Ilikuwa ni fedheha ambayo sitokuja kuisahau.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilikuwa ni fedheha ambayo sitokuja kuisahau....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Oct 16, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilifahamiana na huyu kijana mwaka 2004, tulipokutana pale kituo cha utamaduni cha Russia, akawa ni rafiki yangu wa karibu sana. Tulikuwa na mazoea ya kutembeleana mara kwa mara na hata pale kwao walitokea kunifahamu vizuri na hata wazazi wake pia walitokea kunipenda sana.
  Huyu hakuwa mwingine bali ni rafiki yangu ambaye alikuwa na ulemavu wa ngozi (Albino) na tulikuwa tumezoeana sana, alikuwa bado anaishi na wazazi wake maeneo ya Ukonga, na mie nilikuwa naishi Tabata.

  Ni tukio ambalo bado mpaka leo nalikumbuka, ilikuwa ni mwaka 2009, kipindi hicho lile wimbi la walemavu wa ngozi (alibino) kuuawa na kukatwa viungo ndio lilikuwa limeshika kasi kwelikweli hapa nchini. Siku moja alikuja nyumbani kwangu akanikosa, bali alimkuta mke wangu Mama Ngina. Hakukaa muda mrefu akaondoka lakini alimjulisha mke wangu kuwa simu yake imeibwa na hana mawasiliano labda mpaka hapo atakaponunua simu nyingine.

  Niliporudi mke wangu alinipa zile salama, lakini kuna jambo alidai anataka tujadili juu ya rafiki yangu, mimi nikashtuka, na kumuuliza, ni jambo gani hilo? Akaniambia kuwa kutokana na hili wimbi la watu wenye lemavu wa ngozi kuuawa na kukatwa viungo vya mwili, inawezekana huyo rafiki yangu akapatwa na tatizo halafu ikatuletea shida, tukawa suspect……………….
  Nilishtushwa sana na kauli ile ya mke wangu, nilikaa kimya kwa muda kidogo, nikitafakari kisha nikamuuliza, ‘Sasa unataka nimkataze asije hapa nyumbani'

  ‘Hapana, sio lengo langu kuvunja urafiki wenu, lakini jaribu kupunguza ukaribu wenu na hasa kutembeleana, ikiwezekana mwambie unasoma na utakuwa unaishi Hostel kwa muda ili asiwe anakuja hapa nyumbani, mwenzio mimi naogopa'
  alijibu mke wangu kwa sauti ya upole. Sikukubaliana naye na tulibishana sana na hatukufikia muafaka wa jambo hilo. Haikupita wiki yule rafiki yangu alikuja na akashinda kwangu kutwa, ilikuwa ni siku ya jumamosi na tulizungumza mambo mengi sana kuhusiana na mradi ambao tulitaka kuuanzisha, lakini pia alinijulisha kuwa huenda wiki inayofuata angesafiri kwenda Morogoro mara moja kuna kitu anafuatilia kule kwa rafiki yake ambaye alisoma naye.

  Siku iliyofuata asubuhi alikuja mdogo wake na yule rafiki yangu na kuniuliza kama kaka yake alikuwa pale kwangu, kwani tangu alipoondoka jana asubuhi kuja kwangu kama alivyoaga hakurejea hadi asubuhi, na simu yake haipatikani kabisa….. mke wangu alinitupia jicho kali kama la kunisuta, nilibabaika kidogo. Nilimjulisha kwamba ni kweli alikuja kwangu na aliondoka mchana kurudi nyumbani kwao. Basi yule kijana akaondoka, lakini huku nyuma mke wangu alinibadilikia na kuanza kunishambulia kuwa mimi sio msikivu na sana nitapata matatizo asipopatikana huyo kijana wa watu, nilibaki kimya na sikujibu aliendelea kunishambulia huku akilia kwa uchungu kuwa nimejitafutia matatizo. Ilibidi niwe mkali kidogo na kumuonya juu ya fikra zake potofu. Ghafla nikawa nimekumbuka kuwa yule rafiki yangu aliniaga kuwa huenda angesafiri kwenda Morogoro kwa rafikiye aliyesoma naye, hivyo nikamtoa mke wangu wasiwasi kuwa huenda kaenda Morogoro na simu yake imeisha chaji na ndio maana haipatikani.

  Ilipofika jioni, nilipata wageni tena, na hawakuwa wengine, bali wazazi wa yule rafiki yangu, wakiwa wameambatana na watu wengine wawili, ambao sikuwafahamu, waliingia ndani na walinijulisha kuwa mtoto wao hajulikani alipo na wanahisi kuwa huenda nahusika na kutoweka kwake. Mimi niliwajulisha kwamba, ni kweli jana alifika kwangu na alikaa mpaka mchana akaondoka, na nikawajulisha kwamba mtoto wao alinidokeza kuwa angesafiri kwenda Morogoro kwa rafikie waliyesoma naye kwani kuna jambo analifuatilia huko. Wazazi wa yule kijana walikanusha kujua lolote juu ya safari hiyo. Lakini wakati bado wakiendelea kuniuliza, mama wa yule kijana alidakia kuwa nipelekwe kituoni nikatoe maelezo, kwani inawezekana nafahamu kilichompata mtoto wao. Nilipinga kupelekwa kituoni, likazuka zogo mle ndani mpaka majirani zangu wakaja kusikiliza kulikoni!

  Miongoni mwa majirani zangu alikuwepo dada mmoja wa Kichaga, ambaye hakuwa na maelewano mazuri na mke wangu, na aliposikia zile tuhuma, alianza kusema kishabiki kuwa tupelekwe kituoni kwani lazima tunajua aliko mtoto wao. Alianza kulizungumza jambo lile kwa dhihaka akisema, 'watu wanajifanya wana hela na kujitia ufahari kumbe wanauza viungo vya albino!' Alikuwa anaongea kwa sauti na kwa ushabiki akitumia lafudhi ya Kizaramo iliyochanganyika na ya Kichaga, alinikera sana.

  Baada ya mvutano mkali mke wangu alinishauri nikubali kwenda kituoni kutoa maelezo, kwa kuwa sikuhusika na kupotea kwa kijana yule. Nilitoka nje uso wangu ukiwa umesawajika kwa fedheha ile. Siku hiyo ndio niliwafahamu majirani zangu kwa rangi zao halisi.
  Nilifuatana na wazazi wa yule kijana pamoja na baadhi ya majirani zangu waliokuwa wameguswa na jambo lile, kwani pia wapo waliokuwa wakinipa moyo kuwa nisiwe na wasiwasi kwa kuwa sikuhusika, basi kila kitu kitafahamika kule kituoni. Mke wangu mama Ngina alikuwa amefuatana na mimi akiwa analia na alionekana wazi akiwa na wasiwasi sana.

  Wakati tuko njiani kuelekea kituo cha Polisi simu ya yule baba wa kijana iliita, alipoitoa mfukoni , alisita kidogo kuipokea, mkewe akamuuliza kuwa ni nani anapiga simu, yule mzee hakuipokea simu ile alibaki kuikodolea macho akiwa ameishika mkononi. Mmoja wa wale watu aliofuatana nao ambaye nilikuja kuambiwa kuwa ni shemejiye, aliichukua ile simu na kuipokea, ‘haloo, nani anaongea…………..aah mjomba, uko wapi?'
  Wakati anaongea na simu ile wote pale tukajua kuwa alikuwa ni yule kijana aliyekuwa akitafutwa, na watu wote tulikuwa kimya………..yule mjomba hakumwambia kuwa anatafutwa, ila alimdanganya kuwa mama yake yu mgonjwa na anahitajika nyumbani haraka. Alikata simu na kusema, ‘Ni Msakuzi, ni kweli yuko Morogoro na simu yake iliisha chaji akawa amekosa chaji tangu jana na leo kutwa.' Wote tulishikwa na butwaa, na wazazi wa yule kijana waliniomba radhi kwa usumbufu wote uliotokea.

