Ilikuwa lazima aje au kalazimishwa


R

Rwey

Senior Member
Joined
Jul 11, 2008
Messages
103
Likes
1
Points
35
R

Rwey

Senior Member
Joined Jul 11, 2008
103 1 35
Emmanuel Mrema
Daily News; Friday,July 11, 2008 @00:05

Mrembo wa Watanzania wanaoishi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya (Miss EU) Lucy Fundikira kutoka Uholanzi ni miongoni mwa warembo wanne waliojitoa katika kinyang’anyiro cha kumsaka Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania 2008).

Shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania limepangwa kufanyika Agosti 2 jijini Dar es Salaam katika ukumbi utakaotangazwa baadaye. Akizungumza na HabariLeo jana Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga alisema walifanya taratibu zote za kumtumia tiketi Lucy kuja kujiunga na wenzake kambini Hoteli ya Paradise, Bagamoyo lakini waliambiwa hatafika.

“Tumewasiliana na mwakilishi wa Lucy baada ya kukamilisha taratibu zote za kumwezesha kuja nchini, lakini alituthibitishia hataweza kuja kushiriki katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tanzania bila kutaja sababu.

“Nafasi yake imezibwa na mrembo kutoka Kanda ya Ziwa aliyetokea Shinyanga, Regina Julius aliyeshika nafasi ya nne na tayari amewasili na kuungana na wenzake kambini,” alisema Lundenga. Aliongeza kuwa mrembo wa Kanda ya Kati, Irine Salala ambaye juzi hakuwapo alikuwa njiani kuwasili katika kambi hiyo na alitarajia kuwasili muda wowote jana.
 

Forum statistics

Threads 1,238,253
Members 475,878
Posts 29,313,793