Ilianza balozi kutoa ONYO, likaja baraza la Congress, sasa Ikulu ya Marekani ila Kiburi, majivuno yatazaa Vikwazo vya kiuchumi kujiona sisi matajiri

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Naomba tukumbushane hapa,

Balozi wa Marekani alishatoa maonyo mengi juu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo hali ya demokrasia nchini, uhuru wa habari (Kabendela), mahakama kuingiliwa na kutotoa haki ikiwemo kubambikiziana kesi kwa vinogozi wa vyama pinzani, watu kupotea na kutekana, haki za watoto hasa wanaopata mimba mashuleni nk.

Ikaja baraza la Congress kumwandikia rais Magufuli mwezi Dec 2019 lakini sio Ikulu, wala wizara ya mambo ya nje iliyojibu kwa press kama walivyofanya hao wanaoitwa Mabeberu.

Jana Ikulu ya Marekani imeanza process ya kuwekea vikwazo watanzania na baadhi ya viongozi kuingia marekani ikiwa ni mwanzo wa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Huku kujimwambafy kunatuumiza hasa sie raia kwa viongozi wazembe ambao wanakula na kulala kwa kodi zetu.

Ifike kipindi tuwaambie zile ngojera za kiwa mabeberu wanatuonea wivu ni wivu gani wakati kila kitu kinatoka kwao kuanzia teknolojia hadi wafanyakazi wa hiyo miradi tunayojidai nayo?
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
 
Lugha ya mabeberu inaboa sana maana Ukimwita fulani ni mabeberu basi wewe ni jike.
Tuache hizo bhana.
By the way, kuna watanzania hawataki hata kujua USA ndio nini
Wanao nufaika na Uwepo wa hao USA pambaneni
Sisi donar country mutuachie inchi yetu
Marekani nao wamekuwa wa kisusa Susa kama sio mabeberu bwana!!!
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.


P


Tutaingia tu bila visa...au sio
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.


P
Naona umeshasahau uliyomtendea Kabendera na hapa kwa comment yako hiyo fupi umedhihirisha kuwa kinachompata kabendera ni halali yake!
 
Yaani kabudi mabada atumie muda wake kujena mahusiano mazuri kati ya TZ na mataifa wahisani yeye anatoa macho eti anasaidia zimbabwe iondolewe vikwazo vya kiuchumi! sasa yeye akiwekewa vikwazo sijui nani atakuja kumpigania.
We nawe unakuwa kama haujui DIPLOMASIA ya sasa? Ngoja nikusaidie, wakubwa wanasema hivi " Hawaji kwetu na sisi hatuendi kwao" a new economic diplomacy in town!! 😂
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
huo uwezo wa kusimama mtaupata wapi wakati mtakuwa na njaa mtaishia anguka nae kama kuku mwenye mdondo.
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
wewe ni mzalendo au shushu
 
Jana Ikulu ya Marekani imeanza process ya kuwekea vikwazo watanzania na baadhi ya viongozi kuingia marekani ikiwa ni mwanzo wa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Huku kujimwambafy kunatuumiza hasa sie raia kwa mabeberu wanatuonea wivu ni wivu gani wakati kila kitu kinatoka kwao kuanzia teknolojia hadi wafanyakazi wa hiyo miradi tunayojidai nayo?
Hawa ni mabeberu tuu na huu ni wivu juu ya maendeleo yetu na demokrasia yetu ya Tanzanian Democracy ambayo ni part of African Democracy.
Wazalendo wa kweli wa taifa hili, hatuta kubali ubeberu huu, tutasimama na rais wetu.

P
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
Kwa hiyo dreamliner tutakuwa tunanunua wapi?
 
Nchi yoyote duniani inapobadilisha mikataba ya madini( dhahabu, almasi, mafuta, gesi n.k) inakuwa adui mkubwa wa Marekani na Ulaya, hayo mengine ni kuhalalisha uharamia wao.

Tanzania inatumia mfumo uleule wa kidemokrasia wa uchaguzi tokà mwaka 1995 na hakuna hata siku moja waliona Kuna kasoro, kasoro wameiona awamu hii ya 5, kwa Nini? Kwa sababu Rais Magufuli kàbadilisha mikataba ya Madini
 

Similar Discussions

74 Reactions
Reply
Back
Top Bottom