Ilikuwaje Askari Polisi akawa Mwandishi wa Gazeti la Uhuru?

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
5,951
2,000
Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha.

Swali langu ni hili, ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM, haya mambo yanaruhusiwa kikatiba?

View attachment 2079854
Mademu wazuri kinoma
 

makedonia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
2,733
2,000
Ni kawaida sana, wapo wengi sana kwenye vyombo vya habari. Unamkumbuka aliyekuwa anatangaza kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Semunyu Selemani ni Kapteni wa Jeshi la Wananchi. The same jamaa anaitwa Hope Dagaa alikuwa Star TV pia ni Kapteni wa Jeshi. Hata huyo Musiba alikuwa mwanajeshi pale Ngome
Huyu Semunyu selemani pia ni promota wa ndondi...alipromoti pambano la Dulla mbabena KIDUKU...pia pambano la yule Mkongo na Kindunda....kama sijakosea.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
19,571
2,000
Hakuna lolote sababu upo kwenye nchi ya amani ambayo wengi hawana na unapata na muda wa kuingia JF unaandika uharo na point sababu ya wenzako wanaoteseka kwa mishahara midogo tu kwaajil yako
Sehemu kubwa ya dunia ina amani, ni sehemu chache sana zilizobaki zisizo na amani.
 

Rwebo

JF-Expert Member
Oct 17, 2015
515
1,000
Natamani kamanda Siro ajibu swali hili. Na asipo lijibu itakuwa ni fedheha sana kwa jeshi la police. Pia aambatanishe na sheria make hii ni kinyume na civil servant act na regulations zake
Mambo ya usalama yatakuumiza kichwa bure ndugu yangu. Uliwahi kusikia budget yake ikipitishwa bungeni? Je Uliwahi kusikia CAG akitoka report yake kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom