Ili Kuzamia Marekani Wajificha Kwenye Baridi Kali Ndani ya Friza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili Kuzamia Marekani Wajificha Kwenye Baridi Kali Ndani ya Friza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wahamiaji holela 97 wakiwa wamejificha kwenye friza Friday, August 28, 2009 5:11 AM
  Ili Kuzamia Marekani kwa matumaini ya maisha bora, wahamiaji holela 97 kutoka nchini Mexico walikutwa wakiwa wamejificha kwenye friza wakistahmili baridi la nyuzi joto moja. Polisi wa Arizona, Marekani walipigwa na butwaa baada ya kulisimamisha gari la mizigo inayosafirishwa ikiwa kwenye friza na kukuta ndani wahamiaji holela 97 wakiwa wamejificha ndani kwenye baridi kali la nyuzi joto moja.

  Wahamiaji hao 97 watu wazima na watoto waliweza kulistahmili baridi kali sana la ndani ya friza ambalo pia lilikuwa limewekewa mizigo mingine mbali mbali.

  Wahamiaji hao walikuwa wakitokea nchini Mexico na Guatemala na walikamatwa maili chache kutoka kwenye mpaka wa Mexico na Marekani.

  Wahamiaji hao holela walikabidhiwa kwa maafisa wa uhamiaji wa Marekani ambao walianza taratibu hapo hapo za kuwarudisha nchi zao walizotoka.

  "Hawa watu walifanywa kama mizigo. Waliwekwa ndani ya gari hili kwenye hali ya baridi ambayo wangeweza kuganda" alisema Matthew Allen, afisa maalumu wa uhamiaji wa Arizona.

  "Kufuatia kazi nzuri ya polisi kulisimamisha gari hili, maisha ya wahamiaji hawa holela yaliokolewa".

  Arizona inatumika kama njia kuu ya kupitisha wahamiaji holela na madawa ya kulevya kuingia Marekani kutokea Mexico.

  Mwaka jana polisi wa uhamiaji waliwakamata watu 705,022 wakijaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kutokea Mexico.

  Idadi hiyo ya mwaka jana ndio idadi ndogo ya wahamiaji holela waliowahi kukamatwa tangia miaka ya 1970.
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  hiyo freezer lazima ilikuwa off- hata hao buddhist monks hawawezi kuhimili baridi hilo-we call this over the top news
   
Loading...