Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Ndo maana kuna nchi zinaitwa first world na sisi ni third world, get that fact right kwanza kabla ya yote!
Nchi tajiri zina templates kadhaa katika profile zao, wakiamua wanajitegemea, wakiamua wanaweza kututegemea masikini kwa faida zao , wakiamua wanasaidia masikini..kuna wakati nchi hizo zinafanya mamboyote hayo kwa wakati mmoja
hadi leo dawa za kifua kikuu , hiv, zinakuja kama misaada kutoka kwa beberu, meantime copper ya zambia hadi leo hii masoko yake yapo huko huko kwa beberu.
Mama anazunguka huko kwa sababu anajua beberu haipukiki kwa namna yoyote.
She will loose some and win some games katika rounds hizo
Umeongea ukweli.kuna majinga yanatunisha kifua eti tuna madini wakati hayo madini yenyewe ili yaweze kua na manufaa na thamani lazima tuwauzie hao hao mabeberu.Tatizo liko kwenye akili zetu namna yakupiga hatua zetu uku kila mmoja akinufaika ipasavyo.Kwahiyo kushindwa kwetu kunatufanya tuwachukie mabeberu waliotumia rasilimali tulizowapa vizuri uki sisi kile tulichokipata kutoka kwao tuneshindwa kukitumia ipasavyo.
 
Naamini Tanzania inaweza kuendelea bila kutegemea misaada bali ikabaki tu kuheshimiana na kushirikiana kwenye maendeleo...

Wakubwa wa dunia wanaamini kwenye umafia kwa kuendelea kufanya wengine masikini kwa kutumia baadhibya tools zai kila mahala..Wakubwa wadunia wakigundua una mtazamo tofauti wakuwatoa watu kwenye utumwa wa kiuchumi basi hutumia tools zao na vibaraka waliopandikizwa kila mahala kukumaliza..... WaAfrica tujaribu kuwa real na Uafrica wetu tusishupaze shingo na kubabaika sana na hawa pua ndefu....
Hivi ni afrika tu ndiyo inayotakiwa kudidimizwa na wakubwa wa dunia?.Mbona ziko nchi nyingi tu uko asia zimepiga hatua kubwa ya maendeleo na hatuwasikii hao wakubwa wa dunia wakiangaika nao.Mimi bado naamini tatizo liko kwetu wenyewe.Tungekua tunajielewa kwakuacha ujinga tulipaswa tuwe mbali sana na wala hakuna ambaye angeweza kutuzuia.Tunajiona tunadidimizwa kwasababu akili zetu bado hazijataka kua huru kuanzia kwenye kufikiri hadi kutenda.
 
Wewe unaona umefika wapi kama nchi, acha kuwa mjinga basi Taifa lolote duniani ni kama mtoto anakuwa taratibu, Nyerere alipoishia mwinyi alianzia pale. JPM hakuwa malaika alifanya fyongo tu na wala nchi haijafika popote. Sema niwatanzania Wangapi wamekuwa lifted from poverty line. Uongozi wenye makelele mengi ya propaganda kutumia media bias matokeo yake ndio haya, nchi yetu imetoka mbali sana kama hujui tunu yetu kubwa tangu Taifa hili linazaliwa ni (diplomasia) upatinishi ndio Taifa kama msumbiji linatueshimu Sana. Jiulize kwanini mkapa aliwekeza sana kwenye jeshi, Sisi tulikuwa tunauwezo wakuchezea majirani tunavyotaka hata Rais nkrunzinza wa Burundi tuna mkono wetu kwa hiyo ilikuwa rahisi kuingiza chumvi yetu ya uvinza kutoka kigoma, tulienda Congo kumfurusha Kagame maana hao niwatoto wetu, mseveni wa uganga alikuwa hawezi kujamba mbale yetu tunachapa kiboko. Acha ushamba wewe, ulishafika udom ukaona uwekezaji wa serikalii, chuo Nelson Mandela, hospital ya mloganzira na Benjamin mkapa. Najua bado mtoto ukikua utaacha ujinga nchi iliingia mkosi kupata Rais mjinga
Umeandika kama una harisha huku point ikiwa 0

Hebu weka takwimu hapa tuone kiwango cha umasikini wakati wa Mkapa, JK, Magufuli na sasa Samia ili tuone kama hao wengine wameendeleza sana nchi kisha Magu ndio akaiporomosha.

