Ilikuwa vp hata ukawa mpenzi wa Arsenal, Man U, Chelsea or Liverpool?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilikuwa vp hata ukawa mpenzi wa Arsenal, Man U, Chelsea or Liverpool?!

Discussion in 'Sports' started by NasDaz, Oct 16, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Mimi ni shabiki wa Arsenal!

  Ilikuwa ni miaka kadhaa iliyopita wakati nikiwa kijana mdogo ambae nahisi hata kidato cha kwanza nilikuwa sijaanza! Nakiri, wakati huo sikuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua ama kudadisi mambo critically, hususani yale ya magazetini!

  Hata hivyo, jambo ambalo sina shaka nalo ni kwamba nilikuwa ni bonge la shabiki la Dar es salaam Young Africans a.k.a YANGA! Nilikuwa ***** sana enzi hizo! Nilikuwa nashindwa hata kula kisa tu eti Yanga imefungwa! Acha tu baadhi ya Masheikh waseme kwamba kabumbu nalo ni haramu!
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  Basi bana! Siku moja nikiwa kwenye viunga wa Uwanja wa Taifa (siku hizi wa Uhuru) niliokota kipande cha gazeti! Hata hivyo, bado sifahamu kilikuwa ni kipande cha gazeti gani ingawaje nahisi ilikuwa ni ama gazeti la Majira au Uhuru. Kwenye kipande hicho cha gazeti kulikuwa na habari eti Uingereza kuna timu inayoitwa Arsenal ambayo ni marafiki wakubwa wa timu ya Yanga na kwamba Yanga wamekuwa wakipata misaada mbalimbali toka timu hiyo ya kwa Malkia!

  Nakiri kwamba, hiyo ilikuwa ndio siku yangu ya kwanza kusikia kuwapo kwa timu ya Arsenal kwani kabla ya hapo nilikuwa naifahamu Man U na Liverpool peke yake! Mwandishi wa habari hiyo aliendelea kudai kwamba, kutokana na urafiki huo wa karibu kati ya Arsenal na Yanga, timu hiyo ya Uingereza ilikuwa na mpango wa kuja Dar kucheza mechi za kirafiki na wana wa Jangwani!
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Dah! Mzee kichwakichwa nikajikuta nikianza kuipenda Arsenal!

  Na hata pale Ligi Kuu ya Uingereza ilipoanza kuoneshwa kupitia ITV katikati ya 1990's nilikuwa tayari nimeshaoza kwa Arsenal!
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Hivi sasa, nikiwa mtu mzima mwenye uwezo wa ku-reason mambo ndipo naanza kushituka na kujiuliza ukweli wa habari ile (kwamba Arsenal ma Yanga ni marafiki)! Nahisi, ilikuwa ni habari ambayo iliandikwa siku ya Wajinga (April 01) ambayo nami niliimeza kama ilivyokuwa na kuathiri kabisa maisha yangu! [/FONT]

  [FONT=&quot]Je, mwenzangu wewe ilikuwaje hata ukawa mpenzi wa ama Arsenal, Man U, Liverpool , Chelsea au timu yoyote ile ya Ulaya? [/FONT]
   
 2. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Du! hadithi nzuri, kweli kila jambo lina mwanzo wake uwe mzuri uwe mbaya ndio mwanzo wake. Mimi ni mpenzi wa Spurs, ingawa niliwahi kuisikia timu hii miaka ya mwanzo ya 70 wakati huo kuna timu ya Morogoro ilikuwa ikijiita hivi sikuwa mpenzi wake.

  Nilianzaje, hadithi inafanana na hadithi ya kipofu aliyeona punda.

  Mwanzoni mwa miaka ya 90 nilipata bahati ya kwenda Uingereza kwa ajili ya mafunzo fulani, ndipo siku moja nikapata bahati ya kuona mechi yao moja wakicheza na Lutton Town. Ilikuwa mechi ya FA, basi toka hapo ndio mapenzi yangu kwa timu hii yakaanza.

  Inawezekana ni uwe ushamba wa kuwaona kina Lineker, Nahim na wengine ilikuwa kama muujiza hasa miaka hiyo.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  boyfriend.....we acha tu
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  My ex- boyfriend alinifanya niipende sana arsenal hadi jezi navaa cha kushangaza tuliachana na am about to get married and my husband to be imebidi aipende arsenal hamna mfano,nadhani hata watoto wetu wataipenda arsenal
   
 5. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Amekufanya uwe mpenzi wa timu gani?
   
 6. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2010
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mie hata sijui ila kwa kiasi fulani wale majirani zangu wamechangia kwa kiasi kikubwa, maana jamaa na Man U ulikuwa huwaambii kitu na ni familia nzima.

  Mbaya zaidi jamaa walikuwa na Dstv maana baba mwenye nyumba ni mpenzi mkubwa sana wa kabumbu, hivyo kuanzia premier mpaka kombe la dunia najimix kwa jirani, juu ya hayo yote ndio kipindi ambacho Man U walikuwa top in the game.
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  Arsenal
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hahaahah mie mwenzenu nilipopokea ekaristi takatifu (Komunio ya kwanza kwa wakatoliki) mwaka 1984, kaka yangu alinipeleka kuangalia picha siku hiyo, wakati ule ilikuwa ikiitwa sinema hahaah.

  Sasa kabla ya picha yenyewe walikuwa wanaonesha trailer, trailer hii ilikuwa ni mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 1982 kati ya Italy na West Germany wakati ule. Kwa kweli mechi likuwa nzuri sana na Italy walishinda ile mechi, nayakumbuka majina mawili, golikipa wa Italy Dino zoff na captain wa Ujerumani magharibi wakat ule Karl Heinz rummenige.

  Tokea hapo nikawapenda sana hawa wa Italiano na klabu niliyoipenda na NINAYOIPENDA sana pale Italy ni kibibi kizee cha TORINO yaani JUVENTUS. Miaka ya mwanzo ya 1990 hii klabu ilitesa mno na nilliishuhudia LIVE wakiichapa AJAX Amsterdam kule Italy kwenye fainali ya UEFA 1996. Majina makubwa wakati ule ya JUVE walikuwepo akinia Gianluca Vialli, Babu Fabrizio Ravaneli, Kipa gianluca pagliuca. Huyu Vialli nlikuwa namzimkia sana tuu.

  Wakati ule miaka ya mwisho ya 80 na mwanzo ya tisini hakukuwa na luninga, baba yangu alipenda sana kununua gazeti la Africa Now kama mnalikumbuka, Newsweek nk, mle ndani unakuta pcha za timu mbali mbali za ulaya, africa nk.

  KISA CHA KUPENDA NA KUIZIMIKIA CHELSEA NI baada ya JUVE kuchukua Ubingwa wa ulaya, wachezaji hawa wakauzwa, huyu VIALLI alienda CHELSEA wakati ule ikifundishwa na Glen Hoddle, na Ravanelli akaenda Middlesbrough. Chelsea wakamnunua Di Matteo na Zolla, hapo kwa kweli ukawa ushabiki wangu kwa chelsea ukabobea. Its almost 15 yrs niko pale DARAJANI wadau na timu ndo hiyo imekuwa tishio, na Bado JUVE ipo kwenye damu ile mbaya!
   
 9. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimeanza kushabikia Manchester United nikiwa na miaka 10, na mechi yakwanza kuiona iliyonifanya ni washabikie ilikuwa dhidi ya Nottingham Forest.
   
 10. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mimi nilianza kuwa the gunners ki-bahati, wakati nikiwa junior kwenye miaka ya 84-87 nilikuwa mpenzi wa Ajax Amsterdam kwa vile nilikuwa naishi Amsterdam lakini kule UK nilikuwa ni Liverpool lakini niliamua kuachana nao rasmi kwenye mechi ya kufunga msimu 88-89, ilikuwa ni mechi baina ya Liverpool na Arsenal pale Anfield, Arsenal walitufunga 2-0 na kunyakua ubingwa mwaka huo, na kwa kweli kilichonivutia kwenye timu ya Arsenal enzi hizo ni mchezaji mweusi David Rocastle (R.I.P)

  Na pale tulipomsajili Wright miaka ya 91 ndio nikaacha kabisa hata kushabikia hata Ajax mimi nikawa ni Arsenal tu labda na Yanga kule nyumbani, na tulipohamia London toka Amsterdam ndipo nilipoamua kuwa na kadi kabisaaa!!!! GUNNER FOR LIFE!!!!!!
   
 11. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hii ilikuwa premier au FA?, najaribu kuvuta kumbukumbu hii itakuwa miaka gani. Maana tangu Nottingham Forest waiage Premier ni kitambo!
   
 12. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ilikuwa ni 1988 katika Mji mkuu wa Catalan(Barcelona),kulifanyika michezo ya Olympic,wakati huo mjomba wangu alikuwa ni mining engineer ktk nchi jirani hivyo nilrudi tena ktk nchi ile kuitikia wito wa mjomba.

  Wale vijana,wakiongozwa na Josep"Pep"Guadiola,walikuwa hatari mno, Luis Enrique Martinez,Txiki Begiristain n.k,walikuwa wanapepea.Nikaupenda sana mji ule sababu mjomba alinieleza mengi kuhusu historia ya Catalonia na uovu wa Francisco Franco,na kwamba wale vijana ambao nilikuwa nawashabikia,ukiondoa Martinez,kwa wakati huo walikuwa wakichezea FC Barcelona. They finaly won the Olympic Gold. Na kuanzia 1988 mimi ni Shabiki wa FC Barcelona.

  In 1991 Paul Gascoigne "GAZZA" Alipiga free kick maridhawa na ambayo inabakia kwa muda mrefu kichwani mwangu, ilikuwa ni Spurs against Arsenal, nilishangilia sana goli lile, kulikuwa na student mmoja toka london alikuja Field kule kwetu, akanipenda na kwa vile mimi na yeye tulikuwa mara kwa mara tunacheza squash akaniuliza kama kushangilia kule maana yake mimi napenda Spurs, nikajibu ndiyo. Aliporudi kwao akamwambia mama yake kuwa hakutegemea kukuta shabiki wa Spurs Tanzania, basi mama yake akanitumia zawadi ya mpira toka London so nikawa nami naipenda Spurs kwa sababu ya zawadi ile ya mpira. Lakini "Barca 4 Life".
   
 13. g

  gutierez JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  mbona nottingham forest 1998-1999 walikuwepo premier na wakashuka msimu huo wakati ole gunner solsjaer anaingia super sub anawapiga bao 4 kwao city ground stadium
   
 14. g

  gutierez JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  kweli wewe kitambo unafuatilia soka,huyu alikuwa na binamu yake anaitwa Craig Rocastle alicheza chelsea miaka ya 2003 alikuwa kama chipukizi sio 1st eleven sasa hivi yupo Marekani anacheza MLS
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  No comments!
   
 16. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  David Beckham:
  Timu ya kwanza duniani kuifahamu ilikuwa ni Manchester United kupitia katika gazeti la Mfanyakazi na nilikuwa dogo kipindi hicho, nakumbuka miaka ya 88-89 kuna mchezaji ambaye nilikuwa nampenda sana ambaye ni David Beckham mara nyingi uso wake niliuonaga sana ktk gazeti lile la mfanyakazi kurasa za michezo.

  Simba
  Hii timu nilianza kuipenda tangu mwaka 1989 kipindi hicho kaka yangu alimaliza darasa la saba, muda mwingi alikuwa nyumbani, basi kuna kipindi kulikuwa na mechi ya Simba na Yanga ilichezwa ktk Uwanja wa Taifa(Uhuru stadium),kama sikosei Yanga ilishinda, alitoka kichwa chini redioni nikawa namcheka kutokana na kunung'unika kwa Simba kufungwa! Aliniuliza wewe timu gani? nilimjibu kwamba sina timu, ndipo akaanza kunielezea khs Simba na tokea hapo nikawa mshabiki wa Simba mpaka leo Simba damu!

  Arsenal
  Waliochangia kuipenda hii timu ni dada zangu wawili, walinieleza mengi kuhusu Arsenal kabla ya mechi ilikuwa fainali ya kombe la FA kati ya Arsenal na Manchester United mwaka 1999, Man U walishinda kwa mabao 2-0 mfungaji alikuwa Giggs katika dakika za majeruhi, kisa cha kuipenda Arsenal ni baadhi ya wachezaji kama kina Dennis Berkamp, Henry, Kuna kipa mmoja wa Arsenal mstaafu sikumbuki jina na hata Arsene Wenger mwenyewe ndiye aliyenifanya niipende Arsenal.

  Real Madrid
  Hii niliipenda sabu ya Zidane tu na soka iliyooneshwa kwa ujumla na timu hiyo kwenye mwaka ya 2000 hivi, Madrid kipindi hicho walicheza soka murua kabisa yaani habanduki mtu kwenye kochi kutokana na utamu wa soka lao! Zidane nilimpenda tangu Kombe la Dunia la mwaka 98 lililofanyika kwao Ufaransa, si kwamba nilimpenda baada ya Fainali,nilimpenda hata kabla ya Fainali yenyewe maana mpira wa Zidane ulikuwa mtamu hata kwa kuutazama tu!
   
 17. senator

  senator JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kama Kumbukumbu zangu zipo sawa Nchi ya Hispania kupitia mji wake wa Barcelona waliaanda Olympic mwaka 1992..nina matukio mengi sanaa ya mwaka huu especially huko Barceloooonaa!!
   
 18. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jaribu kuangalia kumbukumbu zako vema, Olympic 1988 ilifanyika Seoul, South Korea, hiyo ya Barcelona ni 1992.
   
 19. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu ilikuwa 1992 ndani ya Wembley kwenye fainali ya League Cup.
  **Forest walishuka daraja mara ya kwanza 1993, msimu uliofatia wakapanda tena ila mara ya mwisho kucheza kwenye EPL ilikuwa 98/99 msimu ambao tuliwachapa 8 - 1.
   
 20. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Beckham kaanza kuchezea United mwaka 1992.

  Mkuu ulimaanisha 1992 nini? Maana 1988 Summer Olympics zilikuwa Seoul, South Korea alafu Pep Guardiola ameanza kucheza Barca(first team) 1990 wakati Johan Cruyff kocha.
   
Loading...