Ili tufike Uchumi wa Kati shirikishi tunapaswa kufanya nini?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,506
Ndugu wananchi,

Kama taifa lazima tuwe na dira na Mipango. Marehemu Mzee Mkapa alitamani kwamba ikifika mwaka 2020 ba Pato la Mtanzania liwe limefika USD 3000. Niseme tu kwa wale ambao sio wafuatiliaji wa Mambo kwa sasa GDP per Capita ni USD 1080 Ila tukitumia mfumo wa PPP (Purchasing Power Parity) basi GDP Per Capita imeshafika USD 3000+

Sasa ili kuweka sawa kumbukumbu ni lazima tujue tofauti ya GDP Per capita na GDP per Capita(PPP), hili ninakupa wewe msomaji kazi ya kutafuta na kuweka katika comment hapa chini. Yatosha kusema kwamba GDP (PPP) inaonesha uhalisia wa hali ya uchumi kuliko nominal GDP ambayo ndo hasa tumeambiwa ni 1080.

Sasa nirudi kwenye hoja yangu ya msingi kuhusu ni nini tufanye ili tuweze kufikia Nominal GDP ya USD 3000 kwa mwaka 2025.

Kwanza kabisa lazima tuanze kufanya zoning (yaani tufanya mipango yetu kwa msingi wa Kikanda) ambapo tunaweza kugawa taifa letu katika kanda 7 ambapo katika kila kanda tunakuwa mega city moja -Satelite Cities Tutakazojenga
Katika kila zone ziweka kama ifuatavyo:

1. Eastern Zone tuwe na Mega City Tabora
2. Southern Highland Mega City iwe Mbeya
3. Lake Zone Mega City Iwe Mwanza
4. Northen Zone iwe Arusha
5. Eastern Zone iwe Pwani
6. Southern Zone iwe Lindi
7. Central Zone iwe Dodoma

Hizi mega cities zizungukwe na other cities ambazo zinatakiwa ziwe katika radius ya km 250-350 kila upande. Kila mega city iwe na population isiopungua watu milioni 3 na wasiozidi milioni 10.

Lite cities ziwe na agro production zone, industrial production zone, tourism zones, technology zones, educational zones(yaani maeneo yatengwe maalumu kwa ajili ya shughuli za kilima, viwanda, utalii, technology na elimu)

Haya Maeneo yawe self sustaining kwa maana ya kwamba uzalishaji wowote unaofanyika katika maeneo haya ukidhi mahitaji ya eneo husika na kuzidi.

Utengenezaji wa hizi programs utumie mfumo wa PPP (Public Private Partnership) ambapo baada ya kuundwa kwa hizi zones basi zipewe mamlaka ya kuraise funds katika bonds market local na international ili ku-finance miradi hii mikubwa.

Najua kuna ambao nitawaacha solemba kwenye huu mjadala, ila najua pia kuna ambao wataelewa. Kama wewe ni Mtunga sera hebu angalia kama huu mradi unawezekana ili tuanze kwa kuangalia yale maeneo ambayo bado yako nyuma kimaendeleo tuanze kutekeleza huu mradi wa zoning kisha tukifanikiwa ndo tunakuja huku ambako kumeshapiga hatua tuanye maboresho.

Karibuni kwa Mjadala
 
Iyo ni Chinese Growth Appoach na imefanya kazi vizuri sana.

Umeiweka vizuri sana.

Hapa ungeongelea zaidi namna Central Government itavofanya kazi na huu Muundo kwa sababu Nguvu yote ya uchumi inaenda kwenye Zones.

Tahadhari ya hii model ni kumeguka kwa nchi ikiwa politics zitayumba.

But kuna model nzuri zaidi na Rafiki kuliko hii ambayo ilitumika na Germany...hii tunaweza kuifikiria...

Nadhani kinachohitajika hapa kwetu ni Creation ya Commercial investment ktk Kilimo(Settlers)-Masettler 50 mpk 100 kila Zone pamoja na integrated factories.
Central Bank inapaswa kuona hili inawezekana kwa sababu ni Mapinduzi ya sayansi ya Kilimo.

Mapping ikifanyika vizuri ktk Kilimo na Mifugo na adoption ya High tech ikawepo-Tunaweza kupanda upesi sana kufikia GDP ya 5000Usd ndani ya 5yrs to come.

Model nyingine ni kubadili Value ya Uchumi wetu kutoka kwenye paper(Notes)Kwenda kwenye Stones-Mfano pale Dubai value ya Economy yao iko kwenye Gold na wameweza kustahimili sana licha ya nyakati za mtikisiko wa kiuchumi.

