Ilianza kampeni ya "Magufuli Baki" ikaja "Operation Ng'oa Magufuli" sasa ni Operation "UKUKU".

Mimi naungana na prof Kitila mkumbo ktk kitu kinachoitwa ODD. Yaani OPPOSITION DEFIANT DISORDER. Huu ni ugonjwa ulioikumba upinzan yaani wanakitu kinamiss ktk ubongo wao kinachopèlekea wawe wanapinga kila kitu.ebu tuangalie ktk muktadha wa kioja hicho cha UKUKU.

Wapinzan ndio waliokuwa wanaimba jk ni dhaifu na kwa miaka kumi nchi haikuwa na Rais bali ilikua inajiendesha kwa NEEMA TU.Walifika mbali sana hadi kutumia vipeperush vyao kuomba Tanzania ipate Rais dikteta. Walieleza sabb nyingi mno na kwel ktk sabb walizozitaka Mungu akasaidia akapatikana JPM. Cha ajabu mwaka haukuisha wakaanzisha operation ya kupinga kile walichokihitaj UKUTA.Hapa ODD INAHUSIKA

Katika harakati zao walikua ni vinara wa kusema toka miaka 50 ya uhuru ccm haaijafanya kitu chochote na walikua vinara wa kutuma picha watu wakinywa maji pamoja na mifugo na wagonjwa hospital wakilala wawil wawil na wengine chini.Baada ya jpm kuingia wakageuka na kuanza kumsifia jk kuwa ni kiongoz bora toka Tz ipate uhuru.Ni kitu cha kustaajabiaha kidogo lkn ndo upinzan wetu. Nakumbuka mwaka 2015 UDOM UDSM na mzumbe tena kwa nyakati sawa walikua kwenye mgomo wa kukosa hela za kujikim yaani boom na nakumbuka kipind UDOM tunaandamana jk na serikal yake nzima walikua DODOMA tuliomba kuonana na PM lkn tuletewa mabom ya machozi na virungu. HAISHANGAZI kusikia BAVICHA akisema utawala wa jk uliwajali wanafunz.tatizo ni ODD.

Chama ndani ya mwezi mmoja kinakuwa na kauli mbili zinazokinzana.HII HUTOKEA TANZANIA TU.Wakati wa bunge la bajet likiendelea 2017 upinzan waliamka kwa vifijo na nderemo na kuimba wanaiman na jk.ni haohao walioimba jk tumekumc. ANGALIA HUU UGONJWA UNAVOWATESA.Saizi wanataka jk aondolewe kinga nae ashtakiwe.KIONGOZI BORA TOKA UHURU,KIONGOZI waliyemc leo hii wanapiga kelele ashtakiwe. Sehem zingine ni maajabu ila TANZANIA ni kawaida sana.

Yule kiongoz aliyemkashifu baba wa taifa hadi kufika mbali kuwa ALIZOEA VYA KUNYONGA na kushangiliwa na wafuas wake leo hii kiongoz yuleyule anamtumia baba wa Taifa katika upande wa uzur kujenga hoja
zake na wafuas walewale wanamshangilia.

Haishangazi hata kidogo kwa yanayotokea Tz.mtu badala ya kujiuliza nini kipya nje ongezeko la 2% ye anakazania kupinga tu.yako mengi lkn ngoja niishie hapa

sent from kitochi using jamii forum
Hujaelewa maana ya UKUKU. Kumweleza JK kwamba ni dhaifu ilikuwa sahihi, na wapinzani walitumia haki yao ya kikatiba kutoa maoni yao, na kukosoa utawala wa JK ili uboreshe na kurekebisha makosa. Lengo la kukosoa ni yule anayekosolewa arekebishe makosa. Nyerere pia alikosolewa sana tu na Prof. Shivji enzi zile za ujamaa. Mojawapo ya criticism ya Shivji ilikuwa kwamba Ujamaa wa Nyerere hauna "theoretical foundations". Nyerere alijibu mapigo kwamba hahitaji theory kama za ki-marx katika kutatua matatizo ya watanzania. Nyerere hakumpima mkojo Shivji, wala hakumfungulia mashitaka ya uchochezi. bali alimjibu pale Nkrumah kwa hoja. Miaka kadhaa baadaye tunamshuhudia Shivji akiwa mtetezi mkubwa wa Nyerere. Contradiction? Hapana! alimsaidia Nyerere kuongoza nchi, kwa kum-challenge. sasa anachambua yale mazuri ya Nyerere na kuyaenzi, ili kama alivyosema Nyerere mwenyewe, watu wachukue mazuri yake na mabaya wayaache!! upo hapo?

Sasa JK alikuwa na mabaya yake mengi sana. wanaCCM, UKUKU katika ubora wake, waliyasifia yote bila kuhoji. wapinzani waliyahoji hayo mapungufu, ikiwemo ufisadi, escrow, safari nyingi mno za nje, nk. CCM walipinga kuhoji kwa wapinzani, siyo kwa hoja, bali kwa maana tu ya kupinga na kuzomea. Katika hotuba yake kwa Bunge, JPM alishambulia sana safari za nje, na wanaccm, katika UKUKU uliokomaa, wakamshangilia sana!!
Lakini JK alikuwa na mazuri yake. aliruhusu wapinzani wafanye mikutano yao, japo mifumo mbalimbali katika serikali yake ilipinga, na ilifikia mahali JK aliwaambia CCM wasitumie Polisi kujibu mashambulizi ya wapinzani - hili alilisema katika mkutano mkuu Dodoma. Wapinzani walimuunga mkono JK katika hayo. hawakumkosoa kwa kuwaruhusu kumkosoa. pia walikuwa wanajadiliana naye mpaka huko ikulu, huku "wakinywa chai na juisi ya ikulu". mara kadhaa mijadala hiyo ilizaa maelewano yaliyowezesha mambo yaende mbele, wapinzani wakipata pale na kupoteza pale. wengi waliwakosoa wapinzani kwa kukubali kushiriki michakato ambayo CCM walikuwa wanairatibu kwa karibu. wapinzani kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano na maridhiano, walishiriki. hawakumkosoa JK kwa hayo yote, bali walimsifia.

Kwa hiyo si kweli kwamba wapinzani walimkosoa JK kwa kila kitu. walimchallenge ili atatue matatizo ya watanzania kwa uzuri zaidi na more effectively. huko ni kumsaidia. lakini CCM hawakumsaidia kwa kweli. hata mtu yeyote akifanya kosa ukamsifia, unamharibu na humtakii mema. Leo wapinzani wanaposema kwamba wanammiss JK, ni kwamba wanakumbuka kwamba alikuwa anasikiliza criticism zao. alizifanyia kazi alipoweza. sasa kuna tatizo gani hapo???

JPM hataki kukosolewa. kaomba kazi kwa watanzania, tena kwa kupiga push-up, leo hataki kusikiliza ushauri wala criticism. wapinzani wapo kisheria kwa ajili ya kukosoa. kuwakataza na kuwanyima nafasi hiyo ni kuvunja katiba. mtu anayefanya hayo anapoambiwa, anakuja juu. lakini wana-UKUKU wao hawaoni kitu chochote.
 
Back
Top Bottom