Ilikuwa Umeme na sasa Bei ya mafuta (Petrol) Juu

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Bei ya mafunta yapanda laandika gazeti la leo 'The Guardian". Bei ya mafuta nchi nzima imepanda ghafla na sasa inauzwa kati ya Tshs. 1,600/= mpaka 1,800/= kwa lita moja ya mafuta aina ya petroli kutoka kwenye wastani wa Tshs. 1,400/= mwezi uliyopita. Kulikoni? Tatizo ni uwezo mdogo wa bandari katika kupakua mafuta? Je, Tatizo ni TRA? au tatizo ni wafanyabiashara katika kustage 'shortage' ya mafuta? Kumbuka walianza kwa kudai kwamba bandari inawachelewesha katika kupakua mafuta. Wengine walienda mbali na kudai kwamba 'meli ya mafuta ya IPTL ilipewa kipaumbele'. Duh utafikiri tuko land locked, yani lita ya petroli ni zaidi ya dola moja Dar es salaam.

Kwa mwendo huu maendeleo Tanzania yatabaki kama msamiati wa kigeni.

Urasimu wa kiwango cha juu bandarini ndio chanzo,Tazama inchi kama Zambia ambazo hazina bandari na hupitishia mizigo yao hapa kwetu bei ya Mafuta kwao sio kubwa kama ya kwetu.swali la msingi hapa kwetu nini kinachosababisha bei ya mafuta kuwa Juu?
 
Kwa hiyo tumebinafsisha serikali? au serikali imeingia ubia na wafanyabiashara? Kitendawili hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom