Ili ufanikiwe kwa kitu chochote unachofanya hasa fani au kipaji chako soma haya zingatia tia akilini

Bizzmc

Senior Member
May 2, 2016
187
184
1.Kwanza jitaidi sana usiwe mchoyo wa knowladge ulionayo kwa wenzio kuwa muwazi pengine unaweza ukawa una tango umekaa nalo..

2.Jitaidi sana kuwa mtu wa practical sana na kujipangia project mbalimali binafsi za kuzifanya bila kusimamiwa..

3.Epuka sana kujifanya unajua yote na umeshakamilika hiyo haitakupa nguvu ya kujifunza mengi utahisi unajua kila kitu (epuka ujuaji sana.)

4.Jitaidi kujitesa sana na kushilikiana na wenzako kwa lolote usiwe mbinafsi hat kwa kidogo ujuacho...wengine hata kukupa program anahisi noma..

5.Kubali challenge na vikwazo maana vitakupa nguvu ya kujijua unaweza vipi kusonga mbele.

6.Usiogope sana mbwembwe za watu maana watu wanaoongea sana na mbwembwe nyingi ni mabingwa wa kuwatisha sana wengine na unaweza kujiona upo vibaya kumbe sio...watu wanaoongea sana na mbwembwe nyingi mara nyingi wanakuwaga hamna kitu mbwembwe tu so usiogope maneno ya watu...

7.Chagua mambo yako unayohisi unauwezo mkubwa sana kuyafanya yafanyie sana kazi ikibidi weka latiba ya hiko kitu kila siku I.T pana sana huwez maliza yote kama unapenda database kazia sana utakuwa bora zaidi.

8.Usiwe mtu wa kujiona mdhaifu pindi unaposhindwa na jambo flani haya mambo kila mtu hajazaliwa nayo,jua kila unapokosea ndio hatua ya kujua vizuri zaidi.

9.Jitaidi kujenga urafiki na kuwa kalibu na watu waliokuzidi sana knowladge na epuka kujifananisha na mtu alie levo zako,hautapata changamoto ya kujifunza kwa nguvu so keep it up.

10.Jfunze kwa malengo nia na kuthubutu ila usijifunze ili upate sifa tu hazitakusaidia chochote pia epuka kulewa sifa zisizokusaidia chochote offcoz mi napenda sana maoni kuliko kusifiwa sifa zinamfanya mtu kulemaa so epuka hiyo mambo...

11.Jaribu kujiunga katika makundi mbalimbali yanayohusu fani yako forum mbalimbali za mbele na bongo mfano hii group safi sana admin inasaidia sana watu so kwa kufanya hivo utakuwa mkali sana coz utajifunza na kushare idea sana na wenzako.

12.Jitaidi sana kuwa mbunifu hasa katika designing usiogope kujifunza kutoka katika kazi za wenzako kama umeona mwenzako kafanya vizuri msifie nawewe komaa ufanye zaidi yake na sio uanze majungu hayatakusaidia kitu.

13.Kumbuka i.t technology is not static so usilidhike na kitu ulichonacho jitaidi kusoma sana mambo mengi na kuwa updated coz inawezekana unachojua kiko out of date...

14.Epuka sana dharau na mjungu usimdharau mtu yoyote pindi anapokuomba umsaidie jambo huwezi jua kitu gani anacho pengine anaweza kuwa na msaada kwako na ni mkali zaidi yako.

15.Jitaidi sana kufanya mambo yako kwa makini mkubwa na kama sio lazima watu wengine kuyajua piga kimya epuka mboyoyo mingi,mbwembwe na majigambo yasio kusaidia..coz kuna mtu kama anajua kitu hata kidogo tu kimoja basi anahisi I.T yote kaijua nop utapotea mazima badilika...

NI hayo tu guys love you all.....

Hayo ni machache ambayo nayazingatia sana katika fani hii na nasonga mbele siku hadi siku so kama yamekuingia gonga like au kama unachakuongezea welcome coz nimeona watu wengi wanabugi padogo sana kwa kutokujielewa wanahitaji nini.......
11913230_1449941725314239_8360699879271944125_n.jpg
 
Back
Top Bottom