Sikia bwana mdogo, nmefuatilia viongozi wote tangu Mkapa, JK Magufuli na sasa hivi bado naendelea kufuatilia awamu ya Samia.

Hakuna popote unaweza kuthibitisha kwamba nchi hii iliwahi kuwa tajiri sana ikafika kipindi ikawa masikini ikafika kipindi tena ikawa tajiri kulingana na viongozi wake!

Kiufupi hakuna takataka yeyote anaweza kunishawishi kwa chochote kila kitu naona mwenyewe.!
 
Kwani dhalimu alifanya nini, au zile brainwash za kwenye TV ndio uliona kapatia? Zile $192 alizoongopa tunawadai Barrick mlilipwa. Kile kushika uchumba cha $300m kimeshalipwa chote?
Dhalimu wako alijaribu kuwazindua watz ila vibaraka kama wale walioenda kuolewa na amsterdam wakaanza kuturudisha nyuma
 
Ukisema ukweli na kulishauri taifa unaonekana Msaliti, ukiipinga na kuikosoa serikali unaonekana CHADEMA, na adui wa Nchi.

Ukiisifia na kuipongeza SERIKALI Kwa mazuri unaonekana kuwa wewe ni CCM.
 
Dhalimu wako alijaribu kuwazindua watz ila vibaraka kama wale walioenda kuolewa na amsterdam wakaanza kuturudisha nyuma

Hamna mshamba anaweza kumzindua mtu. Yeye ndio alizinduliwa kwa kupewa urais akaanza ulimbukeni wa madaraka. Matokeo yake saa hii amekaa kwa kutulia wanaume wanaendelea na yao.
 
Huwa nawaza sana tulifikaje hapa tulipo leo,

Hivi ilikuwaje taifa lenye wasomi wazuri kabisa likaamua kufanya maamuzi ya kipumbavu ambayo hata Waroma wa kale walioishi miaka 2000 iliyopita wasingeyafanya. Hivi katika maksudi kabisa, taasisi nyeti za Tanzania ziliamini kabisa kwamba wao wangeweza kuifanya Tanzania nchi tajiri bila kushirikiana na dunia : Hivi ilikuwaje kabisa wataalamu wetu ambao wameenda shule, wanafahamu mifumo ya dunia ya kiuchumi, kiulinzi na kisiasa na wako kule USALAMA, BENKI KUU na MAMBO YA NJE wakakubaliana na huu upumbavu na kuanza kuutekeleza kabisa?

Mpangilio wa dunia yetu ya sasa uliwekewa msingi mwaka 1814 kule Vienna baada ya miaka 25 ya vita za mfalme Napoleon Bonaparte. Mwanamfalme Von Matternich alifahamu kabisa ili dunia isirudie kuingia kwenye songombingo la vita au kadhia yoyote ile, basi ni lazima watengeneze mfumo ambao uko kama utandu wa bui-bui: Kwamba maamuzi ya nchi moja yakifanyika lazima yaathiri nchi zote, hivyo nchi lazima zikubaliane kwenye baadhi ya mambo muhimu yanayowagusa wote. Ndiyo nadharia ya MZANI WA NGUVU (Balance of Power) ikazaliwa.

Mfumo wa dunia ya yetu hii tunayoishi leo hii umejengwa na matukio yaliyotokea miaka ya 1913, 1914, 1918, 1920, 1927, 1928, 1933, 1935, 1939, 1941, 1944, 1945, 1947, 1948, 1971 na 2001 . Kiufupi mlolongo wa matukio haya yafuatayo ndiyo yanatoa mwelekeo mzima wa mwenendo wa dunia yetu ya leo : Nashauri tufanya utafiti wa ndani kuhusu hili.

Formation of the Federal Reserve, World War I, Versailles Peace Treaty, Formation of League of Nations, Signing of Kellog-Briand Pact, The Great Depression, The Monte-Video Convention, America's Abolition of Gold Standard, World War II, The Bretton Wood Agreement, Formation of UNO, Signing of the GATT, Publication of the Universal Declaration of Human Rights, Nixon's Abandonment of the Gold Standard and China's Admission to the WTO n.k.

Mtaalamu yoyote yule wa Uchumi, Diplomasia, Ulinzi na Sheria ni lazima afahamu fika kuhusu haya ninayoyasema hapa. Kwamba dunia nzima tuko ndani ya utandu moja wa bui-bui. Huwezi kufanya jambo lolote lile ukiwa nje ya hapo. Ndani ya huu utandu wa bui-bui kuna kila aina ya watu: Wema na wabaya, Huru na watumwa, Masikini na tajiri, Wenye matumaini na wasio na matumaini, Wababe na dhaifu na Waamini Mungu na Maadui wa Mungu.

