Ilikuwaje, baada ya 2005, CDM kufanikiwa kuipiku CUF katika kukubalika huku bara?

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,014
2,000
Umesahau waraka wa kikristo uliosambazwa kwa waumini wa kikristo hadi katika ngazi ya jumuia kuhimiza kuichagua chadema?

Wasimamizi wa mikutano hiyo walikuwa mapadre

Nafikiri unafahamu siyo wakristo wote ni wakatoliki. Na kwa taarifa yako Pengo hana ushawishi wowote kwa waprotestanti. Na kwa waprotestanti Malasusa hana ushawishi kwa walokole. Na kwa walokole Kakobe hana ushawishi kwa mama lawakatare....the list goes on. Kimsini wakristo hawana block vote kama unavyodhani. Wakristo wana udhaifu mwingi lakini udini kuchanganya na siasa sio miongoni mwao.
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Unajua Gagnija kama kitu kikisemwa na wewe huchukui initiative yeyote kuwa mbali nacho hata kama ni cha uongo watu watadhani ni kweli, tuliokuwepo enzi zile za 90s maandamano na mikutano ya CUF ilikuwa ikitangazwa misikitini, na maandamano mengi yalikuwa yakianza humo hasa baada ya swala ya Ijumaa, mashehe, Bakwata na taasisi zingine za kiislamu zilikuwa hazijifichi kwa hili, lakini on contrary mbali ya Chadema kusemwa cha Kikristo hatuokuona support kutoka kwenye madhehebu hayo, rejea kauli ya Pengo kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu.

mkuu nikusahihishe sio Pengo alisema hivyo.Ni askofu Kilaini alisema hivyo.
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0

Kuna jambo limekuwa linanitatiza kila siku. Ilikuwaje Chadema iliweza kuipiku CUF katika kukubalika huku Bara? Sote twajua baada ya NCCR kupotea CUF ndiyo ilikuwa moto wa kuotea mbali katika kuihenyesha CCM na hiii ilionekana katika uchaguzi wa 2000 na 2005 hasa katika kura ya urais.

Baada ya 2005 CUF ilianza kupotea pole pole. Bila shaka ni kwa sababu CDM waliweza kuipiku CUF katika hoja ya ufisadi na hii inashangaza -- kwani CUF hawakuiona hoja hiyo na kuifanya yao? Kitu gani kiliwazuia?

Umaarufu wa Chadema ulianzia September 2007 kule Mwembeyanga wakati Dr Slaa aliposimama jukwaani na kuitaja ile orodha ya aibu ya watu 11 ikiongozwa na JK mwenyewe. Hilo lilikuwa ni bonge la bao la kisigino dhidi ya CUF, na tangu hapo chama hicho hakikusimama tena sawasawa – kilianza kuchechemea.

Na uzuri ni kwamba orodha ile ilikuwa ya ukweli mtupu, na ndiyo yakaja mambo ya EPA, Meremeta, Deep Green na mengineyo mengi isipokuwa Richmond ambalo lilianzia katikati 2006.

Ingekuwa ni Profesa Lipumba ndiyo alipanda jukwaani na kutaja orodha kama hiyo, hadi leo hii Chadema ingebakia kama zamani, chama cha Wachagga.

Hii inaonyesha Dr Slaa ana uthubutu na ujasiri wa kuweza kufanya maamuzi magumu na mazito, sifa ambayo Profesa Lipumba hana, ingawa yeye anaweza kuwa anamzidi DR Slaa katika kuyaelewa matatizo ya nchi hii na kuyaelezea kwa ufasaha, lakini si katika ujasiri wa kuchukuwa maamuzi mazito.

______________-

Hayo ni kweli kabisa, inashangaza kwa nini CUF hawakuiona hoja ya ufisadi na kuwawahi CDM. Ni kweli pia hoja ya ufisadi imewaumiza sana CCM, hadi leo iko hoi kabisa kinachowasaidia ni ile nguvu ya dola waliyo nayo.

Lakini nadhani pia suala la mgogoro kule Zanzibar liliwachukuia muda mwingi sana CUF kulishughulikia katika kufikia miafaka mara 2. Hivyo nguvu zao zote zilikuwa kule -- hata viongozi wakuu wa CUF huku Bara walipeleka nguvu zao kule. Vinginevyo sikuona sababu ya Pro Lipumba kutoibaini hoja ya ufisadi kama mtaji mkubwa wa siasa. It's too late.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,014
2,000
CUF hawajawahi kuwa na mvuto bara. Walifanya makosa kutokifanya chama chao cha kitaifa. Walijikita zaidi kizanzibari na hawakuweka mipngo mikakati kupenya bara. Watu wa bara ni rahisi kuwapenya lakini sio kwa siasa zile za kizanzibari.
 
Kuna glaring 'irony' katika hili. Tukumbuke kwamba wakati vyama vinaanzishwa 1993, ni CUF pekee, katika vyama vya upinzani, ndiyo kilikuwa na sura kubwa ya kitaifa iliyosistizwa katika Sheria ya Vyama Vya Siasa ya mwaka 1992. Hiiilitokana na ukweli kwamba CUF ilikuwa ni muungano wa vyama viwili vikuu kutoka kila upande wa Muungano wetu -- yaani KAMAHURU ya Shaaban Mloo na Chama cha Wananchi (CWT) cha James mapalala.

Lakini ajabau ni kwamba pamoja na sura hii kibwa ya kitaifa, CUF ilizidiwa sana na NCCR huku Bara katika uchaguzi wa kwanza wa 1995. Kwa hiyo mambo yalianza kwenda kombo tangu wakati ule, ingawa kama usemavyo kupotea kwa NCCR kulipandisha chati CUF katika uchaguzi wa 2000 na 2005.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,014
2,000
Lakini ajabau ni kwamba pamoja na sura hii kibwa ya kitaifa, CUF ilizidiwa sana na NCCR huku Bara katika uchaguzi wa kwanza wa 1995. Kwa hiyo mambo yalianza kwenda kombo tangu wakati ule, ingawa kama usemavyo kupotea kwa NCCR kulipandisha chati CUF katika uchaguzi wa 2000 na 2005.

Hii ni mfano wa waziwazi kuwa siasa hazitabiriki.
 
magnificent

Senior Member
Jun 25, 2011
110
0
Nani akajiunge CUF wkt ukienda kwenye mkutano wa CUF kila mtu mume anakibaragashia na kila mtu mke anaushungi! km nasema uongo tafuta picha yoyote ya mkutano wa CUF uone. maana yake ni chama cha kidini. watu wanaogopa wasije kuitwa makafiri baadae. Bora chadema, chama cha wote.
 
Straight

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
346
0
Alijua ni ya wakatoliki wenzake...ndio aliwaogopa CUF zaidi..kwakuwa wanaonglea equality and justice..

duh... Kumbe ccm ni ya wakatolik... Muasis mkatolik, waendesha nchi wakatolik, ucsahau kuna sanam la mwislam pale halina maamuz hata chembe, ndo maana wana2nyima mahakama ya Kadhi... Baloz wa Vatcan ameaga sanam letu, kamshukuru sana kwa kuzuia mahakama ya kadhi na kujiunga OIC... CCM Bana na wakatolik...
 
onchoseciasis

Member
Sep 24, 2011
33
0
Umetumia kigezo gani kusema cuf ilikuwa juu ya chadema? cuf haijawahi kukubalika na watu wengi Tz bara. Ukichukua mfano wa wabunge hebu nikumbushe (labda nimesahau) kama ilishapata walau wabunge kumi huku bara
kwa chaguzi za 1995, 2000 na 2005 cuf haijawahi pata mbunge bara, ila baadaa kupiga kampeni za kisayansi 2010; imepata wabunge 2 ie mtwara na kilwa
 
Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
874
0
Unajua Gagnija kama kitu kikisemwa na wewe huchukui initiative yeyote kuwa mbali nacho hata kama ni cha uongo watu watadhani ni kweli, tuliokuwepo enzi zile za 90s maandamano na mikutano ya CUF ilikuwa ikitangazwa misikitini, na maandamano mengi yalikuwa yakianza humo hasa baada ya swala ya Ijumaa, mashehe, Bakwata na taasisi zingine za kiislamu zilikuwa hazijifichi kwa hili, lakini on contrary mbali ya Chadema kusemwa cha Kikristo hatuokuona support kutoka kwenye madhehebu hayo, rejea kauli ya Pengo kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu.

mkuu, si PENGO ni YUKE WA KAGERA SAIZI.. Nani?!! Ok ni METHODIUS KILAINI
 
Maengo

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
280
0
Hizi zingine tulizojenga tunaziendeshaje?

Unafurahia kupendelewa na serikali..bado unaweza kujiita mtetezi wa haki?

Serikali imewapendelea wakristo kwa kuwarudishia shule zao na kuwalipia hela za umma through MoU...huo utabaki ni ubaguzi, uwizi, ufisadi uliofanywa na serikali hata kama wakristo mtautetea..