Bank zikubali wananchi wadeposit stones kama value ya economy yao...Transformation ya Minerals acts pamoja na processing technology inahusu hapa....
 
ndugu, umeongea ya maana. Ila kutumia model ya public private partnership - ppp hatuwezi chomoka hata kidogo...

Hii njia ya PPP ndio njia itakayotufanya tuwe ( kama nchi) watumwa kwa private investors na kesi hazitaisha huko ISDS na akina Miga ya Tundu Lissu...
Itoshe tu kusema kwamba kwa sasa namalizia kuandika PhD kuhusu hiyo kitu - public private partnership- comparative analysis (for the past 100 years) in both civil and common law jurisdictions.
Sasa ukichukua time factor (20-30 years); ukachukua cost performance; risk factor; good/best value money v social value ; jibu ni moja tu, hizi PPP ni kichaka cha ujambazi wa kuwaibia wananchi kodi zao...

Miaka 20-30 pekee ni kama chaguzi 5+ ( yaani magufuli watano); ikiwa kila serikali ina vipaumbele vyake, na kila bunge ndani ya serikali na vipindi hivyo zaweza kutunga na kubadili Sheria za nchi, maana yake itafika siku wananchi kufanya revolutin na kuikataa mikataba ya Muda mrefu kama hiyo ya PPP. Hilo likifanyika, litapeleka mwangi kwa private investors duniani na tukapewa figusu kama za Zimbabwe...

cha kufanya:
1 . Tuamue vipaumbele vichache vitakavyoleta maanufaa mengi kwa umma
Mfano- tukiamua kutomeza tatizo la njaa na chakula bora ndani ya miaka 2.5 - hilo limo ndani ya uwezo wetu; tatizo la maji na nishati pia liwe historia...Elimu bora kwa kila Mtoto - tunaweza pia.

2. Tukiamua kutandaza reli nchi nzima kidogo kidogo kutumia vyanzo vya ndani - hilo pia tunaweza- mfano kuanzia lottery ambayo kazi yake ni hii tu - kujenga reli- tunaweza mfano ni Ethiopia waliotumia lottery kujenga bwawa lao kubwa la umeme .

3. Kuhakikisha kwamba kila mtu analipa kodi kwa kila kitu anachofanya kwa kadri ya matumizi yake- hata mama ntilie- hilo pia tunaliweza.

4. Kusimamia kwa ufasaha na kwa endelevu miradi yote kwa kuweka management ya ukakika- hilo nalo limo ndani ya uwezo wetu...hata kama management hiyo itakuwa na raia wa kigeni ni sawa tu.. ili mladi watupe results tunazotaka...

5. Kushirikisha na kuhimiza watanzania wote hata wa huko nje ya nchi kujihusisha na maendeleo ya nchi yetu- isitoshe tu kuwapa passport na wakiondoka basi hakuna anae wajua- twaweza tumia mfano wa Philippine kwa kuwatoza kodi Maalum raia wao wanapoingia na kutoka ndani na nje ya nchi..

6. Kupanua wigo wa kodi Mara mbili ya sasa ili kuhakikisha nchi nia fedha za kutosha kufanya mambo yake bila kutegemea wahisani.

7. Kodi zote na mambo yote ya fedha yafanyike kupitia bank - hata mishahara ya makondakta wa daladala na wafanyakazi wa ndani pia ipitie Bank- yaani bank na makampuni ya siku ndio ziwe TRA ya kukusanya kodi ya serikali...

Ni mengi ya kufanya lakini muhimu tuache hii tabia ya kuimba wimbo- tunakopesheka. Ni wa fedheha sana... tangu lini mtu ukafurahie kuwa na deni au kukopesha?

Ili tuendele, ni lazima tuwashirikishe wananchi wote kuamua ni maendeleo yapi wanataka, vipaumbele vipi wahahitaji...etc na jasho la kazi wa usiku na mchana halikwepeki...tuache uvivu wa kutegemea ajira za serikali na serikali pia iache tabia ya kutoa ahadi zisizo tekelezeka...
 
