Ilikuwaje Askari Polisi akawa Mwandishi wa Gazeti la Uhuru?

Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha .

Swali langu ni hili , ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM , haya mambo yanaruhusiwa kikatiba ?

View attachment 2079854
Hatuendi na katiba Tanzania ni nchi ya chama kimoja, polisi huwapigia saluti viongozi wa CCM.
 
Mkuu, taarifa zote kuhusu huyo marehemu mwandishi wa habari, mbona zimetolewa na kuwekwa wazi na viongozi wake baada ya kifo?

Kawaida "askari" wa majeshi yote ni watumushi wa serikali(umma) na huweza kushikizwa kwenye idara yoyote ya serikali bila shida.

Swali la msingi hapa ni: kwa nini iwe kwenye departmemt ya Sisiem, wakati sheria zinapiga marufuku askari yeyote kufanya kazi za chama, ama kujiunga na chama chochote?
Hawa wapo hata kwenye media houses nyingine mkuu
 
unafikiri atakubali tu ndio, imeshakuwa exposed lazima atafute pakutokea..
Point yako inaweza kuwa sawa, lakini kumbuka kuwa "ngome" kuna wafanyakazi wengi sana maraia walioshikizwa na Wizara ya ulinzi kufanyia kazi pale kutokana na mahitaji ya jeshi.

Watumishi hao wasio wanajeshi huitwa: "watumishi wa umma", hufanyia ofisi mbali mbali pale, zikiwemo za fedha, madereva, mafundi, waandishi nk nk.

Pia kumbuka, mwanajeshi akistaafu anaweza kfanya kazi yoyote ama kujiunga na chama chochote, sheria inakuwa haimbani tena.

Sasa sielewi kama jamaa alikanusha kwa ghilba ama vipi, lakini kwa kulinda maslahi gani na ya nani!
 
So alikuwa anakula mishahara miwili maana lazima Uhuru walikuwa wanamlipa na jeshi la polisi analipwa pia.
 
Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha .

Swali langu ni hili , ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM , haya mambo yanaruhusiwa kikatiba ?

View attachment 2079854
Intelejensia za nchi
 
Hadi huko bar Kuna wanawake ma barmaid lakini ni polisi wako sehem nyingi sana kwenye ulevi ndo sehem wanakusanya taarifa nyingi.
Wengine wamejiunga kwenye makundi ya kijambazi kabisa na wanapiga matukio kadhaa ikibidi huku majambazi wakiamini ni mwenzao, mwsho mnakamatwa wote alaf yeye inasemekana katoroka

Sasa mbona kwenye kesi nyingi kila siku tunasikia upelelezi hujakamilika
 
Nyie endeleeni kuchezea keyboard mchana, kisha usiku mkalale na familia zenu mkijamba mtakavyo.

Kitu hamjui ni kwamba kuna watu wanawajibika usiku na mchana, kuhakikisha,nchi iko salama 24×7×12.

State intelligence ni mfumo mpana. Nyinyi bushlawyers endelezeni uzandiki wenu ila muelewe kwamba mnapoambiwa serikali iko macho, ni kweli iko...MACHO
FB_IMG_1638365723895.jpg
 
Back
Top Bottom