Ili Tusonge mbele Tunahitaji Mahakama ya Wanasiasa

MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
1,336
875
Katika nchi inayotawaliwa na rushwa katika kila idara ya serikali kama ilivyo Tz sasa, uwepo wa mahakama inayofuata msingi wa sheria (kama inavyokuwa kwenye nchi zilizoendelea) unakosa maana. Mfumo wa sheria na haki unafanyakazi yake tu pale siasa zinapotenganishwa na mahakama, na pale tu wanasiasa, ambao ni waunzi wa mahakama wanapokubali kuhukumiwa na chombo walichokitengeneza wenyewe.

Tatizo linakuja kwamba, makosa mengi ya wanasiasa ni ukosefu wa maadili ya uongozi ambayo ndiyo yanayoficha rushwa na kuifanya rushwa isihukumike kimahakama. Makosa ambayo hayatambuliki na kukubalika kimahakama kama makosa mengine, mfano wizi wa kuku sigara au simu. Kutokubalika kwa mapungufu ya maadili ya uongozi katika mahakama zetu kuwa ni kosa linalohukumika kisheria kunatugharimu sana Tz kuliko wizi wa majambazi wa kutumia silaha. Kumbuka hasara tulizopata Tz kutoka Richmond, TLP, Buzwagi, EPA, nk.

Ni ngumu kukamata wala rushwa kisheria, ni ngumu kimahakama kuwafunga viongozi wanaokeuka maadili ya uongozi na hivyo kuliingizia taifa hasara. Na hii inathibitika kwenye sakata la Richmond, rada, EPA, TLP, Tanesco, na rushwa zinazotawala katika chaguzi mbalimbali nchini. Kwa sababu maadili ya uongozi sio kosa kisheria ingawa ndio linaloigharimu Tz mabilioni ya shilingi kila mungu anapolichomoza juwa lake. Leo hii viongozi walioiba fedha kwa mwavuli wa ukosefu wa maadili ya uongozi wanatamba katika jamii kwasababu wanajuwa worse comes to worst watafukuzwa tu kazi kama akina Muhando au wakishiba na kuvimbiwa wataachia ngazi kama Rostam au kama wana ela za kutosha kutawala idara zote za serikali na chama zilizotakiwa ziwapigie kelele wataendelea kuitesa Tz kama akina Mamvi Meupe.

Kibaya zaidi ni kwamba taasisi za kulinda maadili ya viongozi zinaendeshwa na kuwa na ubia na vinara wa rushwa na upungufu wa maadili ya uongozi. Of course, kwani kutoka kwao ndio taasisi hizo (TAKUKURU, usalama etc) zimeundwa. Mwisho wa siku, wanasiasa ndio mahakama, ndio viongozi wa TAKUKURU, ndio wenyeviti wa kamati za maadili kwenye chama na serikalini. Watapindisha mkondo wa sheria kwa matakwa yao, makosa na wizi wao wote utaonekana hauna ushahidi wa kisanyansi bali ni ukosefu wa maadili ya uongozi ambao gharama yake kwa taifa ni umasikini wa kunuka lakini gharama kwa maharamia hawa ni kujiuzuru kwa hiari, kuendelea na kazi wakisema "ni majungu" au kubadirishwa kazi, au kufukuzwa huku wakipewa lundo la ela ambazo watazitumia kizazi hadi kizazi. Na unashangaa siasa ndio ajira pekee ya uhakika Tz!

Leo mamvi meupe anakemea rushwa akiwa nje ya nchi bila aibu. Lakini let us make a U-turn, kwanini asikemee rushwa wakati hajatiwa hatiani kisheria kwamba alikula rushwa au kuiibia nchi? kwani kujiuzulu ni kukubali kosa? Tukipiga U-turn tena tutaona kwamba anakemea kwasababu anajuwa kwamba mapungufu ya maadili ya uongozi hayashitakiki kisheria na hata kama yangeshitakika ana kila sababu ya kushinda kwasababu ni kiongozi wa mahakimu watakao amua, kwa maana nyingine ukimshitaki unambadirishia kazi tu; kutoka kuwa mbunge kwenda kuwa hakimu wa kuhukumu kesi yake mwenyewe.

Hapa ndipo napofikia kusema kwamba wanasiasa ni budi wawe na mahakama yao. Mahakama ambayo itatumia ushahidi wa kimazingira kuwajibisha vikali viongozi wanao kiuka maadili ya uongozi. Kwenye mahakama hii hakuta kuwa na kitu kinaitwa rushwa bali mapungufu ya maadili ya uongozi kwasababu ni rahisi kugundua mapungufu ya maadili ya uongozi kuliko kukamata wala na wapokea rushwa. Kwenye mahakama hii, hatutahitaji ushahidi wa kisayansi kumfukuza na kumfilisi kiongozi atakayeonekana amekeuka maadili ya uongozi. Adhabu za mahakama hii ni mbili tu: kufukuzwa kazi na kufilisiwa. Mahakimu wa mahakama hii wachaguliwe na wananchi, na wadumu kwa mwaka moja tu.

Naamini hili ndio suluhisho la rushwa inayotugharimu Tz. Viongozi wataanza kujiona wana dhamana, wataogopa siasa kwasababu kinga ya "kisayansi" ya wizi wao itakuwa imeondolewa.

Ningependa kusikia kutoka kwa wana JF wengine juu ya hili.
 
nakubalina nawe ! Japo nafikiri hata hizo mahakama za wana siasa zinaweza zisisaidie maana shida si majina ya mahakama bali uhuru na uthubutu wa mahakama kuota meno ya chuma na sio meno ya barafu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom