Ilikuwaje Mkoa wa Mara ukaitwa 'Jamhuri ya Watu wa Chui'?

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,630
3,578
Mtu anayejua historia ya mkoa wa mara ambao kuna kipindi ulijitenga ukaanzisha jamuhuri ya watu wa chui aweke hapa
 
Nyamhanga aliteremsha Bendera ya Tanzania na kupandisha ngozi ya chui na kutangaza rasmi kuwa hiyo si tena Tanzania , kuanzia siku hiyo majeshi yalikusanywa nchi nzima kama vile kulikuwa na vita ya Kagera.

Mapambano yaliendelea kwa siku zipatazo 7 hivi kabla ya Nyamhanga kupitia chini ya nyuma ya mtungi na kupotelea bondeni.

Kama ilivyokuwa kwa Hitira kuna habari za kutatanisha kuhusu huyu bwana baada ya vita kwisha. Kuna wengine wanasema yalitupwa mabomu mengi sana huko alikokimbilia na wengine wanasema alitorokea nje ya nchi.

Kuna Simulizi nyingi tu ambazo siwezi kuziandika hapa hasa kwa sababu zinahusiana na ushirikina wake, nami sina imani na ushirikina.
 
Nyamhanga aliteremsha Bendera ya Tanzania na kupandisha ngozi ya chui na kutangaza rasmi kuwa hiyo si tena Tanzania , kuanzia siku hiyo majeshi yalikusanywa nchi nzima kama vile kulikuwa na vita ya Kagera. Mapambano yaliendelea kwa siku zipatazo 7 hivi kabla ya Nyamhanga kupitia chini ya nyuma ya mtungi na kupotelea bondeni. Kama ilivyokuwa kwa Hitira kuna habari za kutatanisha kuhusu huyu bwana baada ya vita kwisha. Kuna wengine wanasema yalitupwa mabomu mengi sana huko alikokimbilia na wengine wanasema alitorokea nje ya nchi.Kuna Simulizi nyingi tu ambazo siwezi kuziandika hapa hasa kwa sababu zinahusiana na ushirikina wake, nami sina imani na ushirikina.

Mimi nadhani aliitwa Nyamaghanya
 
Ha haaa! Leo asubuhi ktk baragumu ch.ten kulikua na mzee mmoja (mwanajeshi mstaafu)alikua anazungumzia miaka 49 ya muungano na ndipo alipomuuliza mcharo mrutu (mtangazaji ch.ten)kuwa anafahamu kuwa ni mkoa gani kuna mtu alipandisha bendera(ngozi ya chui)? Nashukuru mlioweka historia hii maana hata mimi nilikua sifahamu hili jambo.
 
Nyamaghanya alikuwa jembe kweli na ni shujaa wa kweli wa mkoa wa mara nakumbuka mwaka 1982 alitangaza jamhuri ya watu wa chui nami nikiwa miongoni mwa wakazi wa nchi yake makao makuu yakatangazwa kuwa ni GIBASO na mishahara ya watumishi wake ni ng'ombe alikuwa na jeshi hodari sana likiitwa Esaiga ya gesambiso na vijana wa kati ambao walikuwa hodari wa kupiga mishale ndipo mchongameno akaamua kumwaga jeshi lake toka zenji kuja kumsaka shujaa wa wanamara wakashindwa kumkamata ikabidi watumie mbinu ya kupitia kwa mke wake mdogo ndipo akauwawa au akajiua mwenyewe kwenye mashimo ya gwisalaa hakukamatwa wala hakuzikwa mwili wake ulifichwa ili kukwepesha mauaji zaidi toka jeshi lake
 
Jamhuri ya watu wa chui...niambie kwa kiinglish ndio inaitwa ....repuplic..mmnh, .out of curiosity.
 
Nchi pekeeambayo historia yake haiwekwi wazi kwa vizazi hadi vizazi na kubaki na kazi ya kulisha vizaze vyake historia za nchi za watu

Jamani historia sio tu ya mambo maazuri ya kusaidia ukombozi wa nchi nyingine bali hata yale ambayo hayatufurahishi.

Kuna haja ya historia kama hii kufundishwa kwenye mashule siyo kuleteana mambo ya kina sijui ndiyo wa kina Mansa Kan Kan Musa wakati kwetu kumbe kuna historia iliyoshiba sema inafichwa.

Kuna ile nyingine nayo ya uasi wa Jeshi...Imefiiiiichwaaaaaa.....fundisheni hizi kwenye masomo ya historia ya taifa letu bwana sio kuzificha na kutujia na sifa za kina Mkwawa tu
 
Mkuu unaweza kutupatia hii kwa undani zaidi?

Nadhani Kichuli atakuwa na details zaidi. Namwomba afunguke. Kumbuka siku hizo vyombo vya habari vilimilikiwa na serikali na waandishi wa habari walikuwa ni waajiriwa wa serikali. Lakini kama mtu alikuwa Tarime miaka hiyo ya 1981-82 hii habari haikuwa siri hata kidogo.
 
Inasemekana katika vita vya Uganda, majeneza yalibeba bunduki jamaa akiziamishia Musoma. Baada ya vita na Uganda, akatengeneza jeshi lake na akajitangazia nchi huru, bendera (ngozi ya chui) ikasimama juu ya mlingoti mapambano yakaanza. It was not that much easy kusambaratisha jeshi lake na inasemekana Mwl. Nyerere aliumizwa kichwa sana na huyu jamaa, ila at last waliweza m-defeat na kurestore order.
 
Watu wa Historia wafanye kazi yao ku-research on this historical event....itapendeza sana kuufahamu ukweli na hata ule wa Zanzibar na Okelo!!!
 
HAHAHA ...

Kumbe Mtakatifu Nyerere watu walimu-attempt zaidi ya mara moja!

Lakini naye kazidi..aliwatia watanzania katika mashaka na umasikini usiokuwa wa lazima
 
HAHAHA ...

Kumbe Mtakatifu Nyerere watu walimu-attempt zaidi ya mara moja!

Lakini naye kazidi..aliwatia watanzania katika mashaka na umasikini usiokuwa wa lazima
Hapana. Huyu alikuwa hana nia ya kupindua serikali ya Tanzania. Yeye alichofanya ni kujimegea eneo lake na kutangaza Jamhuri ya watu wa chui. Na Jamhuri yake ilikuwa inaishia eneo moja tu Tarime.
 
Mkuu kichuli nimekupata vyema ngoja nirare na mama bhokhe sasa kesho niwahi sabhato mura!
 
HAHAHA ...

Kumbe Mtakatifu Nyerere watu walimu-attempt zaidi ya mara moja!

Lakini naye kazidi..aliwatia watanzania katika mashaka na umasikini usiokuwa wa lazima
, how dare you are kumkashifu Mwalimu?

Kama ni hivyo Mandela akifa basi ufurahi maana walikuwa na ushoga mkubwa na mwalimu, hata alipostaafu akaja Tanganyika kuaga, na mimi nilikuwepo Taifa siku ile kuimba ule wimbo wa 'Julias Nyerere, hatukufanana nae'
 
Back
Top Bottom