Ilikuwaje Mawaziri na Vigogo wengi wakawa Wasukuma awamu ya 5?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
6,174
2,000
Hivi ni kwa bahati mbaya tu au ilipangwa awamu ya tano kuanzia mawaziri,makatibu na sekta nyeti zote za nchi kukamatwa na wasukuma?

Mimi binafsi sina shida na wasukuma ni ndugu zangu tena wakwe kabisa japo najua mwendazake alikua keshawapandikiza roho ya kuanza kujikuta wao tu ndo wastahili.

Ilifika mahali ukimtania msukuma unanyooshewa kidole kwamba unampeeb rais.

Niachane na hayo mimi swali langu tu ilikuaje wakati wa awamu ya tano mawaziri makatibu manaibu waziri jeshini usalama na kila mahali wakajazwa watu wa kabila la wasukuma tu?Jee ilikua ni bahati mbaya au mipango mkakati wa baadae?maana hata bungeni walichomekwa hata mmoja akatoa waraka wa kuundwa jeshi la wasukuma.

Mimi nawaza tu rais angekua katika mkoa flan hv wale jamaa wa kanda ile ya kule penye maendeleo sana na ateue hata waziri mmoja tu wa kutoka kanda hiyo si angetukanwa,kukemewa na kulaaniwa nchi nzima kwamba ni mkabila?ila kwa wengine ni sawa?hii sio haki ni mkuki kwa nguruwe...watz wote ni sawa ukabila ni mbaya sana.

Haya turudi kwenye swali la msingi swali langu tu ilikuaje wakati wa awamu ya tano mawaziri makatibu manaibu waziri jeshini usalama na kila mahali wakajazwa watu wa kabila la wasukuma tu?Jee ilikua ni bahati mbaya au mipango mkakati wa maksudi?pia angalia kanda ya ziwa kwa ujumla haya angalia marc ,madc na maded wilaya teuzi zilijaa wasukuma watupu.

Haya mashirika ya umma teuzi zilitoka ikulu walijazwa wasukuma watupu huko jeshini ndo usiseme huko polisi ndo usiseme Halmashauri ndo usiseme yaani ukabila mtupu hata washauri wake walikua wasukuma watupu.
 

Mr Excel

JF-Expert Member
Jul 31, 2021
449
1,000
Mpaka umeuliza hii ina maa unajibu tayari na uchunguzi unao tupe jibu lako kwanza na evidence la jibu lako then ndiyo tuchangie na sisi juu ya huu uzi
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,160
2,000
Kims mambo mengine tuwe na aibu hivi jafo, mpango, mkumbo, mkenda, ndalichako, nk ni wasukuma? AIBU uzushi haufai halafu anayezushiwa keshaitwa.
Doto Biteko, kiasili ni mtusi
Ndalichako, kiasili ni mhutu
Mpango ni muha
Marehemu mwenyewe, kiasili ni mtusi

Lakini mmekuwa mkiwajumuisha wote kuwa ni wasukuma. Ni kweli kuwa marehemu alikuwa mbaguzi. Zaidi ya 80% ya teuzi zake ilikuwa kutoka kanda ya Ziwa.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
88,084
2,000
Doto Biteko, kiasili ni mtusi
Ndalichako, kiasili ni mhutu
Mpango ni muha
Marehemu mwenyewe, kiasili ni mtusi

Lakini wamekuwa wakiwajumuisha wote kuwa ni wasukumu. Lakini ni kweli kuwa marehemu alikuwa mbaguzi. Zaidi ya 80% ya teuzi zake ilikuwa kutoka kanda ya Ziwa.
Marehemu hasemwi vibaya
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,617
2,000
Unarusha maneno tu bila ushahidi wowote....

Nilikuwa mpinzani wa serikali na utawala wa aliyekuwa Rais, Mwendazake Magufuli....

Lakini si kweli kuwa katika baraza lake la mawaziri [cabinet], mawaziri wote walikuwa wa kabila lake la wasukuma...!!

Labda kidogo ungeeleweka kama ungesema wengi wa mawaziri katika cabinet yake na wakuu wa taasisi na idara nyeti za umma/serikali alirundika watu wa kanda atokako - kanda ya ziwa especially wasukuma....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom