Ili mfike mbali kimahusiano na yawe yana tija, inatakiwa robo tatu (3/4) ya matarajio yenu yawe yanafanana

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,189
39,953
Mahusiano sio kitu rahisi

Wengi wanaamini kufanya tendo la ndoa ndio mahusiano, hilo si kweli; mahusiano ni zaidi ya tendo.

Mahusiano ni sawa na kuunganisha kampuni A na B, zenye mitazamo tofauti, na hatimaye kujiwekea makubaliano kwa vile vitu mnavyofanana na kutengeneza kampuni mpya C.

Mfano:-
Kampuni A (mwanaume)
  • Anapenda mwanamke mnene
  • Anapenda mwanamke muongeaji
  • Anapenda mwanamke mrefu
  • Anapenda ucheshi
  • Hapendi kuombwa hela
  • Anapenda sana tendo la ndoa
  • Anapenda usafi
  • Anapenda kuajiriwa
  • Ana utu katika kujali
  • Anapenda kuvaa nguo za kizee n.k
Kampuni B (mwanamke)
  • Anapenda mwanaume mrefu
  • Anapenda mtu mcheshi
  • Anapenda mwanaume mwembamba
  • Anapenda kupewa hela
  • Anapenda kujiajiri
  • Hana utu anajali pesa zaidi
  • Hapendi tendo la ndoa
  • Anapenda mwanaume mtanashati n.k

Hizi pande mbili (kampuni A na B), zikitaka kuungana, kuna vitu itabidi pande zote wakae chini na wakubaliane na kutengeneza kampuni ya pamoja C (mwanaume +mwanamke), kama tofauti itakuwa ni kubwa, uhusiano hautadumu.

Kwa mfano wetu hapo juu, pande zote mbili zinatofautiana sana, na kama watalazimisha mahusiano, hayatafika mbali; kwa sababu vitu vingi wanatofautiana.

Ili mfike mbali kimahusiano na yawe yana tija, inatakiwa robo tatu (3/4) ya matarajio yenu yawe yanafanana; lakini kama mwingine anataka kumgeuza mwingine mzazi/sponsor, hapo hakutakuwa na mahusiano.

Na haya utayajua pale mwanzoni, utakapomwambia kila mmoja aorodheshe matarajio yake angalau kumi kwenye karatasi, baada ya hapo mnajipima; mkiona kuna tofauti, achaneni mkapambane na vitu vingine.

NB: Waliodumu muda mrefu kwenye mahusiano, miaka 10+ wana vitu vingi vinavyoingiliana.[/JUSTIFY]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom