Ilitakiwa Wakurugenzi wa Wilaya wawe na minimum required qualification let say Master Degree

Kiti

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
359
234
Kweli iko shughuli. Ilitakiwa wakurugenzi wa wilaya wawe na minimum required qualification let say master degree. Kisha kazi ziwe zinztangazwa na kushindaniwa kwenye usaili.

Hii biashara ya kuteuana ndio inaongeza matakwa ya katiba mpya. Nchi nyingine hata maafisa wakuu wa wilaya kama afya, kilimo, mofugo wanatuma maombi baada ya nafasi kutangazwa. Tusiende mbali hata hapo Namibia wana huu utaratibu.

Watanzania amkeni, bila katiba tumeliwa.
 
Mambo ya kuteuana haya hakuna haki unaweza pata ukiwa haupo kwenye mfumoo

Hii ilibidi iwe nafasi za kati afu inapigwa usaili wa live kama wanavyofanya Kenya kuchagua chief justice, watu tunaona hawa ma DED, RC au wakuu wa wilaya wana maono ganii?
 
Kweli iko shughuli. Ilitakiwa wakurugenzi wa wilaya wawe na minimum required qualification let say master degree. Kisha kazi ziwe zinztangazwa na kushindaniwa kwenye usaili....
Ni ujuha kudhani kuwa mtu mwenye masters ndiye anayeweza kusimamia ukusanyaji wa tozo za serikali! Ni kweli kabisa tunahitaji wasomi katika kuongoza sekta za serikali lakini siyo lazima awe na masters!
 
Formula inayotumika inatokana na falsafa i scratch your back you scratch mine yaani kada wa ccm ndio wana qualify kwenye 87% ya Teuzi na anayeteua kisheria ni mtu mmoja tuu.
 
Kweli iko shughuli. Ilitakiwa wakurugenzi wa wilaya wawe na minimum required qualification let say master degree. Kisha kazi ziwe zinztangazwa na kushindaniwa kwenye usaili...
Hapo nyuma wakurugenzi waliteuliwa miongoni mwa wakuu wa idara kama promotion. Kipaumbele walipewa Planning Officers kwa kuwa ndio walikuwa wasaidizi wa karibu zaidi wa wakurugenzi kwenye masuala ya maendeleo.
 
Ni ujuha kudhani kuwa mtu mwenye masters ndiye anayeweza kusimamia ukusanyaji wa tozo za serikali! Ni kweli kabisa tunahitaji wasomi katika kuongoza sekta za serikali lakini siyo lazima awe na masters!
Basi PHD kama hutaki masters
 
Degree ndio elimu kubwa ya kuweza kufanya kazi kubwa yeyote ya kiuongozi..

Hata rais wa nchi dunia nzima kigezo ni degree 1 tu. Hakunaga kigezo cha master ama phd. Mtu mwenye degree 1 ya halali anaweza kufanya majukumu yeyote ya kiuongozi
 
Wasomi wa Masters wanapigwa Vita sana Mkuu.

Mtu mwenye Masters anauwezo mpana wa kiuongozi .

Naunga mkono Hoja.👍👍
 
Elimu kuu kupita elimu zote nchini mwetu ni kuwa Kada. Na ndio kigezo kilichoangaliwa. Pia kuna watoto wa wakubwa na watu wazito. Watoto wa wakubwa wengi pia hawana ajira kwahiyo wazazi wao wanazo connection za kufosi watoto wao wateuliwe.
 
Ni ujuha kudhani kuwa mtu mwenye masters ndiye anayeweza kusimamia ukusanyaji wa tozo za serikali! Ni kweli kabisa tunahitaji wasomi katika kuongoza sekta za serikali lakini siyo lazima awe na masters!
Mbona ume comment kwa hasira.kasome.sema nyie wafipa hambebani.pengo,Mzindakaya,kimti wote hawa hawajawasaidia.labda msakila ndio alikua na maono.KASOME mkuu
 
Kweli iko shughuli. Ilitakiwa wakurugenzi wa wilaya wawe na minimum required qualification let say master degree. Kisha kazi ziwe zinztangazwa na kushindaniwa kwenye usaili...
Kwamba elimu ya Master ndio utendaji?
 
Mbona ume comment kwa hasira.kasome.sema nyie wafipa hambebani.pengo,Mzindakaya,kimti wote hawa hawajawasaidia.labda msakila ndio alikua na maono.KASOME mkuu
Pengo hakuwahi kuongoza jimbo huko ufipa; angesaidia vipi labda kwa wadhifa aliokuwa nao?!
 
Pengo hakuwahi kuongoza jimbo huko ufipa; angesaidia vipi labda kwa wadhifa aliokuwa nao?!
Kwa nafasi aliyokua nayo,angeweka hata tasisi au chochote kinachompa alama kua alikua kadinali.au unaonaje mkuu??
 
Kwa nafasi aliyokua nayo,angeweka hata tasisi au chochote kinachompa alama kua alikua kadinali.au unaonaje mkuu??
Alikuwa askofu wa jimbo la Dar es salaam, hivyo wajibu wake ilikuwa kwa jimbo aliloliongoza. Kanisa katoliki si sawa na hivi vikanisa unavyovifahamu.

Hujasikia makardinali wanaofunguliwa mashtaka Vatican kwa kutumia madaraka na fedha za kanisa vibaya?!
 
Wewe ni mkatoliki?vikanisa???akili za wapi hizi??? hakuna vikanisa duniani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom