Ili Tanzania iendele inahitaji Uongozi,Rasilimali na Nguvukazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili Tanzania iendele inahitaji Uongozi,Rasilimali na Nguvukazi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Mar 31, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere alianzisha msemo kuwa ili Tanzania iendelee twahitaji ARDHI,WATU,SIASA SAFI na UONGOZI BORA.Vitu vyote hivi vipo hadi leo lakini Tanzania iko nyuma kimaendeleo.Kinachochangia nionyesha kidogo kama ifuatavyo:-
  1. ARDHI - ipo lakini haitumiki ipasavyo kwa kilimo na uwekezaji kwa manufaa ya Wananchi wote.
  2. WATU - wapo lakini hawapatiwi elimu inavyopaswa ili wawe wazalishaji.
  3. SIASA SAFI - Siasa iliyopo si ya kidemokrasia kutokana na ubovu wa Katiba.
  4. UONGOZI BORA - Viongozi waliopo wanatumia Katiba ya viraka kuongoza hivyo hujifanyia watakavyo bila kuwepo nguvu ya kisheria ya kuwawajibisha.

  Hivyo ili Tanzania iendelee inahitaji pia na uchumi imara ili iache kujipendekeza kwa nchi tajiri.
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  watu ndo ukosefu wetu mkubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa....

  Lazima tukubali kuanza upya kwa kuthamini na kuandaa rasilimali watu..
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Ili Tz tuendelee tunamhitaji mtu Dikteta mzalendo mwenye visioni kwa miaka 15 hadi 20 hivi!!!
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Je wewe ulishasoma isimu ya lugha. Ardhi, watu, siasa na uongozi ni ngeli au majina (nouns). Bora, safi ni maneno yanayosifia ngeli au majina.

  Ujamaa ulikuwa ni siasa mbovu. Na uwezi kuwa na siasa mbovu bila ya kuwa na viongozi wabovu.

  Hivyo Tanzania tulichonacho ni ardhi na watu.
   
 5. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Mlishakuwa na Benevolent Dictator kwa miaka 24 na aliacha nchi masikini tu.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu, tungekwua watu tusingeweka vioja kuwa viongozi wetu
   
 7. o

  obseva JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 450
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 80
  Hutuna viongozi bora na tuna siasa chafu.Hivyo wazo la mwalimu halijatimia.
   
 8. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 180
  Hata tungekuwa na vyote vinne mimi siamini kama inatosha kufanya nchi iendelee. Kinachokosekana katika dhana ya Mwalimu Nyerere ni ubunifu na uvumbuzi (innovation and invention). Hii maana yake ni kuwa na uwezo wa kuimudu teknolojia na kuitumia kuibua mawazo mapya na kuyatafsiri katika vitendo. Hili ndilo linalosukuma maendeleo. Watu tunao lakini hatuna aina ya watu wa kuchochea maendeleo. Hapa siongelei viongozi peke yao. Naongelea mimi na wewe. Kama ni elimu kwa sasa hivi wasomi tunao wengi. Shahada za uzamili na uzamivu zimetapakaa kila mahali. Kinachokosekana ni kuzitumia kwa namna inayochochea ubunifu na uvumbuzi. Kwa hili hatupaswai kuitupia lawama serikali peke yake. Bill Gates na mwenzake walipokuja na wazo lililozaa Microsoft walikuwa ni wanafunzi. Walipolijaribu wakaona linafanya kazi hata shule wakaacha. Yaliyofuata ni historia. Tunahitaji watu kama hao.
   
 9. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mahitaji hayo manne ni ya msingi katika jamii inayotaka kuendelea. Mengine yote ni matokeo ya matumizi mazuri ya mahitaji hayo.

  1. WATU: Idadi ya watu wenye uwezo kiafya, kiakili, kielimu wakitumika vyema (kwa ushirikishi, ubunifu na uendelezaji wa mipango yote ya maendeleo inaweza kuleta mabadiliko yanayohitajika. Watu wasio na elimu wala ujuzi hawawezi kusababisha maendeleo ya kasi inayotakiwa. Inabidi nchi iwe pia na watu wenye afya njema, wenye shibe na hivyo kuwa na nguvu za kufanya kazi kwa tija.
  2. ARDHI: Tanzania tumebarikiwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba, madini ya aina mbalimbali, maji yanazunguka nchi nzima. Tuna vivutio mbalimbali vya utalii. Ila vyote hivi haviwezi kuwa na manufaa kama havitaendelezwa kwa umakini, ustaarabu na kwa nia ya kuleta maendeleo yanayotakiwa. Ardhi inayolimwa kwa jembe la mkono haiwezi kuleta tija katika kilimo. Madini yanayovunwa an wageni na kupotelea kwao (mikataba mibovu) haiwezi kuleta maendeleo. Vivutio vya utalii usio tangazwa, usioratibiwa kwa ufanisi haiwezi kuleta tija.
  3. SIASA SAFI: Siasa safi ni pamoja na sera za uendelezaji wa wananchi (kielimu, kiujuzi, kibiashara, kujenga uzalendo n.k.). Sera nzuri za kupambana na rushwa, haki na magonjwa. Sera nzuri za kushirikisha wananchi katika maendeleo yao kwa vitendo. Sera nzuri zinazotoa fursa sawa kwa wananchi wote bila kujali tofauti zao (kwa vitendo). Siasa hizo ndizo zinazoweza kuleta maendeleo yanayotakiwa
  3. UONGOZI BORA: Uongozi bora ni ule wenye nia thabiti ya kuleta maendeleo ya kudumu, kudumisha uhuru, amani na mshikamano. Uongozi unaopambana na maovu yote bila haya. Uongozi unaojua nini kinachohitajika kwa wakati gani kwa Taifa hili ili kufikia malengo inayojiwekea. Uongozi unaoelekeza mipango na kuhakikisha uwazi zaidi ya kutekeleza kila jambo kwa siri. Uongozi wa kidemokrasia, unaochaguliwa na watu bila hila. Uongozi unaoweka maslahi ya Taifa kabla ya maslahi mengine yoyote.
   
 10. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwalimu Nyerere pia alisema "Tanzania tuna adui wakubwa watatu(3) - Maradhi, Ujinga na Umaskini"

  Maradhi yanazidi kutuangamiza yakiwemo Malaria, kifua kikuu, ukimwi na gonjwa la kishenzi na la kijinga kupita yote - kipindupindu!

  Ilituondokane na Umaskini bahati mbaya Ujinga umetuingia! Ubinafsi umeongezeka, na huu ujinga wa kuwaua ndugu zetu maAlbino na vizee vikongwe sijui umetoka wapi! Tunakubali mikataba ya hovyo kuzifanya familia zetu ziishi raha mustarahe huku tunakipiga kidole nchi yote na wananchi wake! Tunawaua Albinos eti viungo vyao vitatuletea utajiri pasipo jasho nk. Tunakimbia vijijini huku asilimia zaidi ya 70 ya wananchi wapo huko - hata wabunge wamehama majimboni mwao na wanarudi kufanya mikutano ya hadhara na wakati wa uchaguzi tuu. Wakifariki huwa sio majimboni mwao, sasa hii ikoje???

  Matokeo yake tunapiga kwata hapa hapa hatuendelei! Kaaazi kwelikweli!!!
   
Loading...