Tutashinda na mtatema tu iko siku..

Tatizo lenu mnatumia muda wenu mwingi kujadili ukristo baadala ya kujadili maendeleo! Wakristo hutumia muda mwingi kupanga maendeleo pamoja na mbinu za kupambana na adui yao mkuu shetani! Adui wa mkristo wala si muislam hata kidogo! Ndugu zangu waislam huwa wanakwepa challenges ndo maana huwa wanataka kila mtu akubaliane nao! Hamuwezi mkawa na mawazo sawa wote halafu mkapata maendeleo, ni lazma mtofautiane kwanza! Ni fedheha sana kupoteza muda na nguvu yako kumjadili mtu ambaye hata hana time na wewe!
 
TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
0
Sababu:
1.Kuungana kwa CCM na Cuf kumepunguza mvuto na nguvu ya Cuf
2.Magwanda kumteua Slaa kugombea urais kumeongezea mvuto wa chama
3.Magwanda ku-take advantage ya ugumu wa maisha kuishambulia CCM
4.Ukali wa spika Makinda umesaidia kuipa Magwanda public sympathy
5.Migogoro ndani ya CCM nayo imeipa sababu magwanda kupiga kelele
6.Fedha na ufadhili wa CDU umeipa nguvu sana Magwanda kwa kufanya maandamano na makusnyiko
7.Baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa kutoa siri za serikali kwa Magwanda

Ndugu Atiwm52;2565548,
Tunashukuru kwa kutupa hizi sababu lakini naona hujaelewa vizuri mjadala wetu. Ukweli ni kwamba hizo sababu ulizotaja zimechangia kwa kiasi kikubwa kuibeba CDM hadi leo. Swali la msingi ni kwamba kwa nini hizo sababu ziliibeba CDM badala ya CUF? Mfano sababu namba 7 uliyoitoa kwamba nanukuu "Baadhi ya maofisa usalama wa taifa kutoa siri za serikali kwa Magwanda". Swali la msingi kwenye hii hoja yako ni kwanini hao maofisa usalama wa taifa watoe siri za serikali kwa Magwanda? Kwa nini wasizipeleke CUF? Tuendelee kujadiliana..
 
TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
0
kwa chaguzi za 1995, 2000 na 2005 cuf haijawahi pata mbunge bara, ila baadaa kupiga kampeni za kisayansi 2010; imepata wabunge 2 ie mtwara na kilwa

Hapana hili sikubaliani nalo. Kumbuka kina Frank Magoba (Kigamboni), Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) nk..
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,217
2,000
CUF hawajawahi kuwa na mvuto bara. Walifanya makosa kutokifanya chama chao cha kitaifa. Walijikita zaidi kizanzibari na hawakuweka mipngo mikakati kupenya bara. Watu wa bara ni rahisi kuwapenya lakini sio kwa siasa zile za kizanzibari.

mkuu baada ya vyama vingi cuf ndiyo iliyokuwa na nguvu huku bara kipindi ikiwa na akina james mapalala
 
JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
625
500
Tuseme ukweli tu ingawa propaganda za ccm zilichangia kwa kiasi kikubwa lkn on the other side of the coin cuf walijimaliza wenyewe kwa viongozi wao kuukumbatia udini japo wao walikuwa waki-claim haupo.
Mikutano yao wanakaa kama msikitini wamama kivyao wababa kivyao, baghalashia na hijab nyingi tu,kusoma dua na mambo kama hayo,
na ndo maana cuf ilikuwa ikielekea kupata mass-support maeneo ya coastal areas kwenye chimbuko la dini hiyo,
na ndo mana hata dar cuf inakubalika zaidi kwenye maeneo ambayo kuna watu wengi wa dini iyo kama manzese, buguruni,temeke.
Ila kwa sasa mtatiro anajaribu kukileta chama kwenye mstari.

Tofati ya cuf na cdm ni kwamba cuf waliikumbatia propaganda ya ccm ya udini wkt cdm wamekuwa wakijikung'uta nayo kwa nguvu zote
 
mbaba

Member
Jun 18, 2011
43
70
kwa hili me nina wasisi na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani waliopita,Mrema,Lipumba wale mashababi wengine kama Tabwe.vyama vinakua vya 'periodically' maybe janja ya ccm
 
Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,316
2,000
Tatizo ni Hamad Rashid
huyu alikuwa akimpenyezea waziri mkuu na mawaziri wengine maswali kabla ya siku husika
HR anafanya kazi kwa ajili ya CCM
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom