Ilikuaje Power Kaaya kuhukumiwa haraka kwa kesi ya ugaidi?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Hivi ilikuaje Power Kaaya aliyemaliza kutoa ushahidi leo mahakamani yeye na mwenzake walikamatwa haraka, wakashtakiwa haraka na kisha kuhukumiwa haraka kwa kesi ya Ugaidi bila kuunganishwa na Wenzake hawa kina Mbowe na Walinzi wake?

Kwani kwa ushahidi huu aliotoa mbona hakuna utofauti wa kesi yake na hii inayoendelea hivi sasa? Kwanini baada ya Mbowe kupelekwa gerezani wao wakaachiwa?

Hii nchi ina mambo mengi sana ukitaka kuyawaza sana uyapasuka kichwa. Hata kuna siku nitakaa na wanangu nitawaambia haya haya.

Haya tunaona mashahidi mpaka sasa upande wa jamuhuri ni kada wa CCM na Mapolisi,haya mambo iko siku tutasali sana kumuomba Mungu.
 

Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
4,324
2,000
Hii kesi imetengenezwa mahususi na vijana wa Mzena, lengo ni kuwatoa watu kwenye kujadili swala la katiba mpya maana moto wa Mbowe ulikuwa mkali, wanachofanya ni kuvuta attention ya raia kutoka kudai katiba kwenda kwenye kujadili swala la kesi then baadae wanamuachia Freeman wakiona upepo umepoa.
 

Townchild

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,578
2,000
Hii kesi imetengenezwa mahususi na vijana wa Mzena, lengo ni kuwatoa watu kwenye kujadili swala la katiba mpya maana moto wa Mbowe ulikuwa mkali, wanachofanya ni kuvuta attention ya raia kutoka kudai katiba kwenda kwenye kujadili swala la kesi then baadae wanamuachia Freeman wakiona upepo umepoa
Je huo sii weledi wa Kitanzania, je sii sehemu ya siasa chafu na ukosefu wa uongozi Bora?
 

boomgate

JF-Expert Member
Jan 15, 2021
248
500
Hii kesi haijalishi imetengenezwa na watu wa serikali au usalama wa taifa ila ukweli ni kwamba ukitaka kudeal na watu wakubwa hasa mtu kama mbowe lazima uwe na akili ya ziada dunia ya sasa hivi imeisha badilika sana, Iwe leo au kesho katiba mpya itakuja tu yaani ni suala la muda hapo ni sawa na tatizo kulisogeza mbele wakati unajua liko pale pale
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
10,477
2,000
Wanatumia Vibaya kodi zetu kuendesha kesi bandia..

Ugaidi wa kuweka magogo road?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom