Uchaguzi 2020 Ilikuwaje Deo Mwanyika wa ACACIA aliyehukumiwa kwa Uhujumu Uchumi achaguliwe na CCM kugombea Ubunge Njombe Mjini?

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,681
3,065
Kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akijigamba kuwa anapambana na mafisadi wakwepa kodi na wahujumu Uchumi pamoja na mabeberu kwa kupitia kauli yake ya vita ya kiuchumi.

Huyu Mwanyika ndo Rais aliyetutangazia kuwa amawasiliano na wanasiasa wa upinzani ili wamuhujumu hadi kutoa ile kauli yake ambayo ilikuja kufanya kazi Sept 2017 kuwa kuna wasaliti katika vita na wanajeshi wanajua msaliti wanamfanyaje?

Ikiwa mtu alihukumiwa palipo shaka kuwa alikwepa kulipa kodi na kupigwa ya bilioni 2 je kwa hayo makando ya uhujumu uchumi na kukwepa kulipa kodi na kuhukumiwa bado anafaa.

Au huyu mwanyika pale Mgodini alikuwa ni Afisa Kificho(undercover) au alikuwa Afisa Kipenyo (penetration officer) au ndo kama yule DSO wa Ngorongoro alokamatwa na kwa kuhongwa magari na Mwarabu na hatujasikia tena kesi yake.

Sitaki kusemea sheria na katiba ila naomba tusemee utamaduni wetu na Rais wetu anaepambana na mafisadi ni kweli Mkuu anapambana na mafisadi majizi na wala rushwa au ni selective nani aachwe nani afungwe.

n2.PNG

Kama niliyemsema siye na majina yamefanana nitangulize msamaha.
 
Magufuli anazuga kupambana na mafisadi, kinachofanyika ni sawa kukiita state sponsored robbery, watu wanaamua tu kulipa hela ili wawe huru.

Tizama akina Sethi waliogoma kulipa hela, hakuna ushahidi wowote wa maana unaopelekwa mahakamani ili wahukumiwe, kwa sababu haupo!

Justice delayed is justice denied.
 
Kama niliyemsema siye na majina yamefanana nitangulize msamaha.
Mkuu huyu ndiyo huyo huyo wa Acacia na pia mgombea Ubunge kwa ticketi ya CCM. Kuna video mtandaoni akiomba kura (Njombe) na aliulizwa kuhusu swala hili akahakikisha ni yeye na akajitetea. Lakini swali lako linafikirisha. Mwenyekiti kampitishaje hiyo ni siri yake. Huyo ndio JPM aliewahi kusema "inategemea nimeamkaje" huwezi kumtabiri. Au walimsingizia Deo wa watu?
 
Personally namfahamu Deo, sijui huko kwenye makashfa ya Acacia Kama Kuna ukweli au lah, Ila ni mmoja wa watu nilio enjoy nao kufanya kazi nae, ana utu na ana vinasaba vyote vya kutosha kua kiongozi, nimefurahi kuona anasimama Njombe, na ni mtu anaekubalika mno, Hilo Jimbo tayari Deo ni mbunge,

Namuombea mafanikio awe sehemu ya mawaziri endapo ccm watachukua nchi.
 
Ndio maana tunasema Mzee yule tatizo lake kubwa ni hana principle.

Hana anachokisimamia kutoka moyoni, muda wote, kwa yeyote, kwa hali yeyote.

Kila kitu kwake kinazungumzika, kina maelewano, kina bei. Hata yeye mwenyewe anazungumzika.

Utaratibu wa kukata jina una maana gani, unatumika nyakati gani kama humkati convicted felon uliyesema ni msaliti anaehujumu nchi kwenye vita ya kiuchumi kwa kutoa siri za nchi?
 
Back
Top Bottom