  Sikuwajibu kitu, nilimshika mke wangu Mama Ngina na kurudi nyumbani. Ni fedheha ambayo sitokuja kuisahau………………………………
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Pole qaqa, ni ajali kama ajali zingine! tukio lako limenigusa sana!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  dah........hii inahitaji movie aisee.....
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, nimejisikia vibaya sana kusoma hii habari yako.

  Je umejifunza nini? kumsikiliza mke? au kusimamia maamuzi yako?

  Nakupa pongezi sana kusimamia maamuzi yako ya kutom'bagua rafiki yako. Japo imekuletea matatizo lakini naamini katika maisha ni vizuri kusimamia unachokiamini hata kama kinakupeleka kubaya! huyo ndiyo anakuwa WEWE HALISI

  Pole...life continues...
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  director nipo...naivutia kasi!
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  pole sana rafiki. Hatuupendi unyanyapaa, lakini nyakati nyingine inabidi, ili tuwe salama na tuepukane na kazi ya kuisaidia polisi kazi bila mshahara
   
 7. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ni kweli tukio linatugusa wengi, hasa ambao wake zetu wana mahusiano mabaya na majirani. Ila sijaelewa hiyo 'qaqa' ndio nini!
   
 8. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Duu, pole sana, maana kama nilikuwa naangalia movie ya kutisha vile, sasa umeamuaje kuhusu hatma ya urafiki wenu? ulizungumza na huyo rafiki yako?
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hii hadithi imenikumbusha kuna mtu alienda mtwara aka chumbia msichana....
  but jamaa alikuwa 'mdhaifu dhaifu' wa afya....

  ndugu wakashika bango kuwa 'hakuna ndoa mpaka wakapimwe hiv....

  kwenda kupimwa jamaa mzima,msichana ameathirika.....lol
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Urafiki bado unaendelea na siku hizi tumekuwa kama ndugu hasa.......... ni tukio ambalo kila mmoja amejifunza kwa kweli
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kweli eh! Ngoja nimtafute Kanumba, laweza kuwa ni Bonge la Idea..........
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyo rafiki yako mpige ban, jamaa wasaka viungo bado wapo.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Walimwokoa mshikaji bila kujua, maana na hali yake ya udhaifu dhaifu angeviongezea na vidudu angekufa kipindi cha seroconversion!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni kweli nimejifunza mengi, lakini jambo moja ambalo wengi mnaweza msilifahamu, ni kwamba, ile nguvu ya lile tukio ilivutwa na mke wangu.....Najua hakuw na nia mbaya lakini kanuni ya maumbile iko hivi....... kila tunachokiwaza na kukiwekea nguvu , mara nyingi hututokea, mke wangu aliweka kiunzi kwa kutojua, na na ndi maana watu husema kauli huumba. Baada ya tukio lile nilikaa na mke wangu na kumpa Darasa kuhusiana na kanuni ya maumbile na ameelewa vizuri sana.
  Pioa nilikwenda katika familia ile nikiwa na mke wangu na kuzungumza nao na tukayamaliza.............
   
 15. samito

  samito JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  dah, pole lakin hongera kwa kumthamin rafik yako, mke ni muhm kumsikiliza lakim sio kila ki2. kama mdau alivyosema inaitaji movie au itungiwe wimbo
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  The Boss hata mimi niliwahi kuisikia hii
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kweli ni kisa cha kusikitisha, jambo ambalo sijaelewa ni fedhea hii ni kwako au kwa ndugu wa rafiki yako? Hakuna popote kwenye habari yako umefafanua hili,
   
 18. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Inatamkwa 'kwakwa'
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Hii inatokea sana....watu wengi bado tunawapima HIV wenzetu kwa kutumia macho!
   
 20. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Mimi naona ni pande zote zilipata kufedheheka kwa nyakati tofauti. Kabla ya ukweli kuwa wazi ni mleta mada ndiye kwa hakika alifedheheka!
   
Loading...