Iliyokuwa foleni mataa /round abaout Ubungo kwa sasa imehamia kipande cha Rombo hadi Korogwe

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,803
8,794
Tokea kuruhusiwa kwa daraja la juu pale Ubungo kwa magari kupita juu hasa yatokayo Mwanza; Mbeya, Iringa na Bukoba na nchi za nje kulionyesha kama kutaleta unafuu kiasi fulani lakini hali sio kabisa kumekuwepo a foleni sana nyakati za jioni pindi ukimaliza daraja la juu ambalo endapo litafunguliwa napendekeza liitwe daraja la Magufuli kwenda sambamba na hostel zetu pendwa za Magufuli.

Kero hasa ipo kituo cha Korogwe hii inatokana uenda kuna uzembe wa Trafiki ama kuzidiwa na magari hasa kipindi hiki ama vyote kwa pamoja.

Ni muda sasa umefika Trafiki wetu wa Korogwe na Kimara mwisho wabadilike haiwezekani ukimaliza kimara Mwisho kuitafuta Mbezi ya kimara hakuna foleni.
 
Tatizo barabara kutoka ubungo hadi kimara ni nyembamba na haijapanuliniwa tofauti na kuanzia kimara stop over na kuendelea ambapo barabara ni pana. Pia kituo cha mwendokas kimara korogwe kinachangia pia
 
Tatizo barabara kutoka ubungo hadi kimara ni nyembamba na haijapanuliniwa tofauti na kuanzia kimara stop over na kuendelea ambapo barabara ni pana ... pia kituo cha mwendokas kimara korogwe kinachangia pia
Mkuu mbona pale bada ya daraja kumepanuliwa Sana au unaongelea kipindi Cha nyuma..shida IPO pale Korogwe na kimara mwisho sababu ya daladalala
 
Tatizo barabara kutoka ubungo hadi kimara ni nyembamba na haijapanuliniwa tofauti na kuanzia kimara stop over na kuendelea ambapo barabara ni pana ... pia kituo cha mwendokas kimara korogwe kinachangia pia
Pale korogwe tatizo sio mwendokasi(maana mwendokasi inapita njia yake) bali tatizo ni nyakati za jioni abiria wa mwendokasi wanaendelea mbezi wanashuka pale kupanda daladala na bajaj kwa kuwa kimara mwendokasi ina foleni na ili kupanda daladala au bajaj lazima upande daraja.

Ushauri wangu pale korogwe akae traffic mda wote maana daladala na bajaj zinazuia kabisa lane moja hadi nusu saa kusubiri abiria wanaoshuka kutoka kwenye mwendokasi wapite na kusababisha njia moja tu kupitika.
 
Yanayotokea morogoro road, kuelekea kimara yatatokea pia barabara ya Sam Nujoma, kuelekea mwenge! Tusubiri muda, ni mwalimu mzuri ...
 
Daah yaani nikifikiria daraja limegharibu bilioni 200 na bado nikishalivuka nakutana na foleni, nachanganyikiwa kabisa.

Kweli hakuna jambo litafanikiwa kwenye utawwala wa Magufuli
Bado sijaona sababu za kulalamika, akikaa polisi pale sheki hakuna foleni hata kidogo, leo njia ilikuwa wazi kabisa hadi manzese, magomeni trafiki alikuwepo so njia kwa kiasi kikubwa ilipitika vizuri sana.
 
Korogwe itolewe ile stand pale ndio inayoleta tafrani,

roho mbaya ifanyike pale itengenezwe stand ili barabara

kuu iachwe wazi kama ilivyo kimara mwisho pale.. .. ...
 
Nilishasema kitambo sana kwamba haya madaraja sio suluhisho la foleni, kuna mambo mengine mengi ya kufanya. Tutapoteza matrilioni mpaka tupate akili nzuri.
 
Pale korogwe tatizo sio mwendokasi(maana mwendokasi inapita njia yake) bali tatizo ni nyakati za jioni abiria wa mwendokasi wanaendelea mbezi wanashuka pale kupanda daladala na bajaj kwa kuwa kimara mwendokasi ina foleni na ili kupanda daladala au bajaj lazima upande daraja.

Ushauri wangu pale korogwe akae traffic mda wote maana daladala na bajaj zinazuia kabisa lane moja hadi nusu saa kusubiri abiria wanaoshuka kutoka kwenye mwendokasi wapite na kusababisha njia moja tu kupitika.
Kwanini hawa mwendokasi wasiwe na route ya moja kwa moja kutoka mbezi mpk Kivukoni wakaachana na kuwashusha pale korogwe huu iendeshaji wa mwendokasi unabidi ujitathimini kbs
 
Baada ya barabara ya juu Ubungo flyover kuanza kutumika na kumaliza kabisa kabisa ule usumbufu wa foleni barabara ya morogoro sasa imekuwa kero kuanzia kiande cha rombo hadi kimara korogwe

Yaani kutoka Rombo hadi ufike Korogwe tuu ni masaa zaidi 2. chanzo cha foleni hakijulikani na ma trafic wako korogwe kituoni wanavuta magari tuu lakini foleni haiishi.

Uchunguzi niliofanya kwa haraka haraka tangu barabara ya Korogwe kituoni pale kushoto (ya kuelekea maji chumvi )ikamilike kiwekw lmi na kuanza kutumika ndio inachangia maana magari ni mengi sana yanaingilia pale na kutokea

Ombi/ushauri wangu:
Kama kuna uwezekano kuanzia kituo cha mewndo kasi bucher kushoto kama inaelekea kimara kuwekwe alama ya kuongozea magari ambayo yanaingia tu maji chumvi na pale pale mwanzo wa barabara ya kuwekwe alama ya katazo la kuingia barabara kuu ila servise road ile ya zamani kushoto mwa kituo cha daladala korogwe itengenezwe magari yanayotoka majichumvi kuingia barabara kuu yaingilie hapo yakatokezee kule mbele (risot)hii inaweza saidia kupunguza foleni maana imekuwa kero sana kwa abiria wanaishi mbezi.
Karibuni kwa ushauri zaidi.
 
...Uchunguzi niliofanya kwa haraka haraka tangu barabara ya korogwe kituoni pale kushoto (ya kuelekea maji chumvi ) ikamilike kiwekwe lami na kuanza kutumika ndio inachangia maana magari ni mengi sana yanaingilia pale na kutokea
Basi kumbe kuna chanzo kingine hapa umekitaja, na sio kutokana na matumizi ya flyover pale ilipokuwa round-about
 
Tatizo nikituo cha Daladala pale Kimara Korogwe ndio sababu kubwa
Nafasi ndogo then kunanjia ile inayotoka Kule kilungure na hapohapo kunakivuko kikubwa cha waende kwa miguu na soko pembeni
 
Baada ya barabara ya juu Ubungo flyover kuanza kutumika na kumaliza kabisa kabisa ule usumbufu wa foleni barabara ya morogoro sasa imekuwa kero kuanzia kiande cha rombo hadi kimara korogwe...
kwani hamjui kuna trafiki light mbele?
 
Back
Top Bottom