Ilikuwaje Askari Polisi akawa Mwandishi wa Gazeti la Uhuru?

Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha.

Swali langu ni hili, ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM, haya mambo yanaruhusiwa kikatiba?

View attachment 2079854
Detective cop
 
Hili si suala geni (undercover activities), limekuwepo kwa miaka mingi Tanzania tangu enzi za awamu ya kwanza.

Mara nyingi mgawanyo wa majukumu huanzia JKT ambapo mtu aweza kuwa na namba hadi anakufa.

CCP Moshi pia huangalia nani anafaa kwenda JWTZ, kule kwa raisi kuwa msaidizi na kadhalika.

Mimi nawafahamu baadhi ya wazee walikwenda vitani Uganda lakini waliporudi wengi waligawanyika na wengine walikwenda sehemu nyeti sana.

Kuna baadhi ya wazee kama Makamba Kinana JK na co walipigana vita ile na sasa wanatabasamu tu wakituangalia huku JF tunavyojimwambafwai.

Hivyo mtu aweza kuwa mwalimu, nesi, daktari, banker, bank teller, clearing & forwading agent, afisa forodha, luggage hundler pale uwanja wa JNIA, mwanasheria, Afisa TAKUKURU, afisa TRA mwandishi wa habari na kadhalika lakini akawa polisi, MI au JWTZ.

Usisahau mkuu, namba ya kule (unique number) iwe CCP Moshi, au pale Kurasini kwa wale wa form six na UDSM, JWTZ, Mbweni na idara zingine za intelijensia ni namba ya kutumia sehemu zingine kwa kazi maalum.

Yawezekana marehemu alikuwa akisaidia usalama kwa mkuu wa mkoa katika msafara au akitafuta habari ingine kuhusu wana msafara au akihakikisha habari zinaripotiwa kama inavyotakiwa.

Ila kiujumla vitendo hivi hufanywa kwa kiwango kikubwa na serikali isojiamini kutokana na matendo yake yasoeleweka.
 
Mambo ya the american haya
Wamarekani hawafanyi mambo yao hivi ndani ya nchi. FBI Ili kumpachika undercover mahali lazima kuwepo mtu mahususi wanayemchunguza na kwa tuhuma mahususi zinazochunguzwa.
 
HAPANA polisi hawana kitngo hicho...ninacho kijua mimi ni kuwa kazi za polisi ni kazi ya kimdebwedo inayomuwezesha askari anae jiongeza kupata muda wa kufanya kazi nyingine kwasababu muda wanao wa kutosha...wanafanya kazi siku 6...masaa 9 tu...hapo ukijiongeza unaweza kufanya kazi nyingine nje ya uaskari...nawajua maaskari wengi ambao ni watangazaji kabisa kwenye vyombo vikubwa vya habari...kazi maalum ni ya watu maalum jamani na sio maaskari wa jeshi la polisi
Yani watu wanafanya kazi ya kuweka maisha yao rehani wewe unasema mdebwedo.Wewe fala sana!!
 
Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha.

Swali langu ni hili, ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM, haya mambo yanaruhusiwa kikatiba?

View attachment 2079854
Sasa bila makamanda kujichanganya sehemu mbalimbali taarifa za Kiintelijinsia zitapatikana? Si afadhali huyo alikuwa mwandishi, wapo wauza karanga mitaani, shoe shiners, wapiga debe, kuna machizi wanaokota majalalani, na kwa jinsi walivyo na mazingira ya kazi zao sio rahisi kuwatambua,sasa wewe jichanganye ropoka ropoka mambo usiyoyajua utashtukia watu wamekuja kukunyakua kwenda kutoa ushirikiano.
 
Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha.

Swali langu ni hili, ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM, haya mambo yanaruhusiwa kikatiba?

View attachment 2079854
Askari kanzu
 
Wamarekani hawafanyi mambo yao hivi ndani ya nchi. FBI Ili kumpachika undercover mahali lazima kuwepo mtu mahususi wanayemchunguza na kwa tuhuma mahususi zinazochunguzwa.
Hivi huwa mnadanganywa na nani? Nani alikwambia us hawana undercover ?

Kwa taarifa yako idara za marekani zimejaa.majasusi na hii ni kwa faida ya marekani wanapachikwa popote ambapo selikal itahisi pana tija

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom