Ilianza kampeni ya "Magufuli Baki" ikaja "Operation Ng'oa Magufuli" sasa ni Operation "UKUKU".

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,908
2,000
Kwa hisani ya Kwintara Kwinyira.

Imezinduliwa kampeni ya kupinga UKUKU nchini. UKUKU means (Umoja wa Kukubali kila kitu bila Kuhoji).

Kuna watu kazi yao ni kuunga mkono kila kitu ili mradi kimesemwa na kiongozi wao.
Tabia hii imeshamiri sana kwa wafuasi wa CCM. They dont reason at all, Ila mradi kiongozi kasema wao ni NDIOO.
Godbless Lema anasema tatizo sio wao, tatizo ni akili zao. UTG wanaita huo ni uzwazwa, lakini Kwinyara anasema ni UKUKU. Kukubali kila kitu bila kuhoji ni UKUKU.

Watu walewale waliosema JK aongezewe muda, kwa kuwa amesaidia sana taifa, ndio haohao wanaokazana sasa JPM aongezewe muda na kusema JK aliharibu nchi. UKUKU.!

Watu walewale wanaoshangilia viongozi wa upinzani wakikamatwa kwa kufanya mikutano ya siasa, ndio haohao wanaoshangilia CCM ikifanya mikutano. UKUKU.!

Watu walewale wanaopitisha mrabaha wa 04% kwa makofi na kusema unatosha, huku wakiwazomea wapinzani waliposema hautoshi, ndio haohao wanaoshangilia kufikishiwa 06%.
Mnashangiliaje kupandishwa kwa kitu mlichosema kinatosha? UKUKU.!

Na kwa sasa wapinzani wanasema 06% hazitoshi, wao wanasema inatosha. Akija Rais baada ya JPM akaziongeza tena watashangilia na kumuita mzalendo. UKUKU.!

Watu walewale walioshangilia Ngeleja kurudisha hela TRA ndio haohao wanaoshangilia TRA kuzikataa. UKUKU.!

Walioshangilia JK aliposema pesa za Escrow si za umma, ndio haohao wanaomshangilia JPM kusema pesa zilikua za umma. UKUKU.!

Nchi hii imeharibiwa na hawa KUKU. Kila kitu wanakubali tu bila kuhoji. Kataa UKUKU,
U = Umoja wa
KU = kukubali kila kitu bila
KU = kuhoji.
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,398
2,000
Mtu kuwa ccm inabidi uwe Kama jongoo hawaelewi njia hawa maccm, Sura zao tu wanalia Kama wanacheka, Nikiona zile nguo zao za kijani nahisi kichefuchefu maccm ni mikuku

Sent using Jamii Forums mobile app
 

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,659
2,000
ukuku.jpg
Shetani mkubwa lazima tumvue ukuku


Swissme
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,735
2,000
Watanzania wanyonge Masikini wanazidi kutaabika
Wanyonge/Masikini wanapata mlo mmoja kwa sababu ya Mfumuko wa bei (sukari, Sembe etc)


Kukamata wapinzani ndio inawapa masikini mlo?

Mbona hatuoni mafisadi wakifilisiwa na kufungwa?

Movie inaendelea mpaka 2020...

Hataki Demokrasia, ana kampeni ya kupitishwa eti
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,034
2,000
Hivi maghu anakuwa anajiamini utafikiri yeye malaika au karogwa au wale jamaa wa bagamoyo walimchanja kunako ? Kila mtu atapita tuandae mazingira ya kuishi vizuri uraiani.
 

MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,399
2,000
Mimi naungana na prof Kitila mkumbo ktk kitu kinachoitwa ODD. Yaani OPPOSITION DEFIANT DISORDER. Huu ni ugonjwa ulioikumba upinzan yaani wanakitu kinamiss ktk ubongo wao kinachopèlekea wawe wanapinga kila kitu.ebu tuangalie ktk muktadha wa kioja hicho cha UKUKU.

Wapinzan ndio waliokuwa wanaimba jk ni dhaifu na kwa miaka kumi nchi haikuwa na Rais bali ilikua inajiendesha kwa NEEMA TU.Walifika mbali sana hadi kutumia vipeperush vyao kuomba Tanzania ipate Rais dikteta. Walieleza sabb nyingi mno na kwel ktk sabb walizozitaka Mungu akasaidia akapatikana JPM. Cha ajabu mwaka haukuisha wakaanzisha operation ya kupinga kile walichokihitaj UKUTA.Hapa ODD INAHUSIKA

Katika harakati zao walikua ni vinara wa kusema toka miaka 50 ya uhuru ccm haaijafanya kitu chochote na walikua vinara wa kutuma picha watu wakinywa maji pamoja na mifugo na wagonjwa hospital wakilala wawil wawil na wengine chini.Baada ya jpm kuingia wakageuka na kuanza kumsifia jk kuwa ni kiongoz bora toka Tz ipate uhuru.Ni kitu cha kustaajabiaha kidogo lkn ndo upinzan wetu. Nakumbuka mwaka 2015 UDOM UDSM na mzumbe tena kwa nyakati sawa walikua kwenye mgomo wa kukosa hela za kujikim yaani boom na nakumbuka kipind UDOM tunaandamana jk na serikal yake nzima walikua DODOMA tuliomba kuonana na PM lkn tuletewa mabom ya machozi na virungu. HAISHANGAZI kusikia BAVICHA akisema utawala wa jk uliwajali wanafunz.tatizo ni ODD.

Chama ndani ya mwezi mmoja kinakuwa na kauli mbili zinazokinzana.HII HUTOKEA TANZANIA TU.Wakati wa bunge la bajet likiendelea 2017 upinzan waliamka kwa vifijo na nderemo na kuimba wanaiman na jk.ni haohao walioimba jk tumekumc. ANGALIA HUU UGONJWA UNAVOWATESA.Saizi wanataka jk aondolewe kinga nae ashtakiwe.KIONGOZI BORA TOKA UHURU,KIONGOZI waliyemc leo hii wanapiga kelele ashtakiwe. Sehem zingine ni maajabu ila TANZANIA ni kawaida sana.

Yule kiongoz aliyemkashifu baba wa taifa hadi kufika mbali kuwa ALIZOEA VYA KUNYONGA na kushangiliwa na wafuas wake leo hii kiongoz yuleyule anamtumia baba wa Taifa katika upande wa uzur kujenga hoja
zake na wafuas walewale wanamshangilia.

Haishangazi hata kidogo kwa yanayotokea Tz.mtu badala ya kujiuliza nini kipya nje ongezeko la 2% ye anakazania kupinga tu.yako mengi lkn ngoja niishie hapa

sent from kitochi using jamii forum
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom