Ilikuwa ni nguvu ya Nyerere kuitawala Afrika? Au nguvu ya rushwa?

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
ILIKUWA mwaka 1962, jijini Dar
es Salaam, Rais Julius Nyerere kwa wakati huo alifungua
semina ya Mkutano wa Vijana Duniani.


Katika hotuba yake ya ufunguzi
iliyopewa jina la The SECOND
SCRAMBLE,
alitetea ujamaa
akisema utajiri wa nchi unapaswa kutatua kero za wananchi kwa usawa na kero za wachache.


Kwa wakati huo, miaka 51
iliyopita, Tanzania Bara haikuwa
imebobea katika dhana ya matajiri kushindana kuhodhi
hadhi, siasa na madaraka ingawa
pia Mwalimu aliona dalili hizo.


Katika hotuba yake hiyo ya
Kiingereza anasema;

“There is
then ruthless competition
between individual-not to get wealth to feed themselves, or to
clothe themselves, or to house themselves-but to seize enough
wealth to give themselves more
power, more prestige than their
fellows.
“That is, wealth which exceeds their real need and which will
enable them to dominate other
individuals. When that stage is reached, one millionaire is
prepared to spend millions simply in order to destroy
another millionaire.”



Kimantiki, anazungumzia
ushindani usio wa kiutu katika
kujilimbikizia mali ili kuhodhi
mamlaka, hadhi au ufahari.
Kwamba milionea mmoja
anaweza kutumia mamilioni yake
kumshughulikia milionea mwingine.
Kwa kuzingatia mantiki hiyo,
wanaoshangaa rushwa kustawi
katika chaguzi za CCM wasidhani
hilo ni suala la ghafla.


Wasidhani rushwa hiyo ni upepo wa kupita
tu, iwe kwa CCM au vyama
vingine. Rushwa nchini si upepo
wa kupita.


Ni makosa kuitazama rushwa
kwa kuwatazama wanasiasa
pekee. Inawezekana baadhi ya vyama kwa sasa vimekuwa
mawakala wa rushwa, lakini ni
muhimu zaidi kutazama na
kushughulikia chimbuko la mfumo huu wa rushwa.


Mbali na wanasiasa, mfumo wa
rushwa kwa sasa unapaswa
kutazamwa kwa kuwahusisha
wafanyabiashara au wawekezaji
wakubwa.


Tunapaswa sasa kujadiliana
kuhusu mifumo ya uendeshaji
biashara nchini, mifumo ya kodi
na hata mifumo ya kufikia uamuzi kiutawala au kisiasa.


Mifumo ni viwanda vya kuzalisha
watoaji, mawakala na madalali wa rushwa katika sekta zote,
ikiwamo siasa.
Kwa bahati mbaya, Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
wanapotoshwa na kujikuta
wakipambana na matokeo.


Hawapambani na viwanda vya
kutengeneza mawakala na
madalali wa rushwa.

Zingatia maneno haya ya
Mwalimu; “That is, wealth which
exceeds their real need and
which will enable them to
dominate other individuals.When
that stage is reached, one millionaire is prepared to spend
millions simply in order to destroy another millionaire.”


Hapo haina maana
wafanyabiashara waache
kushindana kutafuta faida ya
kupindukia. Tatizo ni namna gani
wanapata faida ya kupindukia?
Kama mwekezaji au
mfanyabiashara amekwepa
mabilioni ya kodi ni dhahiri
atakuwa na mabilioni ya ziada
yanayomshawishi kufikiri namna
ya kukwepa kodi siku zijazo.


Katika kufikiri, atatumia nusu ya
mabilioni hayo kuhodhi mifumo
ya uamuzi ambayo msingi wake
ni siasa.

Atatengeneza wanasiasa wake
ndani ya chama tawala na
upinzani. Ataamua waseme nini,
wafanye nini na kwa wakati
gani. Mabilioni yaliyotokana na
kukwepa kodi yataingilia mfumo
huru wa kisiasa, mfumo wa
kuchagua na kuchaguliwa.

Genge lake litang’ara katika soko
la ununuzi wa kura ndani ya CCM
au chama kingine chochote.
Mwanasiasa anayetokana na
genge hilo sifa yake kubwa ni
kujitengenezea uhalali kwa
kuegemea matumizi ya fedha,
iwe michango kanisani au
misikitini.

Mipango ya kisiasa ya genge la
namna hiyo itaongozwa kwa
nguvu ya rushwa. Hoja ya msingi
kwao ni kuhodhi madaraka,
hadhi na ufahari na si namna
madaraka wanayopigania
yatanufaisha chama au taasisi
husika.

Kwa nguvu za rushwa (si nguvu
za mipango ya maendeleo),
watajipenyeza miongoni mwa
vijana, wanawake na wazee.

Wataimba jina moja teule la
mgombea mtarajiwa wa ubunge
au urais. Mtego mkubwa watakaoutumia
ni kauli mbiu kwamba mteule
wao anazo nguvu za kisiasa.
Kauli mbiu hiyo italenga kuua
hoja sahihi kwamba hizo si
nguvu za kisiasa bali ni nguvu za
rushwa.
Wanaweza kufanikiwa kupata
mgombea ubunge au urais. Hata
hivyo, ni vigumu kwao kupata
mshindi wa kiti cha ubunge au
urais.
Kuwa mgombea ni suala moja na
kuwa mshindi wa
unachogombea ni suala pana
zaidi na sababu ni nyingi.
Kati ya sababu hizo ni ukweli
kwamba, kwa kadiri mipango
yao inavyotekelezwa kwa msukumo wa rushwa ndivyo
wapiga kura halisi mitaani
wanavyoungana kifikra
kumkabili mgombea ambaye ni
zao la mfumo huo dhalimu.
Haya yametokea nchini. Katika
baadhi ya majimbo, nguvu ya
rushwa zilitengeneza
wagombea, wananchi
waliwakabiliana wagombea hao.
Ushauri kwa magenge ya namna
hii ni kutambua, kwa mfano,
nguvu za Nelson Mandela au
Mwalimu Nyerere kisiasa
hazikutokana na kugawa
rushwa.
Rushwa hainunui fikra huru,
wapiganaji wanaounganishwa
kwa nguvu ya rushwa ni mateka
wa baadaye katika jeshi
linaloangamiza rushwa. Ni
mateka

karibu tujadili
 
Mi ngoja niweke mfano. uloandika yote yana taswira kile kinachofanywa na CCM. HASA LOWASSA
 
"that is, wealth which
exceeds their real need and
which will enable them to
dominate other individuals.when
that stage is reached, one millionaire is prepared to spend
millions simply in order to destroy another millionaire."

hapa ndipo point ilipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom