Ili Tanzania iendelee, nchi hii igawanywe mara tatu zipatikane nchi tatu tofauti, au tuwe na sera ya majimbo yenye kujitegemea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Nchi hii ina resources nyingi sana ambazo kama zingetumika vizuri, basi kila eneo la nchi hii lingeweza kufaidika na utajiri wa maliasili unaolizunguka ila bahati mbaya nchi hii imekuwa kubwa na mgawanyo wa kinachopatikana kutokana na maliasili zetu huamuliwa katika mji mmoja (Dar-es-Salaam) hivyo kupelekea mgawanyo mbovu wa kile kinachopatikana kutokana na maliasili zilizopo katika kila eneo la nchi hii.

Mfano mzuri ni gesi iliyopatikana huko kusini ambayo ni namna gani itumike uamuzi ulifanyikie Dar-es-Salaam na matokeo yake leo kila mtu ni shahidi.

Tungekuwa na sera ya majimbo, basi Jimbo la kusini(kama lingeiwa hivyo) saa hizi huenda lingekuwa ni moja ya Jimbo linalonufaika sana na utajiri wa gesi ya kusini na pia Jimbo hilo lingekuwa linachangia mapato makubwa kwa serikali ya shirikisho.

Leo hii tunalia ukosefu wa madarasa kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza ingawa Halmashauri zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini zinakusanya mapato ya kutosha ila kwa utaratibu uliopo sasa tunaambiwa wakubwa walioko Dar-es-Salaam ndio wanaochukua mapato hayo na kuamua ni kiasi gani kirudishwe au hizo fedha zitumike vipi huko katika Halmashauri ambako fedha husika hukusanywa.

Sasa kwa nchi yetu ilivyo kubwa na kwa mgawanyo mbovu wa kinachopatikana katika kuhudumia maeneo mbalimbali ya nchi na watu wake, matokeo ndio haya tunayoyaona leo hii.

Hii nchi ni kubwa na ili kila eneo la nchi hii liweze kupiga hatua kutokana na rasilimali zinazopatikana katika eneo husika pamoja na makusanyo mengine yanayokusanywa kutoka katika biashara zilizopo katika eneo husika, ni wazi inahitajika decentralization ya hali ya juu zaidi (sio hii ya kupitia serikali za mitaa kwa maana ya Halmashauri zilizopo) vinginevyo itatuchukua miaka mingi kupiga hatua kama nchi hasa kwa baadhi ya maeneo ingawa yana rasilimali za kutosha.

Jambo lingine inawezekana hii nchi ni kubwa kuliko uwezo wetu wa kuiongoza na kuitawla hivyo inaweza kugawanywa katika vinchi vidogovido kadhaa vitakavyoweza kutawaliwa vizuri zaidi na nchi hizo zikawa na maendeleo makubwa tu ya watu wake na ya nchi zenyewe.

Aidha, naamini tukiwa na serikali za majimbo, tunaweza kuwa na ushindani wa maendeleo baina ya majimbo na hali hii inaweza kuwa ni moja ya kichochea cha maendeleo kwa nchi nzima.

Naelewa uamuzi kama huu utakuwa na faida na hasara zake, ila kwa nchi yetu hii, naamini faida zitakuwa nyingi zaidi kuliko hasara na tutapata maendeleo kwa hara zaidi kama nchi na standard ya maisha ya watu pia itaboreka.

Watanzania wapewe fursa ya kuamua aina hii ya kujitawala kupitia kura ya maoni ila kwanza wapewe elimu juu ya hili kabla ya kupiga kura.

Ni mtazamo kutokana na hali yetu tukiwa na miaka zaidi ya hamsini ya kujitawala.
 
..process ya kugawanya nchi itatupotezea muda.

..naamini tunaweza kuendelea bila kuwa na majimbo.

..serikali za majimbo zinaweza kutuongezea gharama za watawala.

..tayari tunazo HALMASHAURI kwanini hazina ufanisi?
 
Naunga mkono hoja..

Kila jimbo liwe na Gavana wake anayechaguliwa na wananchi wa majimbo hayo, kila jimbo liwe linakusanya mapato yake yenyewe na kujipangia matumizi yake, Kila jimbo liwe huru kuwa na baadhi ya sheria zake zenyewe..

Rais abaki kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya usalama na controller wa vyombo vyote vya usalama, Magavana wote wawe wanaripoti kwa Rais.
 
Mkuu, kwa nchi kubwa kama hii suluhisho muhimu na la kipekee ktk kutumia vyema rasilimali zetu ni kupitia uongozi wa majimbo, yakiwa na uhuru kupitia maamuzi ya mabunge yake. Wazo murua kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kujenga madaraja ya kupita juu ya bahari huku maeneo mengine(tena mengi tu) wanatumia madaraja ya miti kuvuka mito,ni matokeo ya nchi kutotawaliwa vizuri.
 
Sera ya majimbo kwa tafsiri ya tamaduni za Africa italeta ubaguzi mkubwa.
Jambo la msingi ni ushiriki wa pamoja katika maamuzi.

Mtu mmoja hawezi kuwa na suluhu ya matatizo ya watu zaidi ya milioni hamsini.
Demokrasia hasa kazi yake ndio hii kuhakikisha mawazo ya watu wengi zaidi yanazingatiwa wakati wa kufanya maamuzi.

Hili linawezekana ukiwa na bunge linalotokana na wabunge wenye ushawishi kwa watu wao na walioaminiwa na kutumwa na watu wao, bunge huru na lenye nguvu.

Structure ya uongozi tuliyonayo ni nzuri kama ingefanya kazi kama ilivyokusudiwa kufanya na kama ingekuwa na watu sahihi kwenye nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujenga madaraja ya kupita juu ya bahari huku maeneo mengine(tena mengi tu) wanatumia madaraja ya miti kuvuka mito,ni matokeo ya nchi kutotawaliwa vizuri.
swala sio daraja la juu ya bahari swala ni faida inayopatikana kwa kufanya ivo nchi haiwezi kufanya jambo lisilo na faida kubwa
 
Serikali ya majimbo ni kuongeza tu gharama ya kuwahudumia wanasiasa wanaokula kwa kazi ya kuropoka tu, kama Halmashauri pre 2015 wakati zinakusanya mapato yake hazikuwa na ufanisi ni nini kitasaidia serikali za majimbo kuwa na ufanisi?

Wanasiasa wanatamani nafasi za kisiasa ziongezwe tu ili na wao wapate uhakika wa mlo ila serikali za majimbo kwa Tz ni hasara tu.
 
Back
Top Bottom