Ilikuwaje Askari Polisi akawa Mwandishi wa Gazeti la Uhuru?

Kama alikuwa mtu wa kazi maalum, kulikuwa na sababu gani ya kufichua kazi yake baada ya kufa? Ufala mwingine.

Hivi informer anaweza wekwa taasisi/sehemu yoyote ile?
informer sio tu anaweza kuwekwa taasisi au sehemu yeyote ile hata boda boda ni informers,hajaajiliwa serikalini lakini kuna benefits anapata
 
Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha.

Swali langu ni hili, ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM, haya mambo yanaruhusiwa kikatiba?

View attachment 2079854
Ndiyo uelewe kuwa polisi wakisema intelijensia yao imewafanya waamue jambo fulani, jua wana data. Kwa bahati mbaya huyu alikuwa kwenye magazeti ya CCM lakini usishangae kuwa kuna watangazaji na waandishi ambao wako kwnye vyombo binafsi laikini ni askari; ninapenda sana muundo huo. Kwa nchi kubwa na yenye raslimali nyingi kama Tanzania ni lazima mfumo wa aina hii uwepo na uwe imara sana.
 
Hivi huwa mnadanganywa na nani? Nani alikwambia us hawana undercover ?

Kwa taarifa yako idara za marekani zimejaa.majasusi na hii ni kwa faida ya marekani wanapachikwa popote ambapo selikal itahisi pana tija

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
Marekani haiendeshwi kiholela hivyo, sheria zao haziruhusu kupachika majasusi kila mahali kwenye maisha binafsi ya watu au taasisi zao. FBI kupachika undercover agents wao mahali wanahitaji kuwa na kosa maalum wanalolichunguza na lazima wawe na warrant ya mahakama kufanya hivyo, vinginevyo huwa wanatumia "informers" tu ambao ni watu wenye makosa nao lakini wanawachoma wenzao ili wapunguziwe adhabu au wapewe msamaha kabisa.

Trump aliwasumbua sana FBI kiasi cha kuundwa kamati maalum ya seneti baada ya kugundulika kuna undercover agents walikuwa wanafuatilia kampeni zake za mwaka 2016 na agents wenyewe walikuwa wamepewa kibali na mahakama ya FISA.

Majasusi wa CIA ndio wamepachikwa wengi nje ya nchi kwenye nchi nyingine kwa sababu huko sheria za Marekani hazifiki na ni kwa maslahi ya taifa lao bila kujali kama haki za hao watu zinazingatiwa au kupuuzwa.
 
Ndiyo uelewe kuwa polisi wakisema intelijensia yao imewafanya waamue jambo fulani, jua wana data. Kwa bahati mbaya huyu alikuwa kwenye magazeti ya CCM lakini usishangae kuwa kuna watangazaji na waandishi ambao wako kwnye vyombo binafsi laikini ni askari; ninapenda sana muundo huo. Kwa nchi kubwa na yenye raslimali nyingi kama Tanzania ni lazima mfumo wa aina hii uwepo na uwe imara sana.
Huo ni mfumo wa nchi za kijamaa za chama kimoja, ulipendelewa zaidi na wasovieti na nchi nyingi zilizoingia katika siasa za ujamaa zikauchukua na kuendelea nao hadi leo.
 
Ni kawaida sana, wapo wengi sana kwenye vyombo vya habari. Unamkumbuka aliyekuwa anatangaza kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Semunyu Selemani ni Kapteni wa Jeshi la Wananchi. The same jamaa anaitwa Hope Dagaa alikuwa Star TV pia ni Kapteni wa Jeshi. Hata huyo Musiba alikuwa mwanajeshi pale Ngome
Wengi ni vijana wadogo hawaelewi kwa nini Nyerere aliweka balozi wa nyumba 10 na hii ya askali wa vyombo vya ulinzi ni sehemu ya hiyo ya Nyerere toka miaka ile.

Mfano miaka ile ya mabasi ya Scandinavia Express kulikuwa na askali kadhaa wakipiga gear kwenda sehemu tofauti na unaweza kukuta mwingine ana hips ya upande mmoja akiwa safarini.

Hips = mguu wa kuku!.
 
Tuambie wewe mzee kwa nini Nyerere aliweka balozi wa nyumba 10?
 
Wamarekani hawafanyi mambo yao hivi ndani ya nchi. FBI Ili kumpachika undercover mahali lazima kuwepo mtu mahususi wanayemchunguza na kwa tuhuma mahususi zinazochunguzwa.
Nimeongelea series mkuu
 
Kwa akili yako unaweza kustaafu halafu ukaenda depo?
Hujamuelewa swali lake Mkuu, yaani ametaka kufahamu kwamba hizo kazi za uandishi wa habari alikuwa anazifanya akiwa katika utumishi ndani ya Jeshi la Polisi au alikuwa anafanya baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi?
 
Akiwa ndani ya utumishi wa jeshi
 
Zipo taarifa kwamba mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefariki kwenye ajali iliyotokea Mwanza na kuua watu zaidi ya 14 , ambaye alikuwa anafanyia kazi zake kwenye gazeti la CCM alikuwa Askari Polisi na Amezikwa kwa heshima zote za Jeshi hilo mkoani Arusha.

Swali langu ni hili, ilikuwaje Askari huyu kuwa Mwandishi wa chombo cha CCM, haya mambo yanaruhusiwa kikatiba?

View attachment 2079854
KWani ni zambi?
 
Huo ni mfumo wa nchi za kijamaa za chama kimoja, ulipendelewa zaidi na wasovieti na nchi nyingi zilizoingia katika siasa za ujamaa zikauchukua na kuendelea nao hadi leo.
Siyo kweli kabisa; hata marekani wanautumia sana, na tena marekani wanautumia zaidi ya uandishi wa habari tu. Kuna magents wengi sana wa FBI wana kazi nyingine mitaani. Kama unajua jinsi magaidi wanavyoshikwa kabla hawajatekeleza plani zao za ugaidi marekani, ni wazi utakuwa unajua pia kuwa FBI ina watu wake huko mitaani. Kwa mfano wale wasomali waliokuwa wanakwenda kuungana na ISIS waliokamwata siku ya mwisho kabisa ya plani yano ni kwa sababu walikuwa wakifanya plani hizo wakiwa na FBI agent mmja ndani yao bila wao kujua; huyo hakuwa mwandishi wa habari.
 
kuna msanii mmoja wa bongofleva niligoma kumpa nyaraka fulani.... nikamtafuta Rpc wa huo mkoa akasema usithubutu kumpatia hiyo taarifa,baadae nikapigiwa simu na kamishina wa intelejensia polisi tuliyekuwa tunafamiana binafsi kwenye kazi kuwa ni mpe tu hizo nyaraka na taarifa kwani ni askari kanzu pia yeye ndio kamtuma...
Miaka nane sasa imepita yule kamishina ni some body fulani mkubwaaa kwa sasa, yule mbongo fleva hahit ila show za kitaifa ndio namuona ona mara mojamoja
Tangu siku hiyo nikajua kwaninj polisi wanasema wanataarifa za intelejensia...Wapo vizuri
 
Back
Top Bottom