Iliaanzaje wanawake & wanaume wakajihodhia maeneo ya kulala ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Washikadau,
Katika hili sihitaji kulitolea Source wala ushahidi.
Kila Member ni Sourcer kutoka katika mazingira anayoishi.
Anzia huko tunakokuita Dunia ya kwanza , ya pili, ya 3 , na kama ya 4 ipo ! Iweke kundini.
Katika Dunia zote hizo unapowadia muda wa kulala, basi mwanzoni mwa Kitanda atalala Mwanaume na nyuma yake Mwanamke.
Zingatia about 85% Vitanda huwekwa upande wa pili huwa karibu sana na ukuta na vingine hugusa kabisa ukuta ( na ndiyo upande unaolaliwa na Wanawake)
Hata wenzetu wavulana ambao hawajaoa, pindipo amefumania deal na Mrembo wake mlalo ni huohuo!
Hii ni :
- Declaration ?
If yes, ya wapi ?
- Treaty ?
If yes, ya wapi ?
- Agreement ?
Kama ndiyo ya wp?
Nimejiuliza ulalaji huu kama ni umetokana na sababu za Kisayansi , basi ungekuwepo katika mitaala ya Biology na tangia mashuleni tungefundishwa.
Au kama kuna Mwanaume hapa Jf ambae hulala nyuma ya Mkewe/Mpenzi wake anisute mlango nauacha wazi.
Na kama pia yupo Mwanamke ambae nae hulala mbele ya Mwanaume/Mpnz wake , nae anisute !.
Nimalize kwa kuuliza huku kujihodhia nafasi/eneo la malazi b'twin two genders kulianza'anzaje ?
Na mantik yake nini ?
Naomba kutoa hoja.
 
mie kwangu vise versa, maana kitanda kipo katikati,

Kwa Kitanda kua kati mmh ! Sadiki ukipenda!
Hata Shakila aliwahi kuitolea Thrade yake kupitia Wimbo! Akisema ametembea Ulaya hadi Asia hajakuta kitanda kimewekwa KATI kanuni ama ni mila (mie sijui) kitanda huwekwa pembeni.
 
Mie bachela huwa nalala katikati, mwanzoni, mwishoni, pembeni, mbele au nyuma nalala tu wala sijipi shida...
 
aise mm binafsi nimezoea tu...
hata leo hii ukija geto kwangu,na ikatokea umelala na mm,ukutani kunakuhusu...
kwa iyo nategemea hata nikiwa na mke itakua vivyo hivyo..
 
Mie bachela huwa nalala katikati, mwanzoni, mwishoni, pembeni, mbele au nyuma nalala tu wala sijipi shida...

Mtalingolo ndg yangu pamoja na usimbe unaojinadi nao, inapotokea umefumania turufu ya Mlupo, au Fiacee wako (kama unae) mnalalaje ? Mbele nani ? Nyuma nani? Funguka !
 
Mie pia huwa nalala kwa raha zangu kama mtalingolo...

Je ? Siku ya dash-dash katika kunanihii kula makitu , itakua kama Mtalingolo? Si ufunguke ! Unamuogopa nani Amyner !
 
aise mm binafsi nimezoea tu...
hata leo hii ukija geto kwangu,na ikatokea umelala na mm,ukutani kunakuhusu...
kwa iyo nategemea hata nikiwa na mke itakua vivyo hivyo..

BAGAH ! Yaani uongeaji wako true waonekana hauko serious !
 
Naeza kusema ni natural instincts tu, it comes naturally kwa sababu mwanaume is beleived to be a protector of his wife/woman. Kwa hiyo kulala nyuma yake au pembezoni ambako hakuna mlango zaidi ya dirisha na ukuta its more appropriate/reasonable. Incase anything happens like some sort of an alert the man can dash out quickly to the exit as the wife is rightly behind him. That's how I see it
 
Mi huwa tunalala kama wale wazungu kwnye karata.
MP.
 
Naeza kusema ni natural instincts tu, it comes naturally kwa sababu mwanaume is beleived to be a protector of his wife/woman. Kwa hiyo kulala nyuma yake au pembezoni ambako hakuna mlango zaidi ya dirisha na ukuta its more appropriate/reasonable. Incase anything happens like some sort of an alert the man can dash out quickly to the exit as the wife is rightly behind him. That's how I see it

Js , unanata na bit! Points zako zinaendana kabisa na real uhalisia. Nimeipenda hii.
 
Mi sijawahi kulala na mtu

Jamani ! Fix nyingine !
Anne Makinda atudanganye viwango vya malazi vimepanda Dom,
Chenge nae atudanganye mavumba ya Radar hajalamba!
Na wewe pia utudan.... ?
Unfair play !
 
Back
Top Bottom