Huu ndiyo mfumo wa dunia (The World Order), huwezi kufanya maajabu yoyote yale ukiwa nje: Hata mataifa makubwa yenye nguvu duniani yanaheshimu huu mfumo kwasababu yanafahamu siku mfumo huu unaharibika basi ndiyo utakuwa mwisho wao. Hivyo kuna baadhi ya sheria hata yenyewe yatazifuata tu kwasababu zina manufaa kwao. Mwandishi George Orwell kwenye The ANIMAL FARM aliwahi kusema "All animals are equal, but some are more equal than others" hivyo hata kama tunataka usawa kuna wale waliotutangulia watakuwa mbele yetu kwenye baadhi ya mambo tu.

Sasa kinachoumiza wasomi wa Tanzania wenye PhD za sheria, uchumi na diplomasia. Huku wengine wakiwa na shahada kwenye masomo ya ulinzi, usalama na sayansi za vita wakiwa na akili timamu kabisa, wakaamua kuwa wapumbavu. Wakatundika elimu zao nyuma ya milango na kuanza kutekeleza jambo ambalo hata watu wa kale walioishi miaka 2000 hawakuwahi kuliwaza. Tanzania ina matatizo mengi, lakini ilikuwa inarekebishika vizuri tu kwasababu waliofikisha nchi yetu hapa wanafahamika na tunakula na kunywa nao kila siku.

Kuanza kulaumu mabeberu peke yake haisaidii kwasababu kuna wenzetu ambao wamefanikiwa kutumia mifumo hii-hii ya mabeberu kuwashinda mabeberu kiuchumi, kiulinzi na kisiasa. Ukweli ni kwamba huu mfumo umejengwa na mabeberu lakini hata walioujenga hawaundeshi wanavyotaka wao. Mataifa ya Magharibi ndiyo waanzilishi wa World Trade Organization (WTO) lakini leo hii, WTO imemnufaisha Uchina kuliko tangu alivyojiunga nao mwaka 2001 na mpaka sasa wanajutia kumkaribisha.

Nchi kama Singapore, India, Korea-Kusini na Brazil wamewezaje kucheza vizuri kwenye huu mfumo wa mabeberu hadi kufikia kuwango cha kuwashinda mabeberu kwenye baadhi ya mambo ??? Inahitaji akili ya ziada kutoka kwa Mungu ili kuweza kucheza kwenye huu mfumo. Raisi Donald Trump alijaribu kuitoa Marekani kwenye huu mfumo wa Vienna, lakini pamoja na maguvu yote ya Marekani alifanikiwa ???

Lakini leo hii kuna watu wako ndani ya IDARA ZA USALAMA ZA TANZANIA waliamini kabisa kwamba Tanzania inaweza kujitenga na dunia bila kupata madhara. Yaani waliamini kabisa na wengine bado wanaamini kabisa. Kuna wengine bado wanaamini kwamba mfumo wa Kileninisti na Kimaksisti (Marxist-Leninism) unaweza kutumika kuikomboa Tanzania. Sawa, lakini hata walioutuletea huu mfumo Warusi na Wachina, wamebadilisha sana baadhi ya hizi falsafa.

Dunia ya nchi moja kutawala wengine (Uni-Polar World) au nchi mbili kuamulia dunia nini kifanyike (Bi-Polar World) unakufa taratibu, ndiyo maana Marekani na Urusi wanapata shida kukubaliana na huu ukweli. Wao kama mataifa hawaanguki na bado wana nguvu, ila tu ni kwamba mataifa yale madogo na masikini kama Vietnam, Poland, Mexico yamekuwa makubwa yenye uchumi unaokua kwa kasi sana.

Tanzania tuliachiwa mtaji mkubwa sana kidiplomasia, ambao ulitujengea SOFT-POWER na INFLUENCE ambayo ilifanikisha ulinzi na usalama wa Tanzania kikanda na kidunia kwa kiwango kikubwa sana. Tuliingia sehemu ambazo hata nchi kubwa hazikuweza kuingia, tulipata taarifa nyeti kabla hata baadhi ya mataifa makubwa hayajazipata, tulipewa heshima ya kipekee (Special Treatment) ambayo mataifa mengine yenye uchumi mkubwa kuliko sisi barani Afrika hayakupewa.

Tuliogelea bwawa moja na mababeru, wakomunisti, wajahidina na wazayuni lakini tulitoka salama, kesho tena tukarudi kuogelea. We were a Shrimp among Whales, lakini bado tuliheshimika mno. Lakini leo hii hebu angalia, ile nguvu yote ambayo Mzee Nyerere na Raisi Mkapa walitutengenezea, imemomonyoka kisa kikundi cha watu wachache wasiokuwa na uelewa mpana wa mahitaji ya nchi yetu na nafasi yetu hapa ulimwenguni.

Binafsi naamini ili tuweze kutoka hapa tulipo ni lazima NYUMBA ISAFISHWE aidha mbele ya majirani au kisiri. Mambo ya UHAINI, KUHODHI MADARAKA, KUPANGA KUUA MARAISI WASTAAFU,KUSHIRIKIANA NA MAADUI WA TAIFA na KUWINDANA KWA KUTUMIA MAKUNDI NDANI YA TASISI ZA KIUSALAMA (Cloack and Dagger Diplomacy) tulikuwa tunayasikia nchi jirani tu: Kwetu sisi yalikuwa ni MWIKO KABISA. Vitendo vya kihaini tulishaachana navyo awamu ya kwanza. Lakini leo kuna kakundi kalifikiri kabisa kangeweza kutupangia sisi Watanzania nani awe Mkuu wa nchi kweli?

Halafu bado haka kakundi kanalelewa tu: Kuhakikisha kwamba nchi haiwezi kurudi tena kule ilipotoka there's one place these people belong : The Cemetery, A Noose or A Bullet in the head!!! A prison term is not enough for these ruthless and deranged fanatics (This is legal, legitimate, justified and righteous).

Mara nyingine huwa naumia sana kuhusu Tanzania, natamani hata nisingekuwa nayafahamu haya yanayondelea.....
Hongera kwa makala nzuri ambayo umeiandika kwa uzalendo mkubwa kwa Nchi yako .Lakini kwa Sasa hivi hatuna viongozi wenye uweledi wa kulipeleka mbele Taifa letu. Ukitaka kuona Hilo ebu cheki kesi ya Mbowe ndo utaamini aina gani ya viongozi tulionao.Hata hivo kiunabii Tanzania ipo gizani na hiki kipindi kitapita ili aje atakaetuoeleka mbele.Tafuta ukweli kuhusu utawala wa Tanzania utaelewa nini kinaendelea kwenye nchi yetu.Hivi vitu wanavijua wachache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Malcom Lumumba nitasema ukweli daima, fitna kwangu mwiko. Raisi Magufuli kuna mambo mengi sana aliyafanya vizuri lakini mambo ya nje na diplomasia haviko kwenye hiyo orodha. Dunia yetu ya leo siyo ile ya karne ya 18 na 19 ambayo ulikuwa unaweza kujifungia tu (Isolationism) halafu mambo yakawa yanaenda tu. Tunaishi kwenye ulimwengu wa utandawazi, hivyo ni lazima tunavyojenga ndani na nje tujenge: Lazima kuwe na uwiano mzuri......
Ndugu yangu Malcom, in all honesty, taja machache (notable) kati ya hayo mengi sana Magufuli aliyofanya vizuri.
 
Sasa mjomba ni kweli huwezi endelea bila kujihusisha na dunia sija bisha lakini mm nimekwambia unabidii uanze kujenga kwanza ndani ndiyo ufwate hivi hukuona like jambo la kwenda uchumi wa kati lingeleta tija Katika uwekezaji. By the way magufuli hatunaye Tena Sasa turudi kwa waliopo Sasa hivi unadhani viongozi wanavyo zunguka ni kuijenga uhusiano wa dunia ni kuleta tija mtu unazunguka nchi za watu kwako umeme ni shida, maji ni shida hafu utaleta uwekezaji ni mwekezaji chizi pekee atakae wekeza kwa ajili ya hasara. Yaani beberu yeye ni mtu wa 1 profit, 2 profit,3 profit huwezi enda na pua yako kwa beberu akategemea kuwini. Hivi hujawahi ishi na mtu kakuzidi kiuchumi mbali lakini akakuheshimu kwa jambo moja ambalo ni dogo kwakuwa yeye haliwezi. Ndio hivyo Tanzania inabidii sisi tutambue nini tunaweza na Nini hatuwezi kile tuchoweza tunakifanya ambavyo hatuviwezi tunashirikiana na wengine hichi ndio ambacho jpm aliweza kutaka mtanzani afikiri anaweza. Sasa kuzunguka zunguka kwa kuomba misaada na kuona Kama wananchi ni visiki hatuwezi chochote.

Umeegemea kwenye point ya mwisho kabisa, na hayo mawazo yako ni yakimaskini na kutokujiamini. Baadala ya kuchakata kichwa tunafanyaje na rasilimali zetu. Unakimbilia kujihusisha na dunia ndo wewe utakuja kutusainisha Hadi ushoga ili upate misaada
Una mawazo mazuri lakini still hujumuelewa vizuri mwamba " Malcolm'' kuhusu diplomasia uwezo wa kidiplomasia ambao kama nchi ilikuwa ni tunu yetu ya Taifa. Mtoa mada yuko very clear kwamba nchi yetu ilikuwa isolated na jinsi dunia invyokwenda kwa sababu ya uhafidhina(conservative)wa kiongozi aliepita
Umeandika kama una harisha huku point ikiwa 0

Hebu weka takwimu hapa tuone kiwango cha umasikini wakati wa Mkapa, JK, Magufuli na sasa Samia ili tuone kama hao wengine wameendeleza sana nchi kisha Magu ndio akaiporomosha.

Sikia bwana mdogo, nmefuatilia viongozi wote tangu Mkapa, JK Magufuli na sasa hivi bado naendelea kufuatilia awamu ya Samia.

Hakuna popote unaweza kuthibitisha kwamba nchi hii iliwahi kuwa tajiri sana ikafika kipindi ikawa masikini ikafika kipindi tena ikawa tajiri kulingana na viongozi wake!

Kiufupi hakuna takataka yeyote anaweza kunishawishi kwa chochote kila kitu naona mwenyewe.!
Unajinasibu kwa kuwa muelewa lakini bado una mihemko tu kaa mtoto mdogo anaeweka kila kitu mdomoni akizani ni chakula. Unaweza kuita wenzako takataka kumbe wewe mwenyewe unaishi dampo. Jifunze kuna nchi na taifa, huwezi kujenga nchi huku taifa likigawika, maendeleo sio magorofa wala kelele na kibuli alichokuwa nacho mshamba flani hivi ila maendeleo ni Maisha ya watu
 
Shida ya viongozi wengi ni Ubinafsi, ujinga na kutokuwa na muono wa miaka mingi ijayo.

UCCM na UCHADEMA pia umeathiri Kwa kiasi kikubwa taifa letu.

Kila kitu kinachukuliwa Kwa Mlengo wa kichama.

Vijana ambao wanatarajiwa hapo baadaye waweze kulinda na kuliendesha taifa hili, kulishauri na kulidhibiti ndio hawa ambao kutwa kuchwa wanaleta UCCM na UCHADEMA.

Ukisema ukweli na kulishauri taifa unaonekana Msaliti, ukiipinga na kuikosoa serikali unaonekana CHADEMA, na adui wa Nchi.

Ukiisifia na kuipongeza SERIKALI Kwa mazuri unaonekana kuwa wewe ni CCM.

Sijui hizi akili-mavi zilizojaa vichwani mwa wengi asili yake ni ipi.


Nchi hii ni nzuri Kama ubinafsi utaondolewa, uchama utaondolewa.
Bwana Heriel. Usitake kurahisisha mambo. Hakuna tatizo la “UCHADEMA” wala “UCCM” wala “uchama”. Kuna tatizo la kusimama kwenye UKWELI na kwenye UONGO. Ukisema UBINAFSI sawa.

Wako wengi sana wanaonufaika na uongo. Hivyo ukweli unapigwa vita kwa kila nyenzo. Tena kauli yako kuwa tatizo ni “uchama” wanaipenda sana. Ndio hao wakizidiwa hoja hudai “maendeleo hayana chama”, “maendeleo hayataki siasa bali vitendo tu”, “usiwaamini wanasiasa”, “achana na itikadi; uzalendo kwa nchi tu”.

Serikali yetu (ya CCM) kwa kiwango kikubwa husimama kwenye uongo na propaganda. Wakijitokeza watanzania kukosoa, kutoa taarifa sahihi na ushauri bora huitwa “wapinzani”, “ wasaliti”, “pinga pinga”, CHADEMA”, “wachaga”.

