nyepesi ubeberu au beberu kama inavyotumika kwa muktadha wa siasa ni ADUI au UADUI.
Je, tujiulize hapa kwetu tz hatuna mifumo ya kibeberu makazini, kwa wakulima au kwenye biashara?

Kimsingi ukifuatilia hata kwenye biashara ya mchicha ambao huwatunawaona wakinamama wakipitisha mchicha majumbani mwetu ukifuatilia utagundua kuna ubeberu ndani yake.

Silaha kubwa ya dunia ya sasa ni mahusiano , zama hizi neno beberu halina nafasi hata kama tabia/ mfumo bado upo.
Ni lugha ya watu masikini kuhalalisha umasikini wao kwa kuwatupia lawama matajiri wakiaminishwa umasikini umeletwa na matajiri
 
Back
Top Bottom