Ili tutoke hapa tulipo,tunahitaji wanasiasa,wanaharakati na viongozi wa dini wenye maamuzi magumu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Niwaambie tu kwa aina hii ya viongozi tulionao leo hii na kwa jinsi wanavyotoa majibu mepessi kwa maswali magumu,bila kuwa na wanasiasa,wanaharakati na viongozi wa dini wenye maamuzi magumu,hakuna tutakacho-achieve na zaidi hakuna kitakachobadilika.

Na wala msitegemee eti tuna Bunge linaloweza kusimama na kutimiza wajibu wa kikatiba kwa niaba ya wananchi kwa kufanya maamuzi magumu ya kikatiba.

Hili nalo msitegemee kabisa kutoka kwa wabunge hawa wenye masilahi manono na maisha mazuri huku baadhi yao wakiwa na rundo la vitega uchumi mitaani.

Watanzania wamekosa tu watu wa kuwaongoza na kuwahamasisha na ipo siku watajiongoza wenyewe baada ya kuona waliowapa dhamana hawana tena msaada kwao.

Ni ukweli pia tunahitaji wanasiasa, wanaharakati na viongozi wa dini ambao hawana cha kupoteza au wako tayari kupoteza walichonacho kuwapigani na kuwatetea watanzania kwa gharama yoyote tena bila kuchoka.

Ipo siku tutapata kizazi cha wanasiasa na wanaharakati ambao wametoka vyuoni na mitaani na ambao hawana ajira wala mali za kupoteza na ambao watakuwa teyari kuwaongoza watanzania ambao nao idadi yao kubwa watakuwa hawana cha kupoteza.

Tusubiri idadi ya wasio na ajira iendelee kuongezeka,wanoamaliza vyuo na kukosa ajira na kushindwa kujiajiri waendelee kuongezeka, wanaopoteza ajira waendelee kuongezeka, kilimo kiendelee kudorora na wanaokataa tamaa ya maisha nao waendelee kuongezeka alafu tutaona matokeo yake.
 
Back
Top Bottom