Wako pia wanaounga mkono upinzani/CHADEMA hata katika mapungufu ya msingi. Wanabishia ukweli na wakati mwingine kuukalia kimya. Lakini hawana athari sana kwenye nchi zaidi ya vyama vyao.

Wanaotoa matamko ya kuiunga mkono serikali hata katika makosa wengi ni wanapropaganda na wasaka fursa ndio maana wanaitwa “CCM”. Vile vile wako mashabiki wa watu binafsi wasioangalia ukweli bali propaganda kama “MATAGA”, “sukuma gang”, “msoga gang”, “wakojani”, n.k.

Tatizola Tanzania ni jamii iliyojengeka kusaka fursa za ulaji tu. Hakuna cha siasa makini, vyama makini, wala uongozi bora.
 
Hakuna ambae hakutaka kushirikiana na nchi nyingine ila kushirikiana kwa kutunyonya hilo ndo tulikataa awamu ya tano na inatakiwa iwe hivo kwa nchi zote za Africa gasa kusini mwa jangwa la sahara! Ile mikata ya kusaini mi nakuletea kandamili ww nipe Tanzanite hatuitaki

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfano mlijitoa mahakama ya haki za binadamu Africa, mlijitoa Open Governance Initiative ambayo ina advocate uwazi na uwajibikaji serikalini n.k. let alone influence yetu kidiplomasia AU,SADC, na EAC ilishuka sana hatukua power brokers/Regional Kingpins kama enzi zile za 70s-90s.

Nakumbuka hadi Kuna sheria iliundwa ikitaka arbitration eti zisikiliswe humu humu nchini kwa mahakama za ndani?? Kuna mindset mbovu ilijengeka kwamba tunaweza fika mbali bila input ya dunia.

Weird!
 
Yawezekana hujamwelewa Lumumba, yeye amejikita zaidi katika awamu ya tano...

Ndio maana naamini kabla na baada ya awamu ya tano, nyinyi wataalamu mlipewa nafasi na makafanya kazi

Swali langu, kabla na baada ya Magufuli mmeisaidiaje Tanzania katika vipengele alivyotaja Malcom?

Asante.
Ndio maana wanataka Nchi ifanyiwe format ili kila mwenye uwezo apewe nafasi
 
Akili za Kabudi hizo. Yaani ukitaka kuteseka mpe masikini cheo na hela.
Alikuwa akinywa sharubati na kutafuna korosho kwenye vikao vya baraza la mawaziri huku anapigwa na kiyoyozi anasahau matatizo yoye anaiona Tanzania ipo sawa na USA anaanza kuwakemea masponsa wake 😁
 
Alikuwa akinywa sharubati na kutafuna korosho kwenye vikao vya baraza la mawaziri huku anapigwa na kiyoyozi anasahau matatizo yoye anaiona Tanzania ipo sawa na USA anaanza kuwakemea masponsa wake 😁
Kumuamini binadamu ni kazi sana. Halafu nilichogundua yule Mzee hanaga aibu.
 
Hakuna wakumuogopa ila ukweli lazima tuwe makini. Kwani nani ambae hajui kuwa wale watu hawataki nyie mpate? Ukitaka kuwa rafiki mzuri wa nchi za Kimaghalibi linda maslahi yao basi hapo umemaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa mada ametoa mfano wa baadhi ya nchi zilikuwa kwenye lindi la umaskini lakini wakaweza kujiposition ndani ya system na wakatoka kiuchumi. Je, hao wazungu wasiotaka tuendelee hawakuwepo wakati nchi hizo sijapiga hatua?

Mtoa mada bila shaka hakuzitaja nchi hizo kwa bahati mbaya bali ni kuleta fikra kwamba inawezekana kutengeneza good cooperation framework ya kuweza kuendelea. Je, hujaona kipengele hicho?
 
Hivi Nyakubonga kuna Raisi ambaye alifanikiwa kukuza uchumi wa Tanzania kwa kupitia Diplomasia kama Mzee Mkapa ??? Japo alikuwa na makosa yake mengi tu, lakini alitumia vizuri mtaji ulioachwa na Mzee Nyerere. Unakumbuka baada kwenda G8 nini kilitokea: Hivi
Mkuu kwanini unambana Magufuli kwenye angle moja tu(diplomacy)?

Je nchi haiwezi kuendelea bila diplomacy?

Kipindi cha kikwete tulikua vizuri sana kwenye diplomasia na uhusiano wa kimataifa, lakini tuliambulia nini kama taifa?

Magufuli hakua vizuri kwenye diplomasia lakini ni kweli hakufanya kitu kama tunavyoaminishwa?
 
Una mawazo mazuri lakini still hujumuelewa vizuri mwamba " Malcolm'' kuhusu diplomasia uwezo wa kidiplomasia ambao kama nchi ilikuwa ni tunu yetu ya Taifa. Mtoa mada yuko very clear kwamba nchi yetu ilikuwa isolated na jinsi dunia invyokwenda kwa sababu ya uhafidhina(conservative)wa kiongozi aliepita

Unajinasibu kwa kuwa muelewa lakini bado una mihemko tu kaa mtoto mdogo anaeweka kila kitu mdomoni akizani ni chakula. Unaweza kuita wenzako takataka kumbe wewe mwenyewe unaishi dampo. Jifunze kuna nchi na taifa, huwezi kujenga nchi huku taifa likigawika, maendeleo sio magorofa wala kelele na kibuli alichokuwa nacho mshamba flani hivi ila maendeleo ni Maisha ya watu
MImi sikatai kuwa jamaa aliharibu diplomasia ila mtoa uzi katumia point moja ya diplomasia kumponda kabisa jiwe kuonesha hafai kabisa na katumia point hiyohiyo kuwapaisha baadhi ya watu.

Madhaifu ya jpm ya kidiplomasia yanerekebishika lakini madhaifu ya wanadiplomasia anaowataja mtoa maada yakina nape na January makamba huo sio udhaifu Bali ni msiba wa vizazi na vizazi mtu anawaza kubinafsisha Tanesco, juzi juzi kaulizwa kwanini umeme unakatika alichokijibu anakijua mwenyewe.

Mtoa maada angeweza kutoa maada yake kwa kuangalia pande mbili angeanisha magufuli alichokosea na angesema Nini viongozi wabebe kutoka kwa magufuli. Kwa maana alichokuanacho magufuli ni kikubwa kawazidi Cha hao madiplomasia
 
Mkuu kwanini unambana Magufuli kwenye angle moja tu(diplomacy)?

Je nchi haiwezi kuendelea bila diplomacy?

Kipindi cha kikwete tulikua vizuri sana kwenye diplomasia na uhusiano wa kimataifa, lakini tuliambulia nini kama taifa?

Magufuli hakua vizuri kwenye diplomasia lakini ni kweli hakufanya kitu kama tunavyoaminishwa?
Jakaya Kikwete naye alikosea na tukamsema, uzuri alikuwa ni mtu ambaye anapenda kusikiliza ushauri wa kitaalamu, kufuata kanuni taratibu na aliheshimu sheria za kimataifa: Ndiyo maana hata aliposhindana na baadhi ya mataifa alikuwa kwenye upande salama kwasababu alifahamu fika kwamba hakuna nchi inayoweza kuendelea duniani bila diplomasia.

Sasa Raisi Magufuli tukisema kwamba alikuwa haheshimu kanuni na taratibu, na alikuwa ni mtu ambaye hataki ushauri hata kwenye mambo nyeti mbona mnakasirika wakati ushahidi uko mwingi tu. Mimi ninayezungumza na wewe nakwambia ukweli kwa yake ambaye nimeyaona kama mwanasheria. Nimekaa na watu ambao ni walikuwa washauri wa karibu wa Raisi Magufuli, na wanasema kweli alivurunda. Mengine hatuwezi kuyaweka wazi tu,....

Nikuulize labda hivi unafahamu kwanini tulikuwa tunawinda sana na mabeberu hadi wakakamata ndege zetu, ambazo tukawa tunaogopa hata zisiruke nje ??? Tanzania tuna Bilateral Investment Agreements (BIT's) na nchi zisizopungua 30. Sasa Raisi Magufuli hali akifahamu kwamba kuna utaratibu maalumu wa kufuata unapotaka kuwashughulikia mabeberu, yeye akaamua kufanya kama anavyoshughulika na BAVICHA.

Nchi ikawa inaingia kwenye taharuki zisizo na msingi kisa tabia yake ya kutopenda kusikiliza na kujifanya anajua kila kitu. AU haya nayo umeyasahau mkuu ???
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom