Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Katika kijiji cha Mtakuja walimpata Mfalme ambae alikuwa kipenzi cha watu. Watu walimpenda Mfalme na Mfalme aliwapenda raia wake. Mfalme alirithi ufalme kutoka kwa baba yake, na alikuwa bado na nguvu zake. Raia walimtegemea jemedari huyu kuwaongoza kwa muda mrefu.
Matatizo yalianza katika kauli za Mfalme. Wazee wenye busara na waganga wa kienyeji katika kijiji kile waligundua tatizo la Mfalme. Shida ikawa jinsi ya kumfahamisha kuwa Mfalme unahitaji tiba.
Afya ya akili ni afya kama ilivyo ya mwili. Wakati mwingine chemikali na chembe hai zinazosafirisha habari zinapata matatizo. Tatizo la afya ya akili linatibika ingawa linahitaji tiba ya muda mrefu na mgonjwa awe ametulia. Lakini katika miaka ile wana Mtakuja walitegemea mizizi na miti shamba katika tiba zao.
Wote waliokwazwa na kauli za Mfalme walimsamehe baada ya kugundua matatizo yake.
Asante sana marehemu bibi yangu kwa kunisimulia kisa hiki.