Waliofuta AZIMIO LA ARUSHA kule Zanzibar ndio wameliingiza Taifa katika Utumbuaji Majipu.Namwonea huruma Rais wangu Magufuli kwani kazi iliyombele yake ni kubwa mno.Wengi waliomzunguka nakumsifia kwa utumbuaji majipu hao hao ndio waliotengeneza majipu hayo wengine wapo ndani ya chama CCM hata Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere baada ya Uhuru waliibuka wenzake waliopigania nae uhuru wenye roho za kibepari ndio akamua kupitisha AZIMIO LA ARUSHA hivyo akatenga kazi ya kutumikia wanainchi na biashara.Kwa vile leo Mh.Rais hawezi kurudisha AZIMIO LA ARUSHA nafasi aliyonayo ni kusimamia KATIBA MPYA ili yale anayoyaona waliomtangulia walishindwa yeye ayasimamie kwa dhati ili Tanzania tuepuke matusi ya kina DONALD TRUMP kwamba viongozi wa Afrika wameshindwa kuongoza kazi yao ni kunyonya waafrika wenzao.Pia Rais wangu awe makini na viongozi waliomtangulia ambao wamejiingiza katika biashara wanaweza kuwa kikwazo katika nia yake ya kutumikia Watanzania.Mungu ibariki Tanzania.