Kinachonifurahisha zaidi na huwenda tukafanikiwa Kwa haraka, ni pale tuapojaribu kuzungumzia swala zima la Uchumi wetu, kwamba ni nini kifanyike ili tufike

Nadhani hii ndio njia sahihi ya mtu yeyote mwenye lengo la kutoka mahali alipo na kusogea

Cha msingi ni zile shabaha zifuatwe, na tukidhamilia kwa dhati tunafika mapema zaidi, jambo la msingi baada ya kuwa tumeamya, mtu yeyote anayejaribu kuturudisha nyuma aonwe kuwa ndiye adui no moja, ashughurikiwe kimyakimya, kiundwe kikundi kitakachodili na hao wajinga

Tusitaniane, nchi za wenzetu, Wakati wa kuyaendea malengo ya nchi zao ya kupiga hatua za kiuchumi!, kuna waliokuwa wahuni serikalini, wanasiasa uchwara, walishughurikiwa bila aibu, hii ni Sawa na kusema, unyasi mmoja ukidondoka kwenye nyumba, nyumba haiwezi kuvuja

Sisi, Tanzania, Mungu ametubariki tunawatu wazuuri mno wakikaa wakaandaa mpango wa namna ya nchi Yetu kupiga hatua kiuchumi, tatizo letu halipo hapo, tatizo letu wengi wetu si wazalendo

Swala lingine,Tunapoamua kujenga Uchumi wetu kama NCHI, ni mhimu kuwepo na ushirikishwaji wa watu na Kada zote kutoka katika sectors zote, vyama Vyote n.k
 
7. Kodi zote na mambo yote ya fedha yafanyike kupitia bank - hata mishahara ya makondakta wa daladala na wafanyakazi wa ndani pia ipitie Bank- yaani bank na makampuni ya siku ndio ziwe TRA ya kukusanya kodi ya serikali...
Big up" hii ndio itakayofanya mapato ya Serikali kuongezeka mara dufu
 
Cha msingi ni zile shabaha zifuatwe, na tukidhamilia kwa dhati tunafika mapema zaidi, jambo la msingi baada ya kuwa tumeamya, mtu yeyote anayejaribu kuturudisha nyuma aonwe kuwa ndiye adui no moja, ashughurikiwe kimyakimya, kiundwe kikundi kitakachodili na hao
Hapa ndo Kuna shida kubwa. Mfumo mzuri ni wengi wape na wachache wasikilizwe. Mawazo mbadala hata kama hatukubaliani nayo yanatolewa kwa nia njema, badala ya kuyatafakari kwa kina, tunakimbilia kuona wengine maadui na kuunda vikundi vya wasiojulikana kuteka na kuuwa kimya kimya!

Sisi, Tanzania, Mungu ametubariki tunawatu wazuuri mno wakikaa wakaandaa mpango wa namna ya nchi Yetu kupiga hatua kiuchumi, tatizo letu halipo hapo, tatizo letu wengi wetu si wazalendo
Uzalendo unapatikana vipi kama hao wengi hawasikilizwi??
 
1 . Tuamue vipaumbele vichache vitakavyoleta maanufaa mengi kwa umma
Mfano- tukiamua kutomeza tatizo la njaa na chakula bora ndani ya miaka 2.5 - hilo limo ndani ya uwezo wetu; tatizo la maji na nishati pia liwe historia...Elimu bora kwa kila Mtoto - tunaweza pia.
Upo sahihi mkuu tusiende na mambo mengi kwa mkupuo tuangalie vipaumbele ambavyo tunaweza kuvitekeleza kwa uwezo binafsi then tunajipa muda flani kutekeleza then tunaenda hatua inayofuata naamini tutafika mapema tu uchumi wa kati.
 
Hayo ndio tunatakiwa kufanya kama nchi, kushika mambo mengi kwa muda mchache tutakwama tu...pia tujenge mifumo ya uwajibaji na kutoa haki panapo stahili na utamaduni wa keheshimu vya kwetu, kuvilinda na kuvitunza... labda tufike mwisho pia tuseme wanasiasa wanaotoa ahadi za uongo watupwe jela kama ahadi hizo hazikutekelezeka, hii itasaidia wawe makini na wanancho ahidi...
 
My opinion kwenye hili, ni kwamba bado tupo kwenye right direction, kufikia huo uchumi wa kati USD (3000).
Pale alipo tuacha JK uchumi wetu ulikuwa unaelekea kuwa stagnat.
1. UMEME
Tusingeweza kuendelea tena kiuchumi, kwa umeme ule wa majenereta, umeme wa mgao, na umeme ulio kuwa haujafika sehemu kubwa ya Tanzania. So hatuna budi kusuburi kwa miaka miwili kupata umeme wa uwakika na wa bei nafuu, utakao punguza garama za uzalishaji. (MTO RUFIJI)

2. FOLENI DAR
Hii ilikuwa hatari sana 2HRS kwenye foleni ilikuwa kitu cha kawaida sana, hapa pia pana karibu 2 yrs kumaliza foleni DAR.

3. UPANUAJI WA UCHUMI.
Mpango wa serikali kuamia Dodoma pia hii impact yake itakuja kuonekana badaye, tulizoe kila kitu kina Anzia Dar ambako uchumi wake kama ulidumaa hivi, so serikali kuinvest dodoma kunapanua wigo wa uchumi wetu kukuwa kwa kasi.

4. UJENZI WA RELI (SGR)
Hii impact yake pia hatuwezi kuona Leo, lakini ikakamilika, itasaidia sana movement za watu, kwa muda mfupi, na kuongeza uzalishaji, katika sector mbalimbali

5. UJENZI WA BARABARA KUUNGANISHA MIKOA NA WILAYA.
Hili pia lilikuwa tatizo kubwa sana kwa Mikoa na wilaya nyingi kuwa nyuma kimaendeleo, usafirishaji ulikuwa tabu sana. Hili pia likikamilika kwa asilimia 100.
5 years ijayo tunaweza kufanya Maajabu katika uchumi wetu.

5. KUENDELEA KUDHIBITI UFISADI
Hili pia likidhibitiwa vizuri litasaidia sana kuyatekeleza hayo yote hapo juu.

Tatizo la nchi yetu lilikuwa ni miundo mbinu, ya kiuchumi ilikuwa ovyo sana, muda mwingi tuliwekeza kwenye sera za kiuchumi, wakati miundo mbinu ya kutekereza hizo sera hakuna, ndio maana kila tulicho kuwa tunakipanga kilikuwa kina fail, kwa sababu ya hizo changamoto hapo juu.
 
Hayo ndio tunatakiwa kufanya kama nchi, kushika mambo mengi kwa muda mchache tutakwama tu...pia tujenge mifumo ya uwajibaji na kutoa haki panapo stahili na utamaduni wa keheshimu vya kwetu, kuvilinda na kuvitunza... labda tufike mwisho pia tuseme wanasiasa wanaotoa ahadi za uongo watupwe jela kama ahadi hizo hazikutekelezeka, hii itasaidia wawe makini na wanancho ahidi...
Na pia bungeni kuwekwe utaratibu wa wabunge kusaini pale wanapopitisha miswada ya sheria mbalimbali na mikataba ya serikali ili baadae ikija kugundulika kuna upigaji au mikataba mibovu wawajibishwe wote waliopitisha.
 
Kinachonifurahisha zaidi na huwenda tukafanikiwa Kwa haraka, ni pale tuapojaribu kuzungumzia swala zima la Uchumi wetu, kwamba ni nini kifanyike ili tufike

Nadhani hii ndio njia sahihi ya mtu yeyote mwenye lengo la kutoka mahali alipo na kusogea

Cha msingi ni zile shabaha zifuatwe, na tukidhamilia kwa dhati tunafika mapema zaidi, jambo la msingi baada ya kuwa tumeamya, mtu yeyote anayejaribu kuturudisha nyuma aonwe kuwa ndiye adui no moja, ashughurikiwe kimyakimya, kiundwe kikundi kitakachodili na hao wajinga

Tusitaniane, nchi za wenzetu, Wakati wa kuyaendea malengo ya nchi zao ya kupiga hatua za kiuchumi!, kuna waliokuwa wahuni serikalini, wanasiasa uchwara, walishughurikiwa bila aibu, hii ni Sawa na kusema, unyasi mmoja ukidondoka kwenye nyumba, nyumba haiwezi kuvuja

Sisi, Tanzania, Mungu ametubariki tunawatu wazuuri mno wakikaa wakaandaa mpango wa namna ya nchi Yetu kupiga hatua kiuchumi, tatizo letu halipo hapo, tatizo letu wengi wetu si wazalendo

Swala lingine,Tunapoamua kujenga Uchumi wetu kama NCHI, ni mhimu kuwepo na ushirikishwaji wa watu na Kada zote kutoka katika sectors zote, vyama Vyote n.k
Ningeshangaa usingekimbilia kusema kuna watu si wazalendo, wanao kua kinyume au kuturudisha nyuma washughurikiwe...apa imeonyesha dhairi kua umekua mshiriki wa vitendo hivyo.
Ngoja kidogo nije nichangie mada vizuri ingawa niliwai kuileta na kuchangia pia
 
Mleta mada hii ahsante sana kwa kuliona kua tuhitaji uchumi wa kati ingawa huko nyuma tumeambiwa tayari tumefika iwe basi tujadiri uchumi wa juu.
Mwisho uwezi kufanya hivyo kwenye uchumi bila ya kua na sera imara na Serikali imara na inayo wajibika pamoja na falsafa ya Taifa ambayo ni imara.
 
Back
